Historia Ya KARL MARX


Shukrani sana, kweli JF ni kisima cha kujifunza
 
Marx alikufa katika hali ya umasikini uliobobea. Maandishi yanasema kuwa mpaka wakati anakaribia kufa alikuwa akiishi kwa kuomba msaada wa senti na chakula kutoka kwa rafiki yake Friedrich Engels.
Alikuwa anafukuzwa katika kila nchi aliyojaribu kuweka makazi kutokana na kuanzisha aina ya uasi wa fikra zake za class struggle. Kuna wakati alipata kuwa Editor ktk vyombo vya habari kadha, lakini vyote vikaishia kufungiwa na bourgousie(neno hili limenitesa miaka yote) kutokana na bitterness ya articles zake!
 

Tofauti ya socialism na capitalism iko katika mitazamo mingi mfano,
1. Socialisim - Based on public ownership of major means of production. While capitalism based on private ownership of major means of production.
Ziko nyingi tutapata wasaa wa kuzichambua tukifika kwenye historia ya Russia revolution huko tutajua zaidi kuhusu ujamaa toka enzi za Utopian Socialism.
Pia siasa za ujamaa za mwalimu nyerere lilikua ni wimbi la matokeo ya Scientific socialism hasa baada ya Chinese revolution ya mwaka 1949 ndipo Nyerere na mataifa mengine yakaamua kuchukua siasa ya ujamaa, mfano Uganda kulikua na Common mans charter under Obotte, Libya kulikua na Islamic socialism under Gaddafi, zilikua nyingi.

Nadhani utakua umepata idea ya haya mambo. Naahidi kuzungumzia socialism kwa kirefu siku zijazo.
 
Samahani mkuu nilisahau kuzungumzia swali lako kuhusu V.I Lenin, huyu alikua ni kiongozi wa mapinduzi ya Urusi Octer reveolution ya mwaka 1917 na alifanikisha haya kwa kufuata miongozo ya Karl Marx na yeye pia aliandika mungozo wake ulipewa jina la The April thesis aliandika alipokua akiishi uhamishon Uswisi. Alitawala USSR tangu mwaka 1917 baada ya mapinduzi na alikufa mwaka 1929 ndipo USSR ikaangukia mikononi mwa Joseph Stalin.
 
Nakumbuka kidogo theory of surplus value na mambo fulani fulani..long time.. ila mwalimu wangu aliniambia eti alikufa kwa kipindupindu!! Na sikumbuki kama nilimuuliza je wakai huo kilikuwepo?

Hapana, mwalimu huyo alikudanganya; Marx alikufa kwa ugonjwa wa kawaida (inasemekana kansa ya ini), siyo kipindupindu. Aliugua kwa takriban miaka mitatu kuanzia kifo cha binti yake na mkewe ambao pia walikuwa wamekufa kwa kansa ya ini. Kipindupindu kisingedumu mwilini mwake kwa muda huo wote.

Ingawa alikuwa akiishi maisha ya kimaskini sana, inabidi tukumbuke pia kuwa hakuwa fukara. Alikuwa mwandishi mashuhuri wa magazeti na vitabu mbalimbali, ambavyo ingawa vilikuwa havipendwi na bourgeoisie, vilikuwa vinapendwa sana na proletariat. Matatizo makubwa ya Karl ni kwa sababu alikuwa hawezi kukaa sehemu moja kwa amani, kila mara alikuwa akiingia matatizoni na hivyo kuwa anashindwa kustabilize.
 
akina kubenea wameanza kitambo kumbe
 
Vitabu vyake hivyo vinapatikana bure Google- books; nimeweka kimoja hapa kwa anayetaka kukipitia. Nitaleta kingine baadaye nikishanikiwa kupunguza ukubwa wa faili. Vitabu hivi vilikuwa ni sehemu ya DS100 UDSM miaka ya themanini.
Mkuu nashukuru sana kwa kutuwekea soft copy.Mimi ninayo hard copy tu kwa hiyo umetusaidi sana, ubarikiwe
 
nashukuru mkuu kweli nipo darasani naendelea kusubiri mazuri zaidi mkuu
 
ni kweli karl marx alikufa kwa umaskini mkubwa na alikufa hivyo kwa sababu idea zake hazikubalika wakati huo naye pia hakukubalika. hivyo kumfanya aishi kwa shidashida.
lakini badae watu walianza kuzifwata na kuona zina mashiko wengine walifanikiwa wengine walishindwa.waandishi wengine wakazimodify wangine walizipinga.ila kwa kweli alieleza mambo ya kweli na kina.haswa katika namna gani watu waishi na jinsi ubepari ulivyokuwa na unyonyaji.
 
marx alitoa mchango mwingi katika yafuatayo
uzalishaji,jamii,dini,sheria,na sayansi.
 
Kwa jinsi nnavyofuatilia mlolongo wa mjadala huu inawezekana tukaingizana chaka au watoto wa mujini wanasema tunaweza kulishana sumu mchana kweupee kwa sababu huyu anasema hiki anachokifahamu alafu anakuja mwingine anasema kingine anachokijua ambacho ni maelezo tofauti na ya mwanzo. Mwingine anakuja na story huku akisema "kama sijakosea" nyingi kiasi cha kutia wasiwasi kuhusu asemacho.
Maada ni nzuri ila mkanganyiko unaojitokeza unaweza kutuharibia historia nzima tunayotaka kuijua. Let us be careful on this
 
Vitabu vyake hivyo vinapatikana bure Google- books; nimeweka kimoja hapa kwa anayetaka kukipitia. Nitaleta kingine baadaye nikishanikiwa kupunguza ukubwa wa faili. Vitabu hivi vilikuwa ni sehemu ya DS100 UDSM miaka ya themanini.
Katika vitabu vyote vya Karl Marx nakipenda Das Kapital,
 

Mkuu usiwe mvivu was kusoma ingia Google kila kitu kipo
 
Jaribu kupitia tena kwenye wino mwekundu. inachanganya kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…