cement
JF-Expert Member
- May 5, 2012
- 581
- 218
Nimekuwa nikisikia sana hili jina Mwanamakuka anasifiwa sana na baadhi ya redia kama nembo ya wanawake wajasiriamali. Binafsi nimetafuta google sijapata hints zozote!
Naomba mwenye kujua anifahamishe ni nani na mchango wape ni upi katika taifa hili maana nasikia sasa hivi kuna kuna tuzo zinaitwa jina lake.
=========
Habari zaidi...
HAKIKA HUYU MWANAMAKUKA ALIKUWA MWANAMKE WA SHOKA KATIKA ZAMA HIZO.
Mwanamakuka kwanza ni mwanamke wa kwanza kabisa mjasiliamali katika historia yetu.
Mwanamakuka alikuwa kipande cha mwanamke amepanda hewani, mlimbwende mwenye weusi wa sungusungu uzuri wake huo ndio ulikuwa ukimpa chati wakati ule, ukichanganyia
pia alikuwa mcheshi mwenye cheko bashasha na mkarimu kwa watu.
Alikuwa mnyamwezi wa Tabora ailiyekuwa akisafiri kufanya biashara na wakoloni ambao wakati huo walikuwa waarabu. Mwanamakuka alikuwa akisafiri kutoka Tabora mpaka bagamoyo kibiashara. Na hii ilikuwa karne ya 18.
Ujasiriamali wa wakati huo ilikuwa ni mbadilishano wa malighafi, vyakula vya nafaka kama vile mahindi, mtama, uwele, pia vyungu, asali na chumvi.
Waarabu walikuwa wakimpa vyombo na bidhaa za kauli, kama ujuavyo wakati ule biashara zilikuwa za kubadilishana zaidi. Mama huyu sifa yake inayomuweka katika historia ni ujasiriamali.
Mwanamakuka aliolewa na Chifu Pazi, chifu wa kizaramo. Walikaa katika ndoa na mumewe lakini hawakubahatika kupata mtoto kurithi na kuendeleza jina.
Alifariki mwaka 1793 na kuzikwa hapo Bagamoyo katika nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe pia Chifu Pazi alifariki na kuzikwa hapo hapo.
Ili kuenzi kazi zake na mafanikio yake kwa wanawake kuna shindano linafanyika kila mwaka linaloitwa Mwanamakuka awards kama heshima ya kuenzi alichokifanya.

Mwanamakuka kwanza ni mwanamke wa kwanza kabisa MJASIRIAMALI katika historia yetu.
Mwanamakuka alikuwa kipande cha mwanamke amepanda hewani,mlimbwende mwenye weusi wa sungusungu wenye mg'aro mithili ya chungu ndio ulikuwa ukimpa chati wakati ule.Alikuwa mcheshi mwenye cheko bashasha na mkarimu kwa watu.
![]()
Hili ndilo eneo alilokuwa anaishi Mwanamakuka ambalo saivi limejengwa shule.
Alikuwa mnyamwezi wa Tabora ailiyekuwa akisafiri kufanya biashara na wakoloni ambao wakati huo walikuwa waarabu.Mwanamakuka alikuwa akisafiri kutoka Tabora mpaka bagamoyo kibiashara.Na hii ilikuwa karne ya 18 leo tupo karne ya 21 ni miaka mingapi iliyopita?
Ujasiriamali wa wakati huo ilikuwa ni mdadilishano wa mali ghafi,vyakula vya nafaka kama vile mahindi,mtama,uwele,pia vyungu,asali na chumvi.
Waarabu walikuwa wakimpa vyombo na bidhaa za kauri.Kama ujuavyo wakati ule biashara zilikuwa za kubadilishana zaidi.Mama huyu sifa yake inayomuweka katika historia ni ujasiriamali.
![]()
Shule hii ilipewa jina lake (Mwanamakuka) kama ishara ya kumuenzi.
Mwanamakuka aliolewa na Chifu Pazi,chifu wa kizaramo.Walikaa katika ndoa na mumewe lakini hawakubahatika kupata mtoto kurithi na kuendeleza jina.
![]()
Hiyo kama nyumba ndio kwa ndani kuna kaburi la Mwanamakuka na mume wake.
Alifariki mwaka 1793 na kuzikwa hapo Bagamoyo katika nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe pia Chifu Pazi alifariki na kuzikwa hapo hapo.
![]()
Kaburi la Mwanamakuka,lipo karibu sana na Pwani ya Bagamoyo.