mheshimiwamtemi
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 291
- 218
"Shikamoo" limekuwa ni neno linalotumika kuonesha heshima baina ya watu. Desturi na tamaduni za Afrika mashariki hutumia neno hili kama salamu ambapo anayeitikia husema "Marhaba".
Pengine umewahi kujiuliza mini hasa maana ya "Shikamoo" Binafsi nakumbuka kuna Mzee mmoja aliwahi kunitukana nilipomsalimia shikamoo cha ajabu hakuniambia sababu zaidi ya kusema "unajua maana yake?".
Ukoloni na utumwa ulitawala Afrika Mashariki tangy karne ya 8. Hapo awali maingiliano baina ya Waarabu na wenyeji wa upwa wa Afrika Mashariki yalikuwa ya kibiashara zaidi. Tangy biashara ya Utumwa ishamiri kuanzia Marne ya 14 na kuendelea wenyeji hao wenye miili mikubwa na nguvu walinunuliwa na kuuzwa ili wakatumike katika mashamba na shughuli mbalimbali za waarabu.
Wengi tunakumbuka jinsi biashara ya Utumwa ilivyokuwa haramu na dhariri. Masoko ya kuuza na kununua binadamu kama bidhaa zingine yalifunguliwa. Baadhi ya maeneo hayo ni Zanzibar na Bagamoyo ambapo watumwa walipelekwa kwa ajili ya kuuzwa.
Katika biashara hiyo ilikuwa ni kheri ya Utumwa aliyepata mteja wa kumnunua kuliko yule aliyekaa sokoni muda mrefu kwani alikuwa anateseka na kuteswa hali iliyowafanya wengine kupoteza maisha.
Hali ilikuwa hivi, wakati waarabu na wanunuzi kutoka middle east na far east walipofika sokoni ilimpasa mtumwa kujipogia deve yaani kushawishi ununuliwe. Kwakuwa watumwa hawakuruhusiwa kuongea maneno mengine basi iliwapasa kusema "Shikamoo" wakimaanisha mnunuzi ashike ndani ya mfuko wake wenye fedha ili amnunue... Baada ya kujua bei mnunuzi aliitikia "Marhaba" akimaanisha Mali haba yaani hakuna na kiasi kile cha fedha kutosha kumnunua Utumwa yule.. Basi Utumwa aliangua kilio.
Leo tunatumia kama salamu. Yapi ni maoni yako mdau wa JF? Tuendelee au kuache kusalimiana shikamoo?