Historia ya Penicillin

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ilianzia mwishoni mwa karne ya 19 kulikuwa na misemo mingi ya wanasayansi na madaktari juu ya antibacteria unyevu na ukungu ikiwemo penicillin ukungu, lakini hawakuwa wamegundua njia ya uhakika au ushahidi ni kitu gani kilisababisha kutokea kwake. Kilichosababisha unyevu na ukungu wa penicillium uliweza kugundulika na kuweza kutolowe mwaka 1928 na mwanasayansi wa Kistcotish Alexander Fleming, katika kazi zake ilionekana ilikuwa tofauti na matokeo yaliyoripotiwa kwanza. Fleming aliandika ugunduzi wake wa penicillin kuwa ilikuwa asubuhi ya Ijumaa, September 28, 1928. Hadith ya asili ya kisa hiki inaelezewa kama ajali: maabara yake iliyokuwa katika ghorofa ya chini ya Hospitali ya St Mary London (ambayo sasa ni sehemu ya Imperial College), Fleming aligundua ki sahani sthapylococcus (aina ya chenga za bacteria zenye umbo la zabibu) ambazo ziliachwa wazi kwa makosa na zilikuwa zimepata ukungu wa blu-kijani kutoka kwenye dirisha lillilokuwa wazi, ukungu ule ulionyesha kukua. Fleming aligundua kuwa kulikuwa na duara katikati ya ukungu ule, lililotoa vitu vilivyozuia kukua kwa bacteria wale na hatimae kuweza kuua bacteria hatimae.

Baada tu ya ugunduzi huu, Fleming aliotesha pure culture (aina moja ya organism) na kugundua kuwa ukungu ule ulikuwa ni Penicillium ambayo ilikuja kujulikana kama Penicillium notatum. Flemin alianzisha neon “penicillin” kwa kuelezea uchujaji wa culture kutoka kwenye ukungu wa Penicillium. Fleming alimuomba C.J. La Touch amsaidie kuchunguza ukungu, ambae kwa makosa alisema ni ukungu wa Penicillium rubrum (ilisahihishwa baadae na Charles Thom). Alielezea hitimisho lake kuwa penicillin itakuwa na matumizi makubwa sana ya kuua bacteria, kwasababu ya umuhimu wake na pia ina kiwango kidogo cha sumu kulinganisha na aina nyingine ya vitu vilivyotumika kuua bacteria wakati huo. Alugundua umuhimu wake katika maabara katika kuondoa Bacillus infuenzae (inayojulikana kama Haemophilus influenza).

Fleming hakuwa mzuri katika mawasiliano wala hakuwa mzungumzaji mzuri, hii ilimaanisha ugunduzi wake haukupewa hamasa sana. Hakuweza kuwashawishi wanakemia kuweza kumsaidia kutoa na kuhifadhi mchanganyiko ule wa antibacterial kuweza kuchujwa. Pamoja na kuwa hakukuwa na kemia ya uhakika, aliweza kuendelea na hamasa yake ya umuhimu wa penicillin na aliweza kuandika “paper” kazi yake aliyoiita “A Medium for the Isolation of Pfeiffer’s Bacillus” ambayo aliipeleka kwenye Medical Research Club ya London, ambako haikupewa umuhimu sana na pia wataalamu hawakuonyesha moyo wa kumuunga mkono. Kama mafanikio ya Fleming yangepewa kipaumbele na wanasayansi, penicillin kama dawa ingeanza kutumika mapema kuliko ilivyokuja.

Alexander Fleming.

Hata baada ya wanasayansi kutokuonyesha hamasa na ugunduzi ule, Fleming aliendelea kufanya majaribio mengi kwenye antibiotic aliyogundua. Majaribio ya muhimu sana yalikuwa kugundua kuwa haikuwa na madhara kwa binadamu kwa kujaribu kwanza kupima kama sumu inaweza kuua wanyama na baadae kwa binadamu. Majaribio yake mengine aliyafanya kuangalia mabadiliko katika hali ya joto na kiwango cha alkalin (pH) nah ii ilimwezesha kuendlea kuweka mkazo kwenye mchanganyiko huo. Jaribio la muhimu sana ambalo wanasayansi wa sasa wamelikosa katika kumbu kumbu za Fleming ni jaribio la penicillin kwa mnyama mwenye maradhi, majibu yake ambayo yangeweza kuleta hamasa kubwa katika penicillin na kuongeza kasi ya maendeleo yake kwa takriban miaka 10.

Hatua za Kitabibu.

