Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Aprili 26, 2024: Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuriy a Watu wa Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi lilithibitisha Mkataba huo

Muundo wa Muungano

Muundo wa Muungano wa Tanzania kama ulivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una vyombo viwili vyenye mamlaka3 ya utendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar; Vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ambavyo ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Zanzibar; na vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma ambavyo ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara. Aidha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inashughulikia mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Sababu za kuwepo kwa Muungano

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile udugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pia, adhma ya kuwa na Muungano wa Afrika hususan kwa kuanzia na Shirikisho la Afrika Mashariki. Hata kabla ya uhuru wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere pamoja na viongozi wengine waliokuwa wakipigania uhuru katika ukanda wa Afrika walikuwa na matarajio ya kuwa na Muungano wa Afrika. Mwalimu Nyerere binafsi alipendelea uwepo Muungano wa Afrika kwa kuanzia na Mashirikisho ya kikanda.

Kimsingi zipo sababu mbalimbali zilizosababisha Muungano huu kama vile historia za nchi hizi mbili, ukaribu wa nchi hizi mbili, muingiliano wa kijamii, ushirikiano wa kibiashara, ushirikiano madhubuti na wa muda mrefu wa kisiasa baina ya TANU na ASP, ushirikiano na urafiki wa muda mrefu kati ya watu, viongozi, na wakati wa harakati za utaifa uliopelekea uhuru wa nchi hizo mbili.

Hati ya Makubaliano ya Muungano

Msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za mwaka 1964. Hati za Muungano zilitiwa saini na waasisi wa Muungano tarehe 22 Aprili, 1964, na kupelekea Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baada ya Muungano, Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya ya Muungano wa Tanzania na Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aprili 26, 1964 Bunge la Tanganyika lilipitisha Sheria za Muungano.

Halikadhalika, Sheria hizi zilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar. Sheria hizi za Muungano zilithibitisha Hati za Muungano, zilitaja Rais na Makamu wa Rais, zilitaja Muundo wa Muungano na Katiba ya Muungano.

Aidha, Aprili 27, 1964, waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni Sheikh Abeid Amani Karume, Kassim Abdala Hanga, Abdulrahaman Mohamed Babu, Hassan Nassor Moyo, Sheikh Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Sheikh Idris Abdul Wakil. Baada ya kuapishwa kuwa Wabunge wakateuliwa kuwa Mawaziri wa Serikali ya Muungano.

Kabla ya Muungano, kulikuwa na Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1962 na upande wa Zanzibar kulikuwa na Amri za Katiba (Decrees). Katiba ya Tanganyika baada ya kufanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya Muungano iliendelea kutumika kama Katiba ya Muungano ya mpito hadi mwaka 1977 ilipopitishwa Katiba ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria za Muungano.

Aidha, marekebisho hayo yalimtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais, akiwa ni msaidizi wa Rais kwa masuala yote ya kiutawala kwa upande wa Zanzibar, na Waziri Mkuu kuwa ni Makamu5 wa Pili wa Rais ambaye atamsaidia Rais kwa masuala yahusuyo upande wa Tanganyika na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.

Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliainisha mambo kumi na moja ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano chini ya usimamizi wa Serikali ya Muungano ambayo ni pamoja na Katiba na Serikali ya Muungano Mambo hayo ni: - Mambo ya Nchi za Nje; Ulinzi; Polisi; Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari; Uraia; Uhamiaji; Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje na Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Mambo mengine ni Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha; na Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

Kuongezeka kwa Orodha ya Mambo ya Muungano Mambo ya Muungano yaliongezwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwa kushirikisha pande zote mbili za Muungano. Juni 10, 1965, mambo yote yahusuyo sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yoyote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusu fedha za kigeni yaliingizwa kuwa jambo la 12 la Muungano.

Lengo kubwa la kuongezwa kwa jambo hilo ilikuwa ni kuwa na sarafu ya pamoja ya Tanzania baada ya Muungano, na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na mabenki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki mwaka 1964.

