Historia ya Savimbi

Historia ya Savimbi

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
8b4780ea2c5f5449bfa7f85a2ef5ef60.jpg


JONAS MALHEIRO SAVIMBI, MWANAHARAKATI ALIYEBADILIKA KUTOKA MSOMI NA MWANAMAPINDUZI MPAKA KIBARAKA NA KIBAKA KWA WATU WAKE WA ANGOLA.


Na, Comred Mbwana Allyamtu.

Sunday - 01/10/2017.


JONAS MALHEIRO SAVIMBI Agosti 3, 1934 ndiyo siku aliyoletwa duniani, katika mji wa Munhango, Jimbo la Moxico katika kitongoji cha Reli ya Benguela, nchini Angola. Baba yake Savimbi alikuwa Mkuu wa Kituo cha Reli Benguela enzi za ukoloni na pia mchungaji wa Kanisa la Kiprotestant lilioanzishwa na Misionari kutoka Marekani. Savimbi aliyelelewa kwenye mazingira ya Kikristu na kusoma shule za seminari za Kiprotestant na Katoliki, anadaiwa kunusurika majaribio 15 ya kuuawa kutoka kwa wanajeshi wa Angola.

Savimbi, alikuwa mwanasiasa na mwanzilishi wa Chama cha Unita, ambaye pia alikuwa kiongozi wa Jeshi la Ukombozi la Unita, kama ambavyo mwenyewe alikuwa akiliita. Pia Savimbi alikuwa kiongozi pekee wa waasi wa msituni waliopigana ndani ya Angola mpaka taifa hilo lilipopata uhuru.

Savimbi alisoma Elimu ya dawa huko Lisbon Ureno na alipata Elimu kwa kiwango cha PhD katika falsafa katika Chuo Kikuu cha Lausanne. Aliporudi nchini kwake Angola alitaka nafasi ya uongozi katika chama cha MPLA ambacho kilikuwa na mitazamo ya Marxist (Movement ya Watu kwa Uhuru wa Angola), ambapo chama hicho kilianzishwa mwaka wa 1956 na Kiongozi wake aliye tambulika wakati huo Kama Agostinho Neto.

Baadae alijiunga na chama cha FNLA kilicho kuwa kikiongozwa na Holden Roberto Wa chama kilicho jitambulisha Kama (National Front for Liberation of Angola) mwaka 1964. Ambaye Kiongozi huyo Roberto aliendesha halakati zake za ukombozi kutoka Kinshasa Kongo. Hata hivyo Miaka miwili baadaye, mwaka 1966, Savimbi alianza harakati yake mwenyewe, kwa kuanzisha chama chake mwenye kilichoitwa UNITA (- Umoja wa Kitaifa wa Uhuru wa Angola). Savimbi Alisafiri hadi China kupata silaha na msaada na kupata mafunzo katika vita vya guerrilla. Lengo rasmi lilikuwa ni kupindua utawala wa kikoloni wa Kireno.

Jonas Savimbi mwenye umaarufu wa kimataifa ni zao la siasa baridi (wakati wa mivutano wa mataifa makubwa wakati huu baina ya USSR na USA). Awali, kundi la waasi wa Unita lilianza kama kundi la wapiganaji wa msituni waliokuwa wakipambana na utawala wa kikoloni wa Ureno kuanzia mwaka 1966 mpaka mwaka 1974. Hata hivyo Savimbi Aliyebadilika kutoka msomi na mwanaharakati aliyepigania uhuru wa watu wake wa Angola mpaka kibaraka aliyepigania madaraka na kuuawa kama kibaka!.

Savimbi, awali, alishirikiana na FNLA na MPLA lakini baadae Ureno ilipoliachia koloni la Angola, yakatokea mapambano ya kutaka madaraka ya uongozi wa nchi, Baada ya kupatikana uhuru mwaka 1975, Savimbi na kundi lake waligeuka na kuwa kundi la waasi na kuanzisha vita dhidi ya Serikali ya Chama cha MPLA Savimbi akakwama katika mapambano hayo.

Baada ya minyukano hiyo baadae savimbi Akaondoka na UNITA yake. Hapa ndipo mashaka yalipoanza. Angola ilipopata uhuru Novemba, 1975 na Ndugu Agustino Neto na chama cha kijamaa cha MPLA kuongoza nchi, dola za kibepari hazikuridhika kuona ujio wa taifa jipya linalofungamana na Urusi. Uasi huo ulizaa vita ya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 1975 mpaka mpaka Februari 22 mwaka 2002. Vita ilikomaa baada ya Savimbi kuuawa na wanajeshi wa Angola.


Ikumbukwe, Msumbiji ilipata uhuru Juni 1975 na kufungamana na Urusi pia Savimbi akashawishiwa na nchi hizo za magharibi na kupewa msaada wa fedha na silaha, akawa wakala wa nchi hizo na kuanzisha mapambano ya silaha ili kuing’oa serikali iliyo madarakani. Mbaya zaidi, misaada hiyo ikawa inamfikia kupitia serikali ya makaburu ya Afrika Kusini ambayo nayo ilikuwa ni adui wa serekali ya Agustino Neto wa MPLA kutokana na mistijala hiyo pia taifa la makabulu la Afrika kusini ilikuwa inaiogopa Urusi. Kutokana na hali hiyo iliamua kuisapoti kikundi cha waasi cha UNITA cha Savimbi.

Vita alivyoanzisha, ni moja kati ya vita ndefu na mbaya ya wenyewe kwa wenyewe kutokea Afrika baada ya nchi kuwa huru. Vita ilikuwa ndefu kwa sababu serikali ya Angola ilipata Wajamaa wa kuipigania. Urusi ilitoa msaada wa kifedha na silaha na Castro akatuma wapiganaji ambao, kwa ushindi mkuu, wakafanikiwa kuihami serikali ya Luanda. Madhara ya vita hivi nchini Angola yapo hata leo!.

Mara tu baada ya dola la Urusi kusambaratika na ujamaa kuanza kupururuka duniani, nchi za magharibi zikaona huduma ya Savimbi hawaihitaji tena. Alikuwa ni mfano wa ganda la muwa. Utamu umekwisha, la nini tena kinywani! Wakamtema, wakamsitishia misaada yote na kumtelekeza.

Angola iliporuhusu vyama vingi Mwaka 1991, Unita ilikubali kusaini mkataba wa kusitisha mapigano na MPLA na kukubaliana kuwa chama hicho cha Savimbi kiwe huru kushiriki chaguzi mbalimbali. Hata hivyo, pamoja na kushiriki chaguzi hizo, Unita ilishindwa kupata ushindi mwaka 1992, jambo lililomchukiza Savimbi na kuamua kurudi msituni kupambana na Serikali ya Angola.

Savimbi Alipo kwama katika uchaguzi akarudi pori. Akasalia kibaka akiuza almasi za Angola kwa magendo ili kuzimudu harakati-pori. Hata hivyo, mwisho wa Savimbi ulikuwa Februari 22, 2002 alipovamiwa kwenye ngome yake ya kijeshi kwenye mji alikozaliwa na kuuawa na majeshi ya Angola, yaliyokuwa yakimsaka kwa muda mrefu. Kifo chake, akiwa amevurugwa kwa risasi pekee yake bila makamanda wa kumhami ni ulikuwa ni ushahidi wa mkwamo uliokuwa unamkabili


[emoji768]Wako Mjuvi wa Historia ya dunia na mambo ya dipromasia ya dunia......
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu

5d0b25b52570edd1bd8d676b3f369edc.jpg
 
Back
Top Bottom