Historia ya Manchester Derby

Historia ya Manchester Derby

Pionaire

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
1,603
Reaction score
1,135
MANCHESTER DERBY,
20221001_102847.jpg

Ni mechi za mpira wa miguu zinazowakutanisha timu kuu mbili nchini Uingereza ambao ni Watani wa Jadi kutokea jiji la MANCHESTER upande wa GREATER MANCHESTER, Nao ni MANCHESTER UNITED(Man United) na MANCHESTER CITY(Man City).

Viwanja vyao vya mchezo ni ETIHAD(Kwa Man City...unaochukua idadi ya watazamaji 53,400 ) na OLD TRAFFORD(Kwa Man United...unaochukua idadi ya watazamaji 74,310) na Vikiwa vimetenganishwa na umbali unaokaribia miles.4 sawa na 6.4 Km tu.

HISTORIA ZAO,
Man United ilianzishwa mnamo mwaka 1878 ikitambulika kwa jina la NewTon Health LYR F.C na baadae kubadilishwa jina lake na kuitwa Rasmi Manchester United F.C mnamo mwaka 1902 na mashabiki wa timu hiyo wakitambulika kama THE RED DEVILS(Mashetani wekundu).

Man City ilianzishwa mnamo mwaka 1880 ikitambulika kwa jina la St.Mark's(West Gorton) F.C, kisha ilibadilishwa ikawa Ardwick Association Football Club mwaka 1887 na baadae kubadilishwa jina lake na kuitwa Rasmi Manchester City F.C mnamo mwaka 1894 na mashabiki wa timu hiyo wakitambulika kama THE CITYZENS(Wana nchi) na SKY BLUES(Wana Anga).

UHUSIANO WAO NA JIJI LA MANCHESTER.

Timu zote mbili ni wawakilishi sahihi kutokea jiji la manchester kwa maana ya kwamba zote zinabeba historia ya jiji hilo...KWA KUWA MANCHESTER TOKEA HAPO KALE NI MJI WA PILI NYUMA YA LIVERPOOL(Bandari yake iliyoanzishwa mwaka.1701 kwa maagizo ya King.James wa Britain na kufa 1710 kisha kufufuliwa upya mnamo mwaka 1846) WENYE BANDARI KONGWE PALE UINGEREZA ILIYOANZISHWA 1.JAN 1894(Mwaka sawa na uliyopo kwenye Badge/Logo ya Man City).
20221001_123820.jpg


Uwepo wa meli katika logo zote za vilabu hivii unawakilisha historia ya Bandari hiyo na Mlango wake mkuu wa kuingilia kutokea Baharini ukiweka umbali wa mile.36(km.58) tu kukuta upande wa magharibi mwa jiji hilo, hivyo kubadili taswira ya jiji la manchester kutoka kuwa Landlocked City na kuwa Port City.

Man city ikaenda mbali zaidi kwa kuiwakilisha mito mikuu mitatu iliyopo jijini manchester ijulikanayo kwa majina kama Irwell, Irk na Medlock kupitia mistari mitatu ya blue mpauko kwenye sehemu ya chini iliyo kwenye muundo wa diagonal katika ile bahari iliyobeba Meli. Kwenye Logo yao.

Kwa maana hiyo hii bandari ndo ilipelekea mapinduzi makubwa ya uchumi wa viwanda nchini uingereza yaliyoanzia Jijini manchester na tokea apo bandari hii imekuwa ni historia kubwa sana kwa Wakazi wa Jiji Hilo kwa Vizazi na Vizazi, na ata Wakazi wengi ambao ndo Mashabiki/Supporters/Wanachama wa hivyo vilabu walitokana na familia za wafanya kazi wa bandari hiyo na viwanda vilivyojaa jijini humo.

MAFANIKIO YAO KATIKA SOKA.
Man United.
Katika mafanikio ya soka la Mataji nchini Uingereza na ulaya Man united yupo mbele ya Man City kwa jumla ya vikombe.69...zikiwemo Ligi.20, kutokana na uwekezaji uliowekwa mapema tokea miaka ya 70's...na kupelekea timu iyo kutwaa mataji ya kutosha ndani na nje ya uingereza hasa katika miaka ya 80's chini ya mkufunzi mkuu Sir.Fergie.