Baada ya kuvunjika kwa Bodi hiyo, kila nchi mwanachama wa Jumuiya ililazimika kuwa na sarafu na mipango yake ya kusimamia mambo ya kibenki na fedha. Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, tarehe 11 Agosti, 1967 mambo mawili yaliongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano ambayo ni leseni za viwanda na takwimu (Jambo la 13), na elimu ya juu (Jambo la 14).

Mwaka 1968, suala la maliasili ya mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa na gesi asilia liliongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano kuwa Jambo la 15.

Vilevile, kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 na kutungwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, mambo yafuatayo yaliongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano ambayo ni Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yanayohusika na kazi za Baraza hilo (Jambo la 16); Usafiri; Usafirishaji wa Anga (Jambo la 17) na Utafiti (Jambo la 18); Utabiri wa Hali ya Hewa
(Jambo la 19); na Takwimu (Jambo la 20).

Kutokana na kuvunjika kwa Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki mwaka 1979, suala la Mahakama ya Rufani ya Tanzania nalo liliongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano na kuwa Jambo la 21. Vilevile, kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Nyalali iliyokusanya maoni ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Uandikishaji wa Vyama vya Siasa na mambo mengine yanayohusiana nayo liliongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano (Jambo la 22).

Suala hilo hatimaye lilipitishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura Namba 258. Utaratibu uliotumika katika kuongeza idadi ya mambo ya Muungano kutoka 11 hadi kufikia 22 ni kupitia maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

HITIMISHO

Muungano umechukuwa nafasi kubwa katika kuwaunganisha wananchi na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wigo mpana kwa wananchi wake kuweza kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa lengo la kujipatia maendeleo.

Ni vyema tukatumia ipasavyo fursa zilizopo Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa kuleta maendeleo yatakayoinua hali ya uchumi wa Watanzania. Ili tuweze kuzitumia vizuri fursa hizi hatuna budi tuulinde,
tuuimarishe na kuudumisha Muungano wetu adhimu kwani ni dira ya maendeleo na mafanikio yetu.

Tovuti Kuu ya Serikali
 

Attachments

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Ulisainiwa Tarehe 22. Aprili. 1964 Na Waasisi, Mwl. Julius K. Nyerere Na Sheikh. Abeid Amani Karume, Na Kupitishwa Na Bunge Tarehe 26. Aprili. 1964. Mnamo Tarehe 27. Aprili.1964, Viongozi wa Nchi Zote Mbili (Mwl. Julius K. Nyerere na Sheik. Abeid Amani Karume) Walikutana Katika Ukumbi wa Karimjee - Jijini Dares Salaam, na Kubadilishana Hati za Muungano. Kisha Mnamo 28. Oktoba. 1964 Likathibitika Jina La Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni Mwa Malengo Ya Muungano, Ni Kutuunganisha, Na Kuchochea Ukombozi wa Kiuchumi Pamoja Na Kifikra, Kwenye Nchi Zote Mbili (Tanganyika na Zanzibar)

MIONGONI MWA FAIDA ZA MUUNGANO, NI PAMOJA NA;

- UKUAJI WA UCHUMI KWA NCHI ZOTE MBILI;
Uwepo wa Muungano Baina Ya Nchi Zote Mbili, Kunaendelea Kuchochea Ukuaji wa Uchumi,
Kwa Kuzingatia Suala La Utalii; Nchi Zote (Tanganyika na Zanzibar) Zina Vivutio Vya Utalii Vinavyochochea Ongezeko la Mapato Ya Taifa Zima, Na Kuwa Na Usimamizi Mzuri wa Fedha za Kigeni
Lakini Pia, Kutokana na Muingiliano wa Kibiashara... Ambapo Zanzibar Imebarikiwa Wafanyabiashara Wenye Uwezo Mkubwa Wanaochochea Ufanyaji Bora Wa Biashara Kati Ya Hizi Nchi Mbili, Pamoja na Kuwa Na Bandari Nzuri.... Lakini Pia, Bara, Ina Bidhaa Nyingi Zinazonunuliwa Kwenda Zanzibar, Na Kuchochea Upatikanaji wa Bidhaa Nyingi Kwa Urahisi... Jambo Linalochochea Utegemezi wa Nchi Hizi Mbili Kiuchumi, Na Ambapo, Zenyewe Kuwa Moja Kutasaidia Kupunguza Sheria Ngumu Na Kuchochea Uchumi wa Taifa Kukua.

