Historia ya neno Daladala

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Asili ya neno Daladala ni jina tulilolitohoa kutoka sarafu ya Marekani, yaani, Dola. Nakumbuka kwenye miaka ya 80 mwanzoni , na katikati ya shida kubwa ya usafiri Dar, nauli za usafiri wa vibasi vidogo vidogo ikaongezeka na kufikia shilingi tano kwa safari moja.

Ndipo hapo tuliweza kumsikia kondakta akiita; " Kariakoo Dala ..dala..dala... dala!"
Maana, shilingi tano yetu iliyokuwa nzito kidogo hata kuishika na yenye pembe sita ilikuwa na thamani sawa na dola moja ya Marekani. Ndipo hapo, shilingi tano yetu ikabatizwa jina la ' Dala'.

Kuna mengi ya kutafakari kuhusiana na uchumi na jamii yetu. Tujiulize; wakati wasafiri wa daladala enzi hizo walikuwa ni watu wa kipato cha chini na hata cha kati, je , wasafiri wa daladala wa leo ni watu wa aina gani? Wasafiri wa Mabasi ya Mwendo Kasi ni watu wa aina gani?

Je, anayepanda daladala leo, na anayepanda mabasi ya mwendo kasi anatazamwa vipi? Ni mtu asiye na uwezo kifedha au anaweza kuwa ni mtu anayeona kuliacha gari lake nyumbani na kupanda dala dala amefanya mawili; amebana matumizi na kuelekeza fedha zake kwingine na hata kutunza mazingira. Maana, magari mengi mijini yanachafua mazingira.

Je, ni kwa nini uchumi wetu wakati huo ulikuwa na nguvu kutuwezesha kubatiza sarafu zetu kwa fedha za kigeni kama dala kwa shilingi tano. Wengine waliita gwala.

Tuliweza pia kuibatiza noti ya shilingi 20 kwa kuiita ' Paundi' ikiwa na maana, thamani ya paundi moja ya Uingereza wakati huo ilikuwa ni sawa na shilingi 20 za Tanzania. Ni kwenye miaka ya 80.

Je, rasilimali zetu ikiwamo gesi na mafuta vinaweza kuturudisha kwenda kuwa ' Taifa Kubwa' kama tulivyokuwa wakati fulani. Maana, nakumbuka nikiwa mdogo nilisikia redioni taarifa ya habari ikisema kuwa ' Tanzania imetoa msaada wa magunia ( Sikumbuki idadi) ya kunde na maharage kwa nchi ya India kutokana na mafuriko yaliyowakumba.

Nilisikia pia Tanzania ikitoa msaada wa chakula kwa nchi ya Msumbiji na kwingineko zilizokumbwa na maafa.

Je, tunaweza kurudia kuwa ' Taifa Kubwa' kiuchumi kama tutaendelea kuruhusu karibu kila nchi kubwa kiuchumi kuwa na benki zao hapa kwetu? Maana siku hizi hapa kwetu kuna benki za Wahindi mpaka Wapakistani! Je, na sisi tuna mabenki kwao?

Na tafsiri ya benki hizo si ina maana pia kuwa nchi hizo zimeamua kujenga ' Vihenge' vyao kwetu kuhifadhia wanavyovuna hapa kwetu na kusafirisha kwenda kula kwao.

Na tuendelee kujadili daladala na uchumi wetu...! Na cha kukuhakikishia, ni kuwa hakuna hatari ya miaka michache ijayo, Daladala zikabatizwa jina jipya, kuitwa 'Bukubuku!' Kwa maana ya nauli za Daladala zitapanda kufikia shilingi elfu moja kwa safari. Jina ' Daladala' litabaki daima kuwa na maana ya usafiri wa ndani wa njia fupi fupi.
 
Awamu ya 5 inatupeleka TANZANIA ya Viwanda Yenye Uchumi wa KATI,Tutafikia hiyo hadhi tuliyokuwa nayo miaka ya 80...Maendeleo hayana CHAMA.
 
Kama ni hivyo sasa hivi Nauli ilipaswa kuwa 2400 kutokana Na dola kwa hiyo tuko vizuri kwenye kudhibiti mfumuko
 
ile nachojaribu kufikiri kwa uwazi nezi hizo rosana ilikuwaje na aliyekuwa anaita kariakoo dala dala alikuwa msomi kiasi gani nahisi kwa heshima ni sawa na madereva wa mwendokasi.. shikamoo dala dala sasa imekuwa chanzo cha mapato kwa ...
 
Tuliweza pia kuibatiza noti ya shilingi 20 kwa kuiita ' Paundi' ikiwa na maana, thamani ya paundi moja ya Uingereza wakati huo ilikuwa ni sawa na shilingi 20 za Tanzania. Ni kwenye miaka ya 80.

Ni kumbukumbu nzuri sana, katika miaka hiyo nakumbuka ndiyo naanza kujua kusafiri peke yangu kutoka Dar kuelekea Tanga nikiwa mtoto, nikapewe Sh 100, Ilikuwa zile noti za shilingi 10, na zilikuwa 10 mpya kabisa. Wakati huo unasafiri, kutoka Chalinze kwenda Segera unaona msitu mkubwa sana na barabara ilikuwa mbaya sana.
 
Wakati huo wa dala kulikuwa hakuna mabank ya nje?
Pia hakuna taifa linakataza kufungua bank ya Tz nje ni sisi tu
Kama hatuelewi mpaka leo mfumo wa maisha ni tatizo la akili tu
Uchumi na maendeleo ya nchi hayana tofauti sana na mfumo wa mwenye nyumba na familia yake anavyoiongoza
Kwani ili tusonge mbele ni lazima tujichanganye na kutafuta uhusiano wa kimasoko ya taifa ili hiyo DALA ilirudi kwenye nguvu yake

Usitegemee uchumi utakuwa kama huuzi kitu nje hata nyanya na pilipili zinawrudishia Familia ya jirani Kenya na Uganda hizo Dala unazozisema na sisi tutakaa kujisifia tu kwenye magazeti ila kiuhalisia bado sana

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…