Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Dr. Kyaruzi alikusudia kuandika kitabu kueleza historia ya maisha yake katika siasa za Tanganyika wakati wa ukoloni na kueleza juhudi zake katika kuchangia fikra katika Constitutional Development Committee akishirikiana na Hamza Mwapachu na Dr. Luciano Tsere.
Kamati hii yao waliipa jina la Action Group.
Mwaka wa 1950 Dr. Vedasto Kyaruzi kama President wa TAA na Abdul Sykes Secretary, uongozi huu uliunda Political Subcommittee (Kamati ya Siasa) ndani ya TAA na jukumu lake lilikuwa kushughulika na mambo yote ya siasa.
Utaona kuwa wajumbe wawili wa Action Group Hamza Mwapachu na Dr. Vedasto Kyaruzi walikuwamo pia ndani ya TAA Political Subcommittee.
Ukisoma mswada wa Dr. Kyaruzi, ''The Muhaya Doctor,'' Abdul Sykes hatokezi sana anamtaja kidogo ingawa anasema kuwa Abdul ndiye alikuwa Secretary wa TAA na alishirikiana nae katika kutayarisha mapendekezo ya katiba.
Kyaruzi anasema katika mswada wake kuwa yeye kama Rais wa TAA ndiye aliyeamuandikia barua Seaton ya kumuomba aje aisaide TAA katika mashauri ya sheria na katiba.
Katika muingiliano huu wa Action Group na TAA Political Subcommittee ni wazi kuwa matokeo yake ni hayo mapedendekezo mazuri ya kuwataka Waingereza waondoke Tanganyika baada ya miaka 13 ya uchaguzi huru.
Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Ikiwa mamlaka inayotawala Tanganyika Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala.
Hili Waingereza hawakuwa wanalifanya kila uchao walikuwa wanazidi kujichimbia wabaki madarakani.
Siku zote watawala wote wawe wa ndani au kutoka nje huangalia maslahi yao kwanza ya kubaki madarakani hawaangalii, kutumia Kiswahili cha sasa ‘’maslahi mapana’’ ya nchi.
TAA haikulala kuanzia mwaka wa 1950 chama kilianza mikakati ya kuwaleta watu pamoja kuidai nchi yao.
Ili kupoza joto hili serikali ikaona itakuwa bora kwa kuwataka wananchi wa Tanganyika watoe mapendekeo ya katiba ili katika mapendekezo yapitishwe na ionekane kuwa wananchi wameshirikishwa katika kutawala na hivyo kuuzima kabisa ule moto wa kudai haki.
Hii ndiyo sababu ya serikali kuunda Constitutional Development Committee na kuomba mapendekezo.
Na mapendekezo walipewa.
Mapendekezo haya yaliwaudhi Waingereza hawakutaka wananchi wa Tanganyika wachague viongozi wao kupitia sanduku la kura kama demokrasia ya kweli inavyotaka na hili la kutoa uhuru ndiyo kwao wao lilikuwa zito na muhali mkubwa sana.
Matokeo yake serikali ikaanza mikakati ya kuwahujumu viongozi wa TAA kwa kuwahamisha katika sehemu mbalimbali za majimbo mbali sana na Dar es Salaam.
Dr. Kyaruzi akahamishiwa Kingolwira kisha Nzega, Hamza Mwapachu yeye akapelekwa kisiwani Nansio, Ukerewe.
Miaka mingi baadae sasa Juma Mwapachu mtu, mzima na kiongozi katika serikali ya Tanzania, Dr. Kyaruzi kwa kumtania Juma alimwambia kuwa baba yake aliwekwa kifungoni kisiwani Nansio na Waingereza.
Nia ya vitimbi hivi vya kuwahamisha viongozi wa TAA ilikuwa kudhoofisha uongozi wa TAA Makao Makuu na ikiwezekana TAA yenyewe ijifie mbali kwa kukosa uongozi wa watu madhubuti wa aina ya Hamza Mwapachu, Dr. Kyaruzi, na wengineo kwa kuwataja wachache.
Watawala hawakutaka kabisa kuwaacha Watanganyika wakawa huru.
Hii ni hulka ya watawala wote wawe wananchi au wageni wao siku zote hujitazama kwanza wao wenyewe na maslahi yao.
Watawala hujisikia vizuri kuwakalia wananchi vichwani na kuwapatia kile ambacho kina maslahi na wao kama watawala hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wanawaumiza wananchi.
Yaliyotokea Tanganyika mwaka wa 1950 katika Mapendekeo ya Katiba ya Twining hayana tofauti na yaliyotokea katika Mapendekezo ya Katiba ya Jaji Warioba.
Tofauti ni kuwa yale ya mapendekezo ya 1950 ya TAA Political Subcommittte yalikataliwa na wakoloni Waingereza na haya mengine yaliyokumba Katiba ya Jaji Warioba tumeyafanya sisi wenyewe lakini lengo ni lile lile.
Lengo ni kuzuia mabadiliko kwa kukataa kusikiliza sauti ya wananchi ili waliokuwa madarakani wabakie madarakani na waendelee kutawala.
Dr. Luciano Tsere
Gavana Edward Twining