Historia ya Sarafu Yetu Tanzania

Mwl. Prof Kichuguu,

Nashukuru sana kwa hiyo elimu.............nimeprint hiyo story na kuwapa wanangu wamefurahia sana

Once again thanks

Mzee Ogah, umerudi kusoma hii kitu tena leo baada ya miaka mitano tungu tuiongelee? Nimepata notification na kuisoma nikakuta ni Mzee Ogah bado anatoa kudos tena: asante sana.

Wakati ule nilifanya research ya kina sana kuhusu tofauti ya pesa zetu (Kenya Uganda na Tanzania) ndipo nikaibua stori hii ndefu sana.

Nashukuru kama imekuwa na impact ya muda mrefu kwa watu wengi kwa muda mrefu kwa sababu nakumbuka tulimaliza kuijadili mwaka 2007, na kuanzia hapo nimekuwa napata messages za wanachama wapya mara kwa mara kila wanapoisoma. Ni miaka mitano imepita tangu niiandike; nilianza research hii kipindi ambacho Saddam Hussein alipokuwa ananyongwa.

Nakumbuka sana wakati huo kwa sababu niliacha project hii kwa muda kama wa mwezi mmoja hivi ku-reflect thamani ya uhai kutokana na video ya sadama alipokuwa anwekwa kitanzi na baadaye kuonekana akiwa kwenye sanda. Baada ya kuwa nimekusanya data za kutosha, sikuweza kupata muda wa kuziweka zote sawasawa mpaka wakati wa summer kwa vile nilikuwa na picha nyingi sana ambazo zilihitaji kupangwa kulingana na timeline ya stori yenyewe.

Hata hivyo summer ilipofika nikajikuta nalazimika kuzunguka barabarani na familia kwa takribani miezi miwili hadi mwishoni mwa July tuliporudi nyumbani ndipo nikaanza kuiweka sawasawa kwa makini (subject to typing errors).

Again, nafurahi kuwa kuna watu wengi wameiona ni both entertaining and educative!
 
Many thanks kichuguu for this.
 
Kichuguu!


Mkuu ina maana kabla ya uhuru nchi za Africa mashariki zilikuwa zinatumia sarafu au hela ya aina moja?je kabla ya uhuru kila nchi haikuwa na hela yake,maana kwenye hizo sarafu naona kuna 1952 halafu imeandikwa East Africa Sh.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Ousofia, Kuanzia mwaka 1920 nchi za Afrika ya mashariki zilikuwa zinatumia sarafu moja; sarafu ya kwanza ilikuwa ni East African Florin, ambayo ilikuwa replaced na East African Shilling baada ya muda mfupi usiozidi miezi sita. Nchi hizo zilitengana mwaka 1966 ambapo kila nchi ikawa na sarafu yake ingwa zote zileiendelea kutumia Shillingi; yaani kukawa na shilingi ya Kenya, shillingi ya Uganda na Shillingi ya Tanzania.
 
Last edited by a moderator:

Hizi nimewahi kuzitumia. Kabla Nyerere hajaleta visungura na visamaki vyake.
 
Umaskini kuondoka lazima tuanzie huku mara Lowassa awapo Magogoni.

Ili kurudisha heshima ya Pesa yetu Shillingi kuna haja hili kuwa halisi na tuache uchumi wa kwenye makaratasi!

The current coins in circulation are as follows: =/05, =/10, =/20, =/50, 1/=, 5/=, 10/=, 20/=, 50/=, 100/= and 200/=.

[h=3][/h]
Profesa Ndulu kuelekea 25/10/2015 kuna haja vijana wako kubadilika maana Mabadiliko haya epukiki.






CC Ben Saanane.
 
Last edited by a moderator:
Hili somo adhimu linaumbusha mbali na kuibua vitu ambavyo wengine hatukuvijua
 
shukrani na nitaanza kuhifadh baadh ya sarafu za sasa kwa ajili ya kumbukmbu ya wanangu na vijukuu na vitukuu
 
Tunakushukuru pia uliepandsha uzi huu leo, tusingeyajua haya
 
Ahsante Kichuguu kwa shule.. Ila nakumbuka sijui ni shule ya msingi au sekondari tulisoma Mji wa kwanza kutengeneza Fedha yake yenyewe ni kilwa. Ila nimeshangaa sijaona popote pale Zanzibar ikitajwa.. Nahitaji ufafanuzi
 
A very useful thread! Mimi nimehifadhi shilingi tano ya Afrika mashariki, ya mwaka 1958: I hope itakua useful huko mbeleni!
 
Asante sana mzee kwa elimu hii, umenifungua macho sana kuhusu historia ya shilingi yetu
 
Mkuu, Asante sana. Ama kwa hakika hili ni shamba darasa, cha kufanya naomba u-update huu uzi, ni miaka 11 sasa.
 
Dah uzi murua wa kumbukumbu.Hiyo senti hamsini ya kasungura tukiwa wadogo tuliitumia kununua pipi za vidonge kwenye duka la mzee mmoja kijijini kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…