Historia Ya Siasa Tanzania Na Wanasiasa Wake Mashuhuri

Historia Ya Siasa Tanzania Na Wanasiasa Wake Mashuhuri

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,509
Reaction score
23,653
Habari wana JF,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nia na malengo ya kuanzisha thread hii ni kukumbushana/kuelimishana/kupeana mawazo/kupeana mtazamo na kuelezana juu ya historia ya siasa nchini (na wana siasa kwa ujumla).

Pia kuangalia chimbuko la siasa ya Tanzania na historia za wanasiasa wakongwe/chipukizi ambao wameunda/wanaunda mizizi na taswira ya nchi yetu ki siasa.

GEORGE ORWELL alinena, nanukuu;

"Katika zama zetu hizi, hakuna kitu kinachoitwa "kujiweka mbali na siasa", kwani kila kitu ni siasa, na siasa yenyewe ni mshikamano wa maswala kedekede...."

Historia ya siasa ni ufafanuzi na uchambuzi wa mambo muhimu yaliowahi kutokea kuhusu siasa, mawazo, mageuzi, mihimili ya serekali, wapiga kura, vyama vya siasa na viongozi. Pia jambo hili linaingiliana na pande nyingi za historia kama vile Historia ya kidiplomasia, Historia ya katiba na Historia ya umma.

Hayo machache,

Wito wangu,

1) Tukumbushane juu ya wanaharakati wowote waliowahi kutokea nchini wa siasa (kutoka chama chochote kile kilichowahi kuwepo au ambao hawakua na chama maalum).

2) Wanamageuzi wa siasa. (Walioi shape na kuibadilisha siasa nchini kwa mazuri na yasiyo mazuri)

3) Wana diplomasia mahiri nchini.

4) Chochote muhimu kinachohusiana na hayo juu.

5) Mtag mwanasiasa yoyote unaehisi anaufahamu wa siasa na kutupa baadhi ya mambo muhimu.

#Changia jambo/mtazamo unaofahamu kwaajili ya kuelimisha tu, na tafadhali usichangie mambo yasiyokua muhimu na yenye nia ovu.(pita kimya kimya bila kuchangia chochote kama huna jambo muhimu la kuelimisha)

Ahsante,

Zitto
 
Historia ya uchaguzi,

Historia ya uchaguzi nchini inaweza kugawanywa katika makundi matatu; Chaguzi tatu chini ya mfumo wa vyama vingi zilifanyika enzi za Tanganyika, chaguzi hizo mbili zilifanyika kabla ya uhuru mwaka 1958 na 1960 na uchaguzi wa tatu ulizofanyika Novemba Mosi mwaka 1962 baada ya uhuru, kabla ya Tanganyika kuungana na Zanzibar.

Baadaye kukafuatia miongo mitatu ya utawala wa chama kimoja na kulifanyika chaguzi sita; uchaguzi wa mwaka 1965, uchaguzi wa 1970, uchaguzi wa 1975, uchaguzi wa 1980, uchaguzi wa 1985 na uchaguzi wa mwaka 1990.
Mfumo wa vyama vingi ulirejeshwa nchini mwaka 1992 na tangu wakati huo kumekuwa na chaguzi nne; uchaguzi mkuu wa 1995, uchaguzi wa mwaka 2000, uchaguzi wa mwaka 2005 na uchaguzi wa mwaka 2010. Katika historia hiyo, kumekuwa na chama kimoja tu ambacho ndicho kimeendelea kutawala, CCM kilichoundwa mwaka 1977 baada ya muungano wa vyama viwili vya TANU na ASP.
Uchaguzi wa kwanza uliofanyika nchini 1958 kwa ajili ya kuchagua wabunge ulikuwa ukijulikana kama uchaguzi wa karata tatu. Uchaguzi huo ndio uliopima ukomavu na nguvu ya Tanu kama sehemu ya maandalizi ya kuondokana na utawala wa kikoloni.

Uchaguzi wa karata tatu,

Uchaguzi huo ndiyo uliopima ukomavu na nguvu ya Tanu kama sehemu ya maandalizi ya kuondokana na utawala wa kikoloni.

Katika uchaguzi huo, wapigakura walitakiwa kuchagua mgombea mmoja kutoka kila kundi: Mwafrika, Mhindi na Mzungu, hivyo kupata wagombea watatu. Kwenye kitabu chake cha Modern History of Tanganyika alichotunga 1976, Mwanahistoria wa Kiingereza John Iliffe alisema, uchaguzi wa aina hiyo ulidhaniwa kuwa ungemaliza migongano. Hata hivyo, serikali ya kikoloni iliweka sifa ya mpigakura kuwa ni pamoja na kipato cha Paundi 150 kwa mwaka, elimu ya miaka minane au kuwa na ofisi inayotambulika.

Mwanzoni sifa hizo zilipingwa na Tanu ambayo ilitishia kujitoa kwenye uchaguzi huo, ikisema kuwa Waafrika wengi maskini, wasiokuwa na ajira wangezuiwa kupiga kura. Lakini baadaye kikundi cha wanasiasa wa Tanu chini ya Mwalimu Nyerere, kiligundua kuwa kugomea uchaguzi huo kungechelewesha uhuru wa Tanganyika au kungetoa mwanya wa ushindi rahisi kwa chama pinzani cha United Tanganyika Party (UTP) kilichokuwa kikiendeshwa na walowezi wa kizungu.

