Historia ya Mwanamakuka

cement

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
581
Reaction score
218
Nimekuwa nikisikia sana hili jina Mwanamakuka anasifiwa sana na baadhi ya redia kama nembo ya wanawake wajasiriamali. Binafsi nimetafuta google sijapata hints zozote!

Naomba mwenye kujua anifahamishe ni nani na mchango wape ni upi katika taifa hili maana nasikia sasa hivi kuna kuna tuzo zinaitwa jina lake.


=========

Habari zaidi...

HAKIKA HUYU MWANAMAKUKA ALIKUWA MWANAMKE WA SHOKA KATIKA ZAMA HIZO.
Mwanamakuka kwanza ni mwanamke wa kwanza kabisa mjasiliamali katika historia yetu.

Mwanamakuka alikuwa kipande cha mwanamke amepanda hewani, mlimbwende mwenye weusi wa sungusungu uzuri wake huo ndio ulikuwa ukimpa chati wakati ule, ukichanganyia
pia alikuwa mcheshi mwenye cheko bashasha na mkarimu kwa watu.

Alikuwa mnyamwezi wa Tabora ailiyekuwa akisafiri kufanya biashara na wakoloni ambao wakati huo walikuwa waarabu. Mwanamakuka alikuwa akisafiri kutoka Tabora mpaka bagamoyo kibiashara. Na hii ilikuwa karne ya 18.

Ujasiriamali wa wakati huo ilikuwa ni mbadilishano wa malighafi, vyakula vya nafaka kama vile mahindi, mtama, uwele, pia vyungu, asali na chumvi.

Waarabu walikuwa wakimpa vyombo na bidhaa za kauli, kama ujuavyo wakati ule biashara zilikuwa za kubadilishana zaidi. Mama huyu sifa yake inayomuweka katika historia ni ujasiriamali.

Mwanamakuka aliolewa na Chifu Pazi, chifu wa kizaramo. Walikaa katika ndoa na mumewe lakini hawakubahatika kupata mtoto kurithi na kuendeleza jina.

Alifariki mwaka 1793 na kuzikwa hapo Bagamoyo katika nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe pia Chifu Pazi alifariki na kuzikwa hapo hapo.

Ili kuenzi kazi zake na mafanikio yake kwa wanawake kuna shindano linafanyika kila mwaka linaloitwa Mwanamakuka awards kama heshima ya kuenzi alichokifanya.
 
Some hints:

 
kwa hiyo jina lake linachukuliwa kam role model kwa wajsirimali wanawake?! let's hope her bloodline wont's make a fuzz out of the idea... wakishajua wajanja wanabonda hela ya tukio...
 
Ok sio mbaya japo nahisi kuna kitu nyuma ya pazia kwa nn sasa hivi??
 
kwa hiyo jina lake linachukuliwa kam role model kwa wajsirimali wanawake?! let's hope her bloodline wont's make a fuzz out of the idea... wakishajua wajanja wanabonda hela ya tukio...


mkuu umenena kweli
 
huyo niliwahi kusikia jina anaitwa kibaka mmoja tandale kwa tumbo na alishakufa kwa kuchomwa moto
 
Ok sio mbaya japo nahisi kuna kitu nyuma ya pazia kwa nn sasa hivi??

Mjini hapa.. watu wakishanusa hela wanachakarika... huoni masemina ya WAMA kila kukicha yanatangazwa..... wanaweka kichwa kimoja cha ukweli toka sirikalini na wadhamini wanamwaga noti..
 
mhn! sina uhakika kama ni hivi sana lakini ninalokumbuka ni mmoja wa watumwa wa mwisho mwisho waliokombolewa wasiuzwe hili lilikuwa linampa umaarufu zaidi siku za nyuma sasa hili lingine mimi mgeni japo kiukweli sio kuwa nawabeza waliotoa tuzo hii lakini naungana na wenzangu kwa nini iwe sasa?
 
Ahsante mwanzoni nilipofika bagamoyo na kusikia jina hili LA Mwanamakuka lilinishinda kulitamka na nikajua ni kama majina mengine ya kina Bashite
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…