Historia ya Misri: Wafalme waliooa dada zao na habari zisizojulikana

Historia ya Misri: Wafalme waliooa dada zao na habari zisizojulikana

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Misri ni maarufu kwa piramidi zake kubwa, miili iliyozikwa ndani yake na hazina zake za dhahabu. Lakini ni kiasi gani tunajua kuhusu Misri ya kale? Je, Piramidi Kuu ilijengwa na watumwa? Maiti ziliandaliwaje?

Taarifa 5 Bora zilizoandikwa na Joyce Tildesley, mtafiti kuhusu Misri.

Usipande ngamia

Ngamia hakutumiwa kila wakati huko Misri hadi mwisho wa falme, badala yake, Wamisri walitumia punda kama wabebaji na mashua kama njia rahisi ya usafiri.

Mto Nile unapita katikati ya ardhi yao yenye rutuba, na kutengeneza barabara kuu ya asili. Mkondo ulisaidia wale ambao walilazimika kusafiri kutoka kusini kwenda kaskazini. Wakati huo huo upepo ulifanya maisha yawe rahisi kwa wale waliotaka kusafiri kuelekea upande mwingine.

Mifereji iliunganishwa na makazi yalikuwa kando na mito, machimbo na maeneo ya ujenzi nazo mashua kubwa za mbao zilitumiwa kubeba nafaka.

Haki sawa kwa wanawake
Kuna maoni ya jumla kwamba Misri ilikuwa jamii ya wazalendo. Lakini huko Misri, wanaume na wanawake walitendewa kwa usawa mbele ya sheria. Hii ina maana kwamba wanawake wanaweza kumiliki, kununua, kuuza au kurithi mali

Wanaweza kuishi bila ulinzi wa walinzi wa kiume, wakifiwa na waume zao au kutalikiwa, wanaweza kulea watoto wao wenyewe.

Ilipendekezwa kwamba kila mtu katika Misri ya kale aolewe. Mke alikuwa msimamizi wa mambo yote ya nyumbani, alilea watoto na familia, wakati huo huo mume ambaye alikuwa na usemi zaidi katika ndoa na alikuwa na jukumu la kutafuta.

Wanawake wanaweza kutawala nchi

Ni desturi kwa mfalme wa Misri kuwa mwana wa mfalme aliyetangulia. Lakini si wakati wote, wakati mwingine wanawake walipata nafasi.

Wanawake walionyesha nywele zao angalau mara tatu katika historia ya Misri, Walitawala kwa uwezo wao wenyewe, walitumia mamlaka kamili ya mfalme. Anayetajwa kuwa aliyefanikiwa zaidi kati ya watawala hao wa kike ni Hatcheput aliyetawala Misri kwa zaidi ya miaka 20.

Unaweza kumuoa dada yako

Baadhi ya wafalme wa Misri walioa dada zao au dada wa kambo. Ndoa kama hizo zilihakikisha kwamba malkia wa nchi alifunzwa kutekeleza majukumu yake tangu kuzaliwa.

Ndoa hizo pia zilitumika kuzuia watu wengi kushindania kiti cha enzi. Waume pia walionekana kama fursa kwa mabinti wa kifalme ambao hawakuwa wameolewa.

Hata hivyo, ndoa za kaka na dada hazikuwahi kufanywa kuwa za lazima. Ndoa kama hizo hazikuwa za kawaida nje ya familia ya kifalme. Neno hilo maalum lilitumika kumuita wakati dadake alipokuwa mke wake.

Piramidi Kuu haikujengwa na watumwa
Mwanahistoria wa kale Herodotus aliamini kwamba Piramidi Kuu, ilijengwa na watumwa milioni moja. Dhana yake ya kufanya kazi kwa bidii katika hali ngumu zaidi kwa wanaume, wanawake na watoto bado inajulikana sana kati ya watengenezaji filamu wa leo.

Lakini ushahidi wa kiakiolojia unaonyesha kwamba Piramidi Kuu ilijengwa na wafanyikazi 5,000 wa kudumu, waliolipwa mishahara na wafanyikazi wa muda 20,000. Wafanyakazi hawa hawakuwa watumwa na walifanya kazi kwa zamu ya miezi mitatu au minne. Walikuwa wanaishi katika kambi ya muda karibu na piramidi. Huko walipewa chakula, vinywaji, matibabu na kadhalika. Waliokufa wakiwa kazini walizikwa katika makaburi yaliyokuwa karibu.

Huenda Cleopatra hakuvutia

Cleopatra VII, malkia wa mwisho wa Misri ya kale, aliwekwa katika mioyo ya watu mashuhuri wa Roma wakiwemo Julius Caesar na Mark Antony. Ikiwa ndivyo, bila shaka, anaaminika kuwa mrembo sana.

Lakini sarafu zake zinaonyesha kwamba hakuwa hivyo
Watu wengi sasa wanafikiri kwamba sura yake na pua, kidevu na macho ni dhahiri si kama mwanamke mrembo. Hata hivyo inafikiriwa kuwa huenda sarafu hizo zilitengenezwa kwa taswira kama hiyo kwa sababu hawakupenda sura yake.

Hakukuwa na mashuhuda waliomwona Cleopatra ana kwa ana. Hata hivyo, mwanahistoria wa kale anabainisha kwamba uzuri wake ulikuwa katika sauti na tabia.

IMG_20220118_112906.jpg
IMG_20220118_112852.jpg
IMG_20220118_112835.jpg
IMG_20220118_112822.jpg
 
Africa ilivamiwa sana na mataifa ya nje
sana....na bahati mbaya yetu hatukuwa na maandishi kuandika historia yetu. Babu zetu walitunza historia kwa kuhadithia. hata kamanda mrumi (Africanos) aliamua kuliita bara letu kwa jina lake.
 
sana....na bahati mbaya yetu hatukuwa na maandishi kuandika historia yetu. Babu zetu walitunza historia kwa kuhadithia. hata kamanda mrumi (Africanos) aliamua kuliita bara letu kwa jina lake.
hata kama zilikuwepo unafikir wangekubal kuziachia
 
Back
Top Bottom