Historia ya migogoro simba na yanga

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
C&P
MAPACHA WA KARIAKOO
[emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769][emoji769]

Baada ya kuingia makundi mwaka 1998 Yanga wakaanza kuvurugana walianza na advataizi kwa kumtimua kocha wao Marehemu Tito Mwaluvanda na kumleta Roul Shungu timu ikaboronga kwenye mashindano kwa kiasi kikubwa lakini choko choko zikaendelea Jangwani pamoja na kuchukua ubingwa wa Kagame mwaka 1999 lakini ndani ya nyumba kulikua hapakaliki wachezaji mastaa wakaanza kuondoka mmoja baada ya Mwingine Shaban Ramadhan,Kalimangonga Ongala,Akida Makunda,Mohamed Hussein mmachinga na mpaka kufikia mwaka 2002 wakongwe Edybily Lunyamila na Sekilojo Chambua nao wakatupiwa virago.Badala ya kujenga na kuimarisha timu Yanga walikua bize na mgogoro wao wa Yanga asili na kampuni.Mgogoro ambao ulikuja kumalizwa mwaka 2006 na hapo ndio Yanga wakashtuka na kuanza kujenga kikosi chao.
Huku mtaa wa pili hali ilikua shwari waliweza kuibomoa Yanga na kuchukua Staa wake wa kutumainiwa Mohamed Hussein Mmachinga lakini pia Simba walikua wanafanya usajili wa uhakika watu kama Emmanuel Gabriel,Boniface Pawasa,Mark Serengo,Suleiman Matola,Said Sued,Juma Kaseja,Ulimboka Mwakingwe,Patrik Betwel,Christpher Alex na Jozeph Kaniki walisajiliwa na Simba walihakikisha mastaa wake hao hawaondoki wala kuuzwa kizembe zembe.Kubwa zaidi na la kufurahisha Simba wakampata mdhamini mwenye moyo na anaeipenda Simba kutoka moyoni Mohamed Dewji,Njaa ikatoweka Msimbazi amani ikatawala timu ilikua ikivaa jezi za KK sukari,Metl na hata taifa soap yani ilikua raha tele.
Utulivu na neema iliyokuwepo Msimbazi ikazaa matunda mwaka 2003 Simba wakaingia hatua ya makundi kwenye ligi ya mabingwa Afrika kwa kishindo baada ya kuwavurumisha mabingwa watetezi ZAMALEKI. Baada ya kutolewa kwenye mashindano hayo stori ikabadilika Msimbazi migogoro ya Chini chini ikaanza wakaanza na advataizi kwa kumtimua kocha wao James Siang'a,Kama haitoshi na Katibu mkuu wao mzee Kassimu Dewji nae akaachia ngazi na mbaya zaidi mdhamini nae akaona ni ujinga akalala mbele,Simba yenye neema ikabaki kama yatima na ata wachezaji tegemeo nao wakaanza kuondoka mmoja baada ya mwingine,Simba wakaanza kuimba wimbo mpya kuwa wanajenga timu,mpaka kufikia mwaka 2006 Simba ilikua imekongoroka na kubaki skrepa huku ukitamba kwenye ligi za ndani kwa nadra na hata walipotoka nje ya nchi walipokea vipigo vikali na vya aibu mfano kutoka kwa Enyimba,Harras El Hadoud,Libolo na Ata Al Ahly Shandy.
Kuanzia mwaka 2006 Yanga wakaona migogoro ni ujinga wakaamua kukaa chini na kutengeneza timu yao,Yanga wakanunua mastaa kama Ben Mwalala,Ambani,Nsajigwa,Kaseja,Nurdin Bakari,Chuji,Abdi Kassimu,Ngassa,Kiiza,Kavumbagu na Domayo na miaka ya 2011 na 2012 Yanga wakabeba kombe la Kagame mfululizo.Pamoja na kuchukua kombe la Kagane hilo halikua lengo lao lengo lao kuu lilikua kuingia makundi kwenye michuano ya CAF na kidogo ndoto yao itimie mwaka 2014 lakini kwa bahati mbaya wakaondolewa kwa mikwaju ya penalt na mafarao wa Al Ahly.Yanga hawakukata tamaa wakaendelea kurundika mastaa kama Yondani,Ngoma,Kamusoko,Dida,Tambwe,Msuva na wengineo hatimaye ndoto imetimia mwaka huu baada ya kuingia makundi ya Confederation....
Je simba itaendelea kuwa na utulivu au ni yale yale ya mapacha wa kariakooo?
 
K
Kwa hiyo hawa mapacha was Kariakoo mmoja ni mkulima na mwingine ni mfugaji? Dah, all in all nimependa bandiko lako. Hakika migogoro ni sumu kwa mustakabali maendeleo.
 
Mkusanyiko wa Askari huitwa Jeshi.

Mkusanyiko wa Wabunge huitwa Bunge.

Mkusanyiko wa Wanachama wa Simba huitwa Mambumbumbu.

It's just a matter of time.
 
Watu hata kufanya uchaguzi tu inabidi wasimamiwe.Kikawaida wanayehitaji usimamizi ni watoto,wafungwa, wagonjwa na vichaa. Sasa sijui Chura wapo kwenye kundi gani hapo juu?
Unapata bilioni moja kutoka Sports Pesa ya udhamini unashindwa kulipa mishahara hata nusu.
Wachezaji wanagoma unachekelea,Makambo kazuiliwa mizigo yake hotelini kwa kudaiwa.
Kocha anadanganywa tumesajili wachezaji kumbe uongo.
Tukiwaita vichaa tumekosea?
Upo uchi unamshangaa na kumcheka aliyevaa suti bila tai.
Wendawazimu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…