- KUIMARISHWA KWA ULINZI NA USALAMA WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR;
Uwepo wa Muungano Ni Chachu Ya Kulinda Ulinzi na Usalama wa Nchi Zote Mbili, Kwasababu Uwepo wa Muungano Utazuia Uwekwaji wa Kambi Yoyote Ya Upinzani Kwa Nchi Moja Wapo (Bara Au Kisiwani)... Lakini Pia Ni Njia Ya Kulinda Mipaka Ya Mataifa Yote Mawili Na Kuyachochea Kuwa Katika Hali Ya Amani.

- KUCHOCHEA NGUVU YA TAIFA LA MUUNGANO WA TANZANIA;
Tukirejelea Taifa Kama Marekani Ya Kaskazini (U.S.A), Limeweza Kuunganisha States Zake Na Kupitia Hilo, Imechochea Marekani Kuwa Taifa Kubwa Lenye Nguvu Duniani... Vivyohivyo Hivyo Muungano Huu wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, Moja Ya Sehemu Ya Kuchochea Nguvu Ya Taifa La Muungano wa Tanzania Kwasababu Pia, Ndiyo Nafasi Ya Kuunganisha Nguvu Kazi Katika Uzalishaji wa Taifa, Lakini Pia Kuwa Chachu Ya Kuwa Taifa Imara.

- NI CHACHU YA MILANGO YA FURSA MBALIMBALI KWA BARA NA KISIWANI;
Muungano Wa Tanzania, Unaleta Nafasi Kwa Wananchi Wote wa Bara na Kisiwani Kuwa Na Upana wa Kupata Fursa Kama Wananchi Halali wa Tanzania, Kikatiba. Hii Imekuwa Hamasa Ya Wananchi wa Kisiwani na Bara, Kumiliki Pamoja na Kutumia Rasilimali Za Bara Au Kisiwani Ili Kujiendeleza... Ambapo, Rasilimali Zote Kutoka Bara na Kisiwani Ni Huru Kwa Wananchi Wa Pande Zote Kunufaika Nazo, Pia Kuzitumia Ili Kujiendeleza Katika Nyanja Za Maendeleo.

Lakini Pia ✍️;

- MUUNGANO NI NJIA YA KUENZI MAAMUZI YA WAASISI WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, NA MATAMANIO YA UWEPO WA MUUNGANO WA AFRIKA;
Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar, Ni Ishara Ya Kuenzi Maamuzi Ya Waasisi Wetu, Walioleta Uhuru Kwenye Nchi Zetu, Ambao Ni, Mwalimu Julius K. Nyerere, na Sheikh. Abeid Amani Karume.... Ambapo Miongoni Mwa Maono Yao, Ni Kuona Muungano wa Afrika, Ikiwa Ni Nia Ya Baadhi Ya Viongozi wa Afrika, Akiwemo Ndugu Kwame Nkurumah, Patrice Lumumba, Na Muammar Gaddafi. Huku Lengo Ni Kuiunganisha Afrika Kuwa Wamoja Kama Njia Bora Ya Kufikia Ukombozi wa Kiuchumi na Kifikra 🌍.

Miaka (60) Sitini Ya Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania. Tumeshikamana na Tumeimarika, Kwa Maendeleo Ya Taifa Letu 🇹🇿

HERI YA SIKUKUU YA MIAKA 60 YA
B9A1591B-8C8F-4CA7-9C06-6DEDEA37C048.jpeg
MUUNGANO WA TANZANIA 🇹🇿

#KaziIendelee 🇹🇿
 
Back
Top Bottom