Man City
Uku Man City wakiwa wanastruggle kwa kupanda ligi kuu na kushuka mara.4(Mwaka.1981, 1983, 1987 na 1998) na mara ya mwisho City kushuka daraja kutoka ligi kuu na kwenda championship ilikuwa ni 1998 na akaja kupanda tena mwaka.2001 na anzia hapo ndipo safari yao ya uhakika ya ligi kuu Uingereza ilipoanzia kwa kutoshuka tena daraja hadi kufikia mwaka.2008 timu iliponunuliwa na Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan kupitia shirika lake mama la Abu Dhabi United Group kwa kiasi cha £210million...inayomiliki kampuni kubwa ya ndege ya ETIHAD AIRWAYS, CITY FOOTBALL GROUP(CFG).LTD...n.k

Hapo ndipo City ikabadilika kutoka kuwa timu ya kawaida Ligi kuu na kuwa timu kubwa uingereza na kutawala soka la nchini uingereza baada ya miaka miwili ya umiliki huo kwa takribani miaka.10 iliyopita hadi apa walipo leo hii. Hii imewapa jumla ya vikombe 14 katika kipindi cha miaka 14 ya umiliki mpya wa mansour...yakiwemo makombe 6 ya ligi wakikamilisha jumla ya makombe yao yote kuwa 36 kabatini mwao.
20221001_170602.jpg


USHINDANI WAO KILA WANAPOKUTANA.
Derby ya kwanza baina ya Man United na Man City ilipigwa mwaka 1881 Nov.12...ambapo Newton Heath LYR(ambayo ndo Man United ya Sasa) wakishinda bao 3 bila dhidi ya St.Marks(ambayo ndo Man City kwa sasa). Hadi kufikia mchezo Ambao utapigwa apo kesho( Oct.2.2022) Majira ya saa.10 Jioni Kwenye dimba la etihad utakuwa ni mchezo wa derby wa 188 kati yao.

Na katika michezo ya jumla 187 hiyo Man united akiwa imeshinda jumla ya michezo.77 na kupoteza 57 huku Man City akiwa ameshinda jumla ya michezo.57 nakupoteza michezo..77, na wakitoka Sare ya michezo 53(KATIKA MICHEZO YOTE ZIKIWEMO CHARITY NA FRIENDLY MATCHES).
20221001_183609.jpg


Na katika michezo ya pamoja Ya ushindani pekee ni jumla ya michezo.164, City wakiwa wameshinda michezo.51 na kupoteza.65 uku United ikishinda michezo.65 na kupoteza.51 na wote wakitoa sare ya michezo.48, Na Cha kushangaza zaidi wamefungana idadi sawa jumla ya magoli.227 na kuruhusu Idadi sawa jumla ya Magoli.227.
20221001_102946.jpg


Na Tokea waanze kukutana vipigo vikubwa na vya aibu(yaani Kuanzia goli.5+) kuwahi kutokea kati yao Man United kapigwa vingi mara.4 huku city akiwa kapigwa mara.1 tu kama muonavyo hapo.
20221001_110923.jpg


Swali Je iyo kesho ni nani ataongeza USHINDI UPANDE WAKE???

Hatimaye Man City wameongeza ushindi mwingine kwenye Cabinet yao na kupelekea ushindi wa jumla kuwa michezo.58 katika MANCHESTER DERBY YA 188.

Mchezo uliopigwa Oct.2.2022 ETIHAD, Na City kuibuka na ushindi wa Bao: 6-3 dhidi ya United.
20221003_000722.jpg
 
Derby waga hazitabiriki na anaye jaribu kutabiri anajidanganya tu.
 
Derby waga hazitabiriki na anaye jaribu kutabiri anajidanganya tu.
Ni kweli mzee, form huwa zina mchango mdogo katika kushinda game kama izi. Na kikubwa ni mbinu ndo huwa KEY sanasana...hivyo ngoja tuone apo baadae mbinu za hao makocha zitawasaidia vip leo.
 
Derby waga hazitabiriki na anaye jaribu kutabiri anajidanganya tu.
Na hasa katika game hizi za karibuni...kumekuwa na ile kila timu inakaza zaidi inapokuwa away lakini kengine naona kwa ukongwe wa P.guardiola kwenye hizi game inaweza ikampa credit mbele ya Ten-Hag maana anajua zaid mtindo wa united kiuchezaji na acheze vip kumaliza michezo kama hii tofauti na ETH ambaye ndo game yake ya kwanza ya derby leo hivyo itahitaji awe na mbinu kwelikweli kumdhibiti genius.Guardiola vinginevyo akijichanganya tutaongea mengine.

