Kweli nimekumbuka nyakati nilizopitia...ni ngumu, chungu zilizojaa giza kukata tamaa kukosa tumaini na kila mtu alinikimbia mpaka ndugu jamaa na marafiki.....
Kukosa chakula,nguo kuchakaa, viatu kuisha kabisa kabisa...mpaka sehemu nilizokuwa nakwenda kuomba vibarua nilikataliwa au nilidhulumiwa
Njaa ilikuwa ni sehemu ya maisha yangu...na ndio nikaja kugundua kulala njaa mwili asubuhi unaamka ukiwa na nguvu sana, sasa hii sijui ni muujiza kwangu tu au inatokea kwa wote?
Na wakati napitia magumu yote haya nyumbani nilikuwa nina mtoto mchanga na mke wangu kajifungua kwa operation.
Tulianza kuuza vitu kimoja kimoja mpaka nyumba ikabaki inatushangaa....
Mungu saidia hiyo nyumba nilikuwa nimeanza kuijenga haina sakafu..haina plasta tuepauwa vyumba viwili tu...nyoka nnge na wadudu mbalimbali walikuwa ndio maskani yao
Pesa ya mkaa tulikosa nikaanza kuokota chupa nachanganya na kuni kidogo ndio zinakuwa za kupikia..sufuria zote ziligeuka nyeusi kwa ajili ya kupikia kuni.
Watu hasa ndugu walianza maneno kwamba kuna laana za mababu,baadhi ya majirani walitushauri kwenda kwa waganga.
Katika yote hayo kwa ndani kabisa ya moyo wangu kulikuwa na sauti inasema waziwazi kwamba iko siku...na mimi mwenyewe nilikuwa ninajitamkia kwamba iko siku mateso haya yote yatakwisha.
Na kweli acheni Mungu aitwe MUNGU.