Mwaka 1939, Cecil George Paine, pathologist (mwanasayansi aliyesomea chanzo na tiba ya magonjwa na anaekaa maabara kuchunguza tissue za mwili kugundua ugonjwa) kutoka Royal Infirmary ya Sheffield, alijaribu kutumia penicillin kwa kutibu sycosis barbae inayotokea kwenye vyanzo vya ndevu, lakini alishindwa. Alihamia kwenye ophthalmia neonatorum ambayo ni maambukizi yanayowapata watoto wadogo wakati wanazaliwa na yanadhuru macho, alifanikiwa na kumbukumbu ya kwanza ya tiba ya penicillin ilikuwa 25 November 1930. Aliweza kuwatibu wagonjwa wengine wane (mmoja mtu mzima na watoto watatu) kutokana na matatizo yale ya macho

Mwaka 1939, mwanasayansi wa Australia aliyeitwa Howard Florey (Baadae Baron Florey) alijiunga kwenye timu ya wanaresearch ya (Ernst Boris Chain, Arthur Duncan Gardner, Norman Heatley M Jennings, wakiwa University ya Oxford kwenye Sir Willima Dunn School of Pathology waliweza kufanya maendeleo katika kuonyesha bacteria waliokuwa hai na action ya penicillin. Mwaka 1940, walionyesha kuwa penicillin ilikuwa na uwezo wa kuua bacteria katika panya. Mwaka 1941 walimtibu polisi Albert Alexader, aliyekuwa na maambukizi makubwa usoni na hali yake ilitengemaa lakini dawa ya penicillin illisha kwenye stock na mgonjwa alifariki. Baada ya hapo wagonjwa wengine wengi walitibiwa na kupona.

Howard Walter Florey.

Kufikia mwaka 1940, team ya Oxford chini a Howard Florey waliweza kubuni mbinu ya kuzalisha penicillin kwa kiwango kikubwa, lakini bado uzalishaji haukuwa mkubwa kukidhi soko. Mwaka 1941 Florey na Heatley walisafiri kwenda Marekani ili kuweza kushawishi makampuni makubwa ya dawa kuzalisha dawa hiyo na wawaeleze mafanikio yao. Mwaka 1945 Florey na kikundi chake walitunukiwa nishani ya Nobel katika Madawa na walimjumlisha Fleming katika kazi yao.

Matatizo ya uzalishaji mkubwa wa dawa hii, mnamo 14 March 1942, mgonjwa wa kwanza alitibiwa na streptococcal septicaemia (maambukizi kwenye damu) kwa kutumia penicillin iliyotengenezwa Marekani na Merck & Co. Nusu ya dawa zilizotengenezwa zlitumika kumtibu mgonjwa yule. Ilipofika June 1942 penicillin kidogo sana zilizotosha kutibu wagonjwa 10 tu ndiyo zilizoweza kupatikana. July 1943, kutokana na Vita Kuu ya II ya dunia, iliamriwa dawa hizi zizalishwe kwa wingi na kusambazwa kwa wanajeshi waliokuwa vitani katika bara la Ulaya. Kutokana na utafiti wa kutumia amino acid kutoka kwenye mahindi ilisaidia kupata culture ya penicillin katika Maabara ya Peoria, Illnos, na kuweza kuzalisha dose 2.3 millioni wakati wa kuvamia Normand (kaskazini mwa Ufaransa) 1944. Soko liligundua kuwa ukungu uliotengenezwa na unga wa mahindi (corn steep liquor) ulikuwa bora zaidi na hii ilipelekea utengenezaji wake uwe kwa kiwango cha juu na matank makubwa ya kuzindika (deep tank fermentation) yaliyotengenezwa na chemical engineer Margaret Hutchinson Rousseau. Matokeo yake vidonge 646 billion vilitengenezwa.

Margarte Hutchinson Rousseau
 
dawa gani kati ya hizi zina kiwango kikubwa cha pennicillin
1.Amoxicillin
2.Ampicillin
3.Cloxacillin
 
dawa gani kati ya hizi zina kiwango kikubwa cha pennicillin
1.Amoxicillin
2.Ampicillin
3.Cloxacillin
For what what I gather penicillin has to be taken with an empty stomach so do ampicillin but amoxicillin and cloxacillin so the answer will be ampicillin. Lakini nitatafuta jibu vizuri kesho na wengine wanakaribishwa.
 
For what what I gather penicillin has to be taken with an empty stomach so do ampicillin but amoxicillin and cloxacillin so the answer will be ampicillin. Lakini nitatafuta jibu vizuri kesho na wengine wanakaribishwa.

Dokta,penicillin is a group of antibiotics,hizo zote alizotaja ni mifano ya penicillins
 
Dokta,penicillin is a group of antibiotics,hizo zote alizotaja ni mifano ya penicillins
tuliongelea strength, sasa sikuwa na BNF lakini ninavyojua nilijibu kwa experience. Ninaelewa zote ni antibiotics mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…