Habari
Labda nikusaidie bwana mdogo. Huyo kijana amesoma ama kusikia kwamba
1) Osama alikuwa rafiki wa marekani, pia kulikuwa na uhusiano wa kibiashara baina ya makampuni ya baba wa Osama na yale ya aliekuwa makamo wa raisi katika utawala wa Bush, bwana Dick Cheney, na Osama alipata mafunzo ya kijeshi kutoka kwa marekani lakini baadae wawili Hawa wamekuja kuwa maaduwi wakubwa
2)Kundi la ISIS limeanzishwa na marekani, lakini kwa sasa pia kuna uadui Mkubwa baina yao
Mi nadhani kinachotakiwa ni kuthibitisha, au kukanusha juu hayo aliosikia huyo kijana na kama ni kweli ueleze kilichosababisha uadui baina ya Osama na Marekani kwa upande mmoja na uadui uliopapo baina Isis na Marekani kwa upande mwengine .