Katika mkutano wake wa mwaka, uliofanyika Januari 1958, Tanu kilikubali kushiriki uchaguzi huo. Wakati huo pia Tanu ilikuwa na migogoro ya ndani iliyosababisha mmoja wa waanzilishi wake, Zuberi Mtemvu, kujitoa na kuanzisha chama kipya cha African National Congress (ANC).

Pamoja na tofauti hizo, Tanu ilifanikiwa kupata ushindi mnono baada ya kupata viti 28 kati ya viti 30 vilivyokuwa vikishindaniwa. Mwaka 1960 ulifanyika uchaguzi wa wabunge na Tanu kikaendeleza ushindi wake kwa kupata viti 70 kati ya viti 71 vilivyokuwa vikishindaniwa.

Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9, 1961 na Mwalimu Nyerere akawa Waziri Mkuu chini ya usimamizi wa Malkia Elezabeth wa Uingereza. Januari mwaka 1962, Mwalimu Nyerere alijiuzulu wadhifa huo na Rashidi Kawawa akachukua nafasi yake. Nchi ikawa Jamhuri na ilianza kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa rais Novemba 1962. Katika uchaguzi huo wa rais, Chama cha Tanu kilikabiliana na Chama cha ANC na wapigakura milioni 1.8 walijiandikisha. TANU ilishinda kwa asilimia 98.15 na Nyerere akawa Rais wa Tanganyika.

Baada ya uchaguzi huo Tanganyika ikawa taifa la chama kimoja cha siasa na mwaka 1964 iliungana na Zanzibar na kuunda Tanzania.

Wakati wa demokrasia ya chama kimoja, utaratibu wa uchaguzi uliokuwapo ni Kamati ya Utendaji ya Tanu kuchagua watu wawili na kuwapeleka kwa wapigakura kwa ajili ya kumpata mbunge. Lakini katika nafasi ya kiti cha urais, utaratibu huo ulikuwa unamhusisha mtu mmoja aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu wa vyama vya Tanu na ASP. Baada ya mtu huyo kupita, alitakiwa kuthibitishwa na mkutano wa uchaguzi. Wapigakura walikuwa wanapiga kura ya ndiyo au hapana.

Mfumo huo wa uchaguzi, ndiyo uliomchagua Mwalimu Nyerere bila kupingwa katika kipindi chote cha utawala wake yaani mwaka 1965, 1970, 1975 and 1980, akiwa anashinda kwenye chaguzi hizo kwa zaidi ya asilimia 90. Mwalimu Nyerere alistaafu mwaka 1985 na CCM ikamchagua Ali Hassan Mwinyi kuwa rais. Hata hivyo, kulikuwa na mabadiliko makubwa mawili, kabla ya uchaguzi wa mwaka 1985: kuanzishwa kwa mfumo wa ukomo wa uongozi kwa nafasi ya rais na kupungua kwa umri wa mpigakura kutoka miaka 21 hadi 18.

Mwaka 1992 nchi iliingia katika mfumo wa vyama vingi. Mwaka 1995, Tanzania ikaingia rasmi kwenye uchaguzi chini ya mfumo huo wa vyama vingi, ikiwa ni miaka 33 tangu uchaguzi wa kwanza ulipofanyika mwaka 1962. Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 1995, CCM ilimteua Benjamin William Mkapa na akashindana na watu watatu kutoka vyama vya upinzani: Augustine Mrema aliyekuwa anakiwakilisha Chama cha NCCR- Mageuzi. Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na John Cheyo wa UDP. Katika uchaguzi huo Mrema ndiye aliyeonekana tishio kwa CCM, lakini mwishoni Mkapa alishinda uchaguzi huo kwa kupata wa asilimia 61 ya kura zilizopigwa na Mrema alipata asilimia 27.

Miaka mitano baadaye, Mkapa alishinda tena kwa asilimia 71, akifuatiwa na Profesa Lipumba aliyepata asilimia 16, NCCR haikusimamisha mgombea katika uchaguzi huo na Mrema ambaye wakati huo alikuwa ametoka NCCR na kujiunga na Chama cha Tanzania Labour (TLP) alipata asilimia saba.

Mwaka 2005 CCM ikamteua Jakaya Kikwete kuwa mgombea wake wa urais na alishinda kwa asilimia 80, akifuatiwa na Profesa Lipumba aliyepata asilimia 11. Rais Kikwete alifanikiwa kutetea nafasi yake hiyo mwaka 2010 alipopata asilimia 62, akifuatiwa na Dk Willibroad Slaa wa Chadema ambaye alikuwa wa pili baada ya kupata asilimia 27.

(Iliandikwa na Athumani Mtulya, 17.06.2015 katika mwananchi.co.tz)
 
Ni Lord Lofa tu mwenye guts za kuliambia Jiwe wewe 2020 usichukue form. Mr Handsome hawezi wala mzee Ruksa ambae anataka mwanae akabidhiwe Zenj.
 
Professor Ibrahimu Lipumba, ni mwanasiasa nguli na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwmo nafasi ya wadhifa wa kuwa mshauri wa raisi katika masuala ya uchumi.
 
Back
Top Bottom