Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
HISTORIA YA KANISA LA AYA SOFIA
Kanisa Lililogeuzwa Kuwa Msikiti Baada ya Kutekwa kwa Mji wa Konstantinopoli
Kanisa la Aya Sofia, lililojengwa wakati wa Ufalme wa Byzantine, lilikuwa ni miongoni mwa majengo muhimu zaidi ya kidini katika historia ya Ugiriki ya zamani. Mji wa Konstantinopoli, uliokuwa sehemu ya Ugiriki, sasa unajulikana kama Istanbul. Baada ya ushindi wa Ottoman mwaka 1453, mji huu ulitekwa na Sultan Mehmed II, ambaye aliubadilisha kanisa la Aya Sofia kuwa msikiti.Masjid Aya Sofia
Alhamdulillah! Baada ya miaka 85 ya kuwa makavazi ya kimataifa huko Uturuki, leo hii korti kuu imebatilisha hukumu hiyo na kurejesha hadhi yake ya kuwa msikiti.Ni siku kama ya leo ya Ijumaa ambapo Sultan Muhammad al-Fatih (RA) alifungua mji wa Konstantinopoli (Istanbul). Aliingia katika mji huo akiwa juu ya farasi wake pamoja na jeshi lake, huku makomanda wake wakimpongeza na kumwambia, "Umekuwa mkombozi wa Konstantinopoli ambaye Mtume wa Allah (SAW) aliyetutabiria."
Kisha alishuka juu ya farasi wake na kupiga sijdah ya kumshukuru Allah SWT kwa kumpa hadhi hiyo na kuwaombea dua mujahidin waliokufa katika vita hivyo vya ufunguzi. Alipoinuka, alielekea kwenye majengo ya Aya Sofia, ambapo mwanzoni ilikuwa kanisa. Ndani yake kulikuwepo makasisi ambao Sultan Muhammad al-Fatih aliwaonyesha upendo na amani, na kuwaahidi kuwahifadhi maisha yao na mali zao ndani ya mji huo. Hadi tarehe inasema, wengi wa Wakristo hao walisilimu kwa kuona haki na maridhiano ya Uislamu.
Baada ya hapo, Sultan Muhammad alitoa agizo la kubadilisha kanisa hilo kuwa msikiti ili Waislamu wajitayarishe kuswali swala ya Jumu'ah hapo. Waislamu walianza kusafisha majengo hayo kwa kuondoa misalaba na masanamu yaliyokuwemo ndani, kisha ikajengwa mimbar ambayo Shaykh Shamsuddin alipata sharaf ya kutoa khutba ya kwanza humo ndani.
Aya Sofia Kugeuzwa Kuwa Makavazi na Kurudishwa Kuwa Msikiti
Tangu siku hiyo, Aya Sofia ilikuwa msikiti hadi mwaka 1935, wakati Mustafa Kemal Atatürk (Baba wa Taifa la Uturuki) alipoamrisha baraza lake la mawaziri kubadilisha msikiti huo kuwa makavazi na kupiga marufuku Waislamu kuswali humo ndani. Baada ya miaka 85, leo hii sheria hiyo imebadilishwa na kurudishwa tena kuwa msikiti.