Japo kuelekea mchezo huu wa leo United inaoekana kuwa ni UNDERDOG...lakini haina maana kwamba mchezo utakuwa mwepesi kwa city.
Screenshot_20221001-115320.jpg
 
Na hasa katika game hizi za karibuni...kumekuwa na ile kila timu inakaza zaidi inapokuwa away lakini kengine naona kwa ukongwe wa P.guardiola kwenye hizi game inaweza ikampa credit mbele ya Ten-Hag maana anajua zaid mtindo wa united kiuchezaji na acheze vip kumaliza michezo kama hii tofauti na ETH ambaye ndo game yake ya kwanza ya derby leo hivyo itahitaji awe na mbinu kwelikweli kumdhibiti genius.Guardiola vinginevyo akijichanganya tutaongea mengine.

Japo kuelekea mchezo huu wa leo United inaoekana kuwa ni UNDERDOG...lakini haina maana kwamba mchezo utakuwa mwepesi kwa city.
View attachment 2374485
Sawa
 
Derby waga hazitabiriki na anaye jaribu kutabiri anajidanganya tu.
Na hasa katika game hizi za karibuni...kumekuwa na ile kila timu inakaza zaidi inapokuwa away lakini kengine naona kwa ukongwe wa P.guardiola kwenye hizi game inaweza ikampa credit mbele ya Ten-Hag maana anajua zaid mtindo wa united kiuchezaji na acheze vip kumaliza michezo kama hii tofauti na ETH ambaye ndo game yake ya kwanza ya derby leo hivyo itahitaji awe na mbinu kwelikweli kumdhibiti genius.Guardiola vinginevyo akijichanganya tutaongea mengine.

Japo kuelekea mchezo huu wa leo United inaoekana kuwa ni UNDERDOG...lakini haina maana kwamba mchezo utakuwa mwepesi kwa city.

COMBINED XI KATI YA CITY & UNITED.
View attachment 2374485
 
Japo Lolote laweza kutokea katika mchezo wa ushindani kama derby...ingawa kuelekea mchezo huu makampuni mengi ya betting wamemuweka United kama Underdog.
20221001_103341.jpg
 
#FACTS kuelekea mchezo wa MANCHESTER DERBY hii leo. Wale wazee wa betting pitien hizi kabla hamjaweka #PESA zenu.
20221001_103254.jpg
 
#FACTS
*Takwimu kwa msimu huu, zinaonyesha Magoli ya city huweza kutokea katika kipindi chochote cha mchezo. Ndani ya Dakika.90 na hasa zaidi dakika. Ya 60 hadi 75.

Huku Magoli mengi ya United yakifugwa zaidi dakika. Ya 15 hadi 30 kipindi cha kwanza cha mchezo na dakika ya 45 hadi 75 ya kipindi cha pili cha mchezo.

Hii inamaanisha United inacheza kimkakati zaidi...huenda kocha atakuwa keshawapanga wachezaji wake kuwa katika dakika.90 za mchezo wana kipindi fulani cha kuchez mpira ili wapate matokeo na kuna kipindi wawe wanajilinda tu.
20221001_103223.jpg
 
Haaland hafungi leo
Sio kweli mkuu huu ni #UONGO wa asubuhi kabisa , japo kwenye mpira yote yanaweza kutokea ila Washambuliaji wa City ni hatariii sana...takwimu hazidanganyi ndugu.

Kizungu wanasema City have #RUTHLESS_ATTACKERS.
Screenshot_20221001-101339.jpg
 
Ila man City inashinda
Hhh!...hivi ndivyo ambavyo wewe na mie tunaona mkuu kwenye macho yetu lakini muda mwingine mpira una matokeo ya ajabu na ya kushangaza sana,

Maana kama ilifika wakati kule ujerumani bayern akiwa wa Moto aliwahi kupigwa 4 nunge na yule mtoto Bochum aliyepanda daraja na akiwa nyumbani kwake bayern. Wakati bayern anamfungaga Barca hadi goli.8.

Kwa hiyo lolote laweza tokea ndugu.
 
Back
Top Bottom