Historia ya Kadi ya TANU 1954

Historia ya Kadi ya TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HISTORIA YA KADI YA TANU 1954
Ndugu yangu mmoja kanirushia kadi ya TANU nami kwa kuonyesha shukurani yangu kwake namuwekea hapo chini historia ya kadi ya TANU kama nilivyoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake.
Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika.

Mfano wa kadi ya TANU ulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion.
Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.

Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA) alichapisha kadi nyingine 2000.

Ally Sykes alikuwa Secretary wa TAGSA.

Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa.

Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo.

Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na John Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Faizi Mafungo kadi nambari 24; Iddi Tosiri kadi nambari 25.''

Picha ya Ally Sykes na Julius Nyerere miaka ya mwanzo ya kuunda TANU.

333019004_552290563668740_5734716338504326809_n.jpg

332259949_1944711935880049_5271359357458178289_n.jpg

332746523_100664599636330_8092948801434138592_n.jpg

Kulia Ally Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere miaka ya mwanzoni ya kuunda TANU​
 
Back
Top Bottom