Historia ya Mwembe wa Ikulu (Mwembe wa Muungano) uliopandwa na Mwalimu Nyerere pamoja na Abeid Karume

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, kuna mwembe mkubwa wenye historia ya kipekee. Mwembe huu, unaotarajiwa kutimiza miaka 61 mnamo Aprili 2024, haujulikani sana kwa wengi.

Mti huo ulipandwa tarehe 26 Aprili 1964 kama sehemu ya kumbukumbu maalum ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Upandaji wake ulifanyika baada ya tukio la kuchanganya udongo kutoka pande zote mbili za Muungano—Tanganyika na Zanzibar—ishara ya mshikamano wa mataifa haya mawili.​

Screenshot 2025-02-28 at 14.59.28.png
Mwembe Ikulu.jpg

Mwonekano wa Mwembe wa Ikulu

Miongoni mwa watu waliobeba udongo kutoka Zanzibar ili kuchanganywa na ule wa Tanganyika ni Hassan Omar Mzee kutoka Unguja. Wengine ni Hassan Kheir Mrema na Sifaeli Kunda kutoka Tanganyika, pamoja na Khadija Abbas kutoka Zanzibar.

Katika hafla hiyo ya kihistoria, mwembe huo ulipandwa kwa pamoja na Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume, na ukapewa jina la “Mwembe wa Muungano.” Udongo uliochanganywa pamoja na vifaa vilivyotumika katika tukio hilo ulihifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa. Udongo kutoka Zanzibar ulitolewa Kizimbani, Unguja, huku ule wa Tanganyika ukitolewa jijini Dar es Salaam.

Mwembe huu umekuwa alama ya Muungano wa Tanzania, ukionesha mshikamano wa kudumu kati ya watu wa bara na visiwani, uhusiano uliodumu kwa karne nyingi. Hadi sasa, mwembe huo bado upo katika viwanja vya Ikulu, ukijulikana rasmi kama “Mwembe Muungano,” ingawa wengine huuita “Mwembe wa Ikulu.”

Kabla ya historia hii, baadhi ya watafiti wa masuala ya kihistoria waliuita mti huo “Mwembe wa Tanzania.”

Inapaswa pia kukumbukwa kuwa majina yanayohusiana na miti ya miembe siyo jambo geni nchini Tanzania wala katika mataifa jirani. Kwa mfano, jijini Dar es Salaam kuna eneo linaloitwa Mwembe Chai, mkoani Kigoma kuna eneo linaloitwa Mwembe Togwa, na ndani ya mji wa Makambako (Njombe) kuna kata iitwayo Mwembetogwa.

Vilevile, nchini Kenya, katika mji wa Mombasa, kuna eneo maarufu linaloitwa Mwembe Tayari.
 
Yaan na huwa nawaza Nyerere si angeumgana na hata na Malawi jamani,sasa unaona uliyotuletea huku na hawa wazanzibar
 
Katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, kuna mwembe mkubwa wenye historia ya kipekee. Mwembe huu, unaotarajiwa kutimiza miaka 61 mnamo Aprili 2024, haujulikani sana kwa wengi.

Mti huo ulipandwa tarehe 26 Aprili 1964 kama sehemu ya kumbukumbu maalum ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Upandaji wake ulifanyika baada ya tukio la kuchanganya udongo kutoka pande zote mbili za Muungano—Tanganyika na Zanzibar—ishara ya mshikamano wa mataifa haya mawili.​

View attachment 3253190 View attachment 3253209

Badala ya kujadili Faida za huo Muungano ambao siku hizi umeonekana kulalamikiwa kila siku na Watu wengi, wewe unaongelea kuhusu mti wa mwembe!!?!!
 
Tanga kuna Mwembe mawazo ,Mwembe basha na temeke Mwembe yanga!
 
Kigoma kuna Mwembetogwa na Mwembenguruwe.
 
Kuchanganya udongo kuna husiana vipi na kupanda mti ? Mwongo mkubwa. Source yako nini ? Au ulikuwepo ?

Hatuhitaji miti wala udongo wa Zanzibar. Siku inaanguka CCM agenda ya kwanza mezani kwa Rais ni kujadili Muungano kwa uwazi.

95% ya Wazanzibar watataka nchi yao. Tutawaambia sepeni.
 
Znz kuna miembe mingi sana
Muembe dezo
Muembe madafu
Muembe makumbi
Kiembe samaki
Miembeni
Muembe mimba
Muembe mmoja
Miembe mingi
Mwembe chai
Muembe shauri
Muembe ladu
Muembe beni
Muembe njugu
Muembe kiwete
Muembe Tanga
Muembe mchomeke
Nk
 
Unajaza saver za watu kwa ujinga huu we uliuonaje huo mwembe kama hujaingia ikulu fanya majukumu yako pita hivi leta vitu vya msingi mengine waachie kina Mwijaku
 
Back
Top Bottom