Historia ya kutisha kuhusu kuzika watu wakiwa hai

Historia ya kutisha kuhusu kuzika watu wakiwa hai

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
b00e6b3e0434a464d659720f6364f6d8.jpg

Watu wengi tumekua tusikia watu wakisimulia juu ya kuwa, kulikuwa na wafalme ambao walikuwa wakizikwa na watu waliokuwa hai, kama sehemu ya mila na tamaduni.

Jamii ambayo ilifanya sana tamaduni hizi ni WAKUSH,ambao walikuwa waafrika weusi waliopata kuishi katika falme ya KINUBIA kuanzia mika ya 1700-350 B.C.E( KABLA YA KIPINDI CHA UKRISTO).

Wafalme wa Kush walipokufa walikuwa wakizikwa takribani na wafuasi 300 waliokuwa hai, kama ishara ya kutoa sadaka kwa miungu yao. Dhana ya kuzika watu hao ilihashiria kuwa binadamu anapokufa huwa kuna maisha mapya, hivyo kwa kuwa aliyefariki alikuwa mfalme basi alipaswa kuzikwa na wafanyakazi wasiopungua 300 ili kumtumikia.

Mfano wa mfalme wa Kush aliyezikwa na wafuasi zaidi ya 300 alikuwa mfalme Kashta aliyetawala kuanzia 760–747 B.C.E ( kabla ya kipindi cha Ukristo) sambamba na hilo makabuli yaliwekwa sehemu ya wazi ili kupata mwanga wa jua, kwani ikumbukwe kuwa wamisri na wanubia waliamini kuna maisha baada ya kifo. Na kwa mujibu wa Wanahistoria na wanaakiolojia wanasema kuwa wamisri walikuwa na miungu yao, moja ya Mungu alikuwa Jua (Sa-ra).

Na asilimia kubwa ya wafalme waliokuwa wakizikwa, walizikwa kwenye sehemu zenye uwazi. Hivyo kuzika watu waliofariki katika sehemu ya wazi na yenye jua, ili waweka watu karibu na Mungu wa jua aliyefahamika kwa jina la (Sa-ra).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....kwa population ya miaka kabla ya Kristo kuzika watu 300 kwa mkupuo mmoja ilikuwa na kuangamiza falme nzima.
.....habari hii ya kuzika watu 300 ntakuwa wa mwisho kuiamini sawa na ile ya Yesu kulisha watu zaidi ya 5000 kwenye mkutano mmoja kwa population ya kipindi kile watu 5000 kuhudhuria mkutano mmoja ni sawa kuwa mkoa mzima ulikuwa pale.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] kweli mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha ! Walizikwa Manyumbu tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
.....kwa population ya miaka kabla ya Kristo kuzika watu 300 kwa mkupuo mmoja ilikuwa na kuangamiza falme nzima.
.....habari hii ya kuzika watu 300 ntakuwa wa mwisho kuiamini sawa na ile ya Yesu kulisha watu zaidi ya 5000 kwenye mkutano mmoja kwa population ya kipindi kile watu 5000 kuhudhuria mkutano mmoja ni sawa kuwa mkoa mzima ulikuwa pale.
Mkoa mzima kuwa hapo kwa kipindi kile ilikua ni jambo la kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom