Historia ya Taifa la Iran

Historia ya Taifa la Iran

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Historia ya Iran

Iran ni taifa la kihistoria kuliko hata Marekani, ingawa pia Marekani pia ni taifa la kinabii, kwa wakati mwingine tutakuja kuona siri ya Marekani na mwisho wake. Iran kibiblia inaitwa Elam na wakazi wake wanaitwa Waajemi, mda mwingine Elam iliitwa Uajemi[Persia]. Hawa si waarabu bali ni Waajemi au wafursi kama wanavyoitwa na Waarabu.

Elamu mara nyingi hutajwa katika Agano la Kale. Taifa hilo lilitoka kwa Elamu, mwana wa Shemu, Mwanzo 10:22. Imetajwa kuwa nchi ya Elam ilikuwa katika muungano na Amraphel, mfalme wa Shinari[Iraq], na Arioki, mfalme wa Ellasar, na Tidal, mfalme wa mataifa, Mwanzo 14: 1. Kati ya mataifa haya katika muungano huo, Chedorlaomer, mfalme wa Elamu, alikuwa mkuu wao, Mwanzo 14: 4.

Hawa kwa pamoja walishambulia falme tano kuu za kanaan ikiwemo Sodoma na Gomora na kuzishinda, hizi falme tano zilikuwa chini ya chadorlaomer baadae wakamwasi ndipo vita vya kurudisha makoloni vikatokea, Chedorlaomer na washirika wake waliua sana na waliteka nyara nyingi sana pamoja na kumteka tajiri Lutu mpwa wa ibrahimu. [Mwanzo 14:1-12].

Bila shaka taifa la Elam zama hizo ndilo lilikuwa super power ya dunia. Ila cha ajabu mtumishi wa Bwana Ibrahimu akiwa na wanajeshi 318 ambao ni vijana wake wa nyumbani pamoja na wanajeshi wa rafiki zake kadha wa kadha walimshinda Chedorlaomer na wafalme hao watano ambao ni washirika wake na kuwafukuza kutoka Kanaan mpaka Syria, wakawanyang’anya nyara zote na kumwokoa Lutu mpwa wa Ibrahimu aliyetekwa na mfalme huyo mkuu. [Mwanzo 14:13-17].

Tazama pia Ezra 2: 7; Ezara 8: 7; Nehemia 7:12, Nehemia 7:34; Isaya 11:11; Isaya 21: 2; Isaya 22: 6, nk Elam imetajwa pia kama sehemu ya ufalme wa Uajemi, na Danieli aliishi Shushani, ambayo ni katika mkoa wa Elamu, Danieli 8:2. Wagiriki na Warumi waliipa nchi hii jina la Elymais. Sasa Elam inaitwa Kusistan. Eneo hili la Elam lifungwa na Uajemi upande wa mashariki, na Media upande wa kaskazini, na Babeli upande wa magharibi, na Ghuba ya Uajemi kusini. Waelamu walikuwa watu wa vita, na walisifika kwa matumizi ya upinde, Isaya 22: 6; Yeremia 49:35.

Lugha ya watu hawa kwa kweli ni ya Kiajemi. Ikulu yake, Shusan, iliyoitwa na Wagiriki Susa, ilitukuzwa sana. Inasemekana mji wa Elam ulikuwa na maili kumi na tano sawa na kilimeta 24, na huko kulikuwa na ikulu/jumba la kifalme lililopambwa la Ahasuero mfalme mkuu wanne wa Uajemi aliyemwoa Esta binti wa Kiyahudi. [Tazama kitabu cha Esta]. Wakazi wake bado wanajifanya kuonyesha huko kuwa lipo kaburi la nabii mkuu Daniel.

Ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya pili na mstari wa 9 utaona wa Parthia, Wamedi na Waelami pia walikuwepo siku ile ya Pentekoste nao walimpokea Yesu na kubatizwa. Waparthia, Waelemi na Wamedi wote walikuwa katika taifa moja la Uajemi/Iran, hapo wanatajwa kwa uzito wao kulingana na umaarufu wa makabila yao. Hivyo historia ya Iran ni historia kongwe toka zama za miaka ya 3700 kabla ya Kristo, hivyo si rahisi kukubali kuwa chini ya taifa lolote lile.

Kuna wakati dunia ilipata mataifa mawili makubwa Misri na Ashuru, haya mataifa yaligombania nafasi ya kutawala dunia, vita vilipiganwa sana, wakati huo Elam/Iran ilikuwepo lakini ilizidiwa kijeshi na mataifa haya. Lakini Ashuru iliibuka mshindi, taifa hili makazi yake yalikuwa huko Mesopotamia, leo ndio Iraq; Ashuru walitawala sehemu kubwa ya dunia ya wakati ule, walikuwa ni taifa hatari sana kijeshi, waliitwa mabwana wa vita, ilifika mahali walimtukana Mungu wa Israeli wakati ule wameenda kuhusuru mji wa Yerusalem zama za mfalme Hezekia. Mungu alimtuma malaika wake mmoja tu katika jeshi la Ashuru, akawaua wanajeshi 185,000 wa Ashuru akabakia mfalme wao tu, Senekerebu.

Akakimbia mpaka katika nchi yake na huko aliuawa na wanawe wawili, ilikuwa ni moja ya hukumu ya Mungu dhidi yake. [Tazama Isaya sura ya 37 na 38]. Zama hizo ufalme wa Babeli ulikuwa unainukia lakini walikuwa wamewekwa chini ya Ashuru, waliposikia habari hiyo, mfalme wa Babeli alimtuma mtoto wake na maofisa wake ili wajifunze imekuaje taifa dogo la Yuda liwashinde wanajeshi 185,000 wa taifa kubwa la Ashuru ambalo limeiweka dunia nzima chini yake? Na pia walikuja kujifunza siri ya uponyaji wa Hezikia pamoja na vivuli vya jua kurudi nyuma kwa madaraja kumi kama ishara ya uponyaji wa Hezekia.

Lakini cha ajabu mfalme hakuwaonesha siri ya mambo hayo matatu bali akawaonesha silaha zake na utajiri wake, jambo hilo lilimuudhi sana Mungu, na akatoa unabii kupitia nabii Isaya kuwa siku moja Babeli itaitawala Yuda maana mfalme wa Yuda hakumpa Mungu utukufu zaidi ya kujipa yeye binafsi. [Tazama Isaya 39].

Ashuru iliendelea kuwa taifa kubwa kwa mda, lakini mwisho nguvu zake zilikomeshwa na ufalme wa Babeli ambao uliungana na ufalme wa Umedi dhidi ya Ashuru. Lakini Babeli ilizidi kupata upinzani kutoka Misri, Yuda na Elamu, lakini jeshi la Babeli chini ya Nebukadreza waliibuka washindi baada ya kushinda jeshi kubwa la Farao Neko huko Iraq. [Yeremia 46:2]. Ndipo Elamu na Yuda nazo zikashindwa kijeshi na kuingizwa katika utawala wa Babeli, ila kwa kiburi cha Wayahudi kulimfanya Nebukadreza awaangamize kwa hasira kali na kulibomoa Hekalu la Suleimani na kuwachukua Wayahudi wengi utumwani akiwemo nabii Danieli.

Lakini baadae taifa la Elam/Uajemi liliasi utawala wa Babel na mwaka 539 Uajemi chini ya mfalme Koreshi alimshinda mfalme wa Babeli na kuuteka mji wa Babeli, ndipo tokea hapo Uajemi ikawa taifa kubwa sana duniani. Taifa hili lilianza kama taifa la demokrasia iliyojali wanyonge mpaka viumbe, Koreshi alitoa uhuru kwa mataifa yote ambayo yalikuwa yamewekwa chini ya utawala wa kidikteta wa Babeli likiwemo taifa la Yuda. Alisaidia taifa hili kujijega mpaka kuwa taifa huru tena mpaka zama za masihi mkuu Yesu Kristo. Koreshi anachukiliwa leo kama mwanzilishi wa tamko la uhuru wa kidemokrasia, na tamko lake ni kama ifuatavyo.

“Mimi ni Koreshi, Mfalme wa Ulimwengu, Mfalme mkubwa na wa haki, Mfalme wa Babeli, Mfalme wa Sumer na Akkad, Mfalme wa pembe nne za Ulimwengu, mwana wa Cambyses… Wakati niliingia Babeli kama rafiki na kupanda kwenye kiti cha enzi huku kukiwa na shangwe na furaha kuu katika ikulu ya maliwali, askari wangu isitoshe walitembea Babeli kwa amani na Uaminifu, nilikataza unyanyasaji na ugaidi kote Sumer na Akkad. Nilipigania amani, huko Babeli na katika miji mingine yote……Nilikomesha kazi ya kulazimishwa kwa heshima wa raia wa Babeli… ambayo ilikuwa dhidi ya heshima yao ya kijamii. Nilisaidia kurejesha nyumba zilizoharibiwa ... Niliwapa wote makazi tena na mahali pa amani. Bata na njiwa… nilijaribu kuhifadhi makazi yao.”

Hayo maneno yalipatikana katika jagi[cylinder] lililopatikana huko Iran kupitia watafiti wa mambo ya kihistoria. Demokrasia ya koreshi si kama ya leo ya wengi wape, bali ilikuwa ni utawala wa kisheria ambao unajali mpaka haki za wanyonge katika matakawa ya wengi. Kuhani Ezra naye aliandika moja ya tamko la uhuru la Koreshi juu ya Yuda.

“Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,

Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee. 2 Mambo ya Nyakati 36:23].”

Taifa hili linachukuliwa kama mfano wa taifa la Amerika leo, mababa walioanzisha taifa la Amerika [America Founding Fathers] walipendezwa na aina ya serikali ya Koreshi, na jambo hilo ndilo lilimfanya rais Jefferson kuandika katiba ya Marekani kufuatana na serikali ya Koreshi. Jambo hili tutaliona wakati mwingine, maana kuna kufanana kukubwa baina ya mataifa haya mwanzo wao na mwisho wao. Baadae taifa hili [Uajemi] lilitoka kuwa katika hali ya Kondoo-upole na kuwa kama Dubu mla nyama-udikteta.

Taifa hili lilijipanua hadi Afrika, lilipigana na Misri na Kush[Sudan na Ethiopia] na kushinda, na likajipanua hadi huko Afghanstan, India kwa upande wa mashariki, na kwa upande wa magharibi, likaitwa asia ndogo[Uturuki] ambao ilikuwa ni miji ya ugiriki kabla ya waturuki hawajahamia huko kutoka asia ya kati. Uajemi ilijipanua hadi Ulaya, na kutawala dola za kigiriki kwa mda wa mwaka mmoja zama za Ahusuhero mkuu. Taifa hili likawa taifa kubwa sana kijeografia kiasi cha mfalme Ahusuero kuwafanyia sherehe maofisa wote dunia nzima kwa siku 180. [Esta 1:1-5].

Lakini wagiriki walikuwa ni mashujaa sana walifanikiwa kuondoa dola la uajemi huko Ulaya na kulisukumia mpaka asia ndogo. Dario mkuu na mwanae Ahusuhero wote walishambulia Ugiriki-Ulaya. Jaribio la Dario halikuwa na mafanikio makubwa, lakini Ahusuhero alichochea vita kwa majeshi mengi, na kuwaongoza wote kwa njia ya ardhi na bahari, dhidi ya Nchi za Kigiriki. Baada ya kushinda vita kadhaa na kuikalia Ugiriki kwa muhura mmoja, Wagiriki walijipanga chini ya uongozi wa Spartan, na kwa uchache wao walifanikiwa kuzamisha meli za Kiajemi na kuziaangamiza, na Jeshi la ardhini la Kiajemi lilifukuzwa nje ya Ugiriki mwaka mmoja baadaye.

Matumaini ya Uajemi ya kudhibiti maji ya Aegean-Ugiriki yalishindwa kabisa; na Ahusuhero akakimbia na jeshi lililobakia. Wakati huo, Wagiriki walikuwa wamepata nguvu. Hivyo picha sasa inatoka katika Dola ya Uajemi ambayo inayumba kuelekea anguko lake. Katika kuteteleka kwao wafalme kadhaa wa Kiajemi wengi baada ya Ahusuhero waliendelea kutawala lakini si kwa mamlaka kubwa, mpaka zama za Dario aliyeangushwa na Alexender mkuu toka Ugiriki.

Je ni nini kitaendelea baada ya hapo? Subiri sehemu ya pili.

FB_IMG_1578247055502.jpeg
 
Naiona Dola ya Amerika ikielekea kuangua.
"POWER IS NOT PARMANENT"
[emoji769][emoji2400][emoji2398] $ Muwe na aibu, unadiriki kusema Maneno hayo uku ukiwa unatumia Twitter, Facebook, Google, Instagram, YouTube, Maps, satellites, Wikipedia, Shazam, Western Union, Coca-Cola, WhatsApp, Android, window, Symbian, iPhone, IOS, ATM
Izo nchi unazozisema zimeshindwa izo projects, sasa watapambanaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hakuna kipindi dunia imeishi bila kuongozwa na dola fulani kubwa..hii dola ya america haikuwepo kipindi cha nyuma, palikuwa na wababe wengine ambao kwa nyakati zao waliongoza dunia'

Hujawai sikia dola la rumi? (Rumi empire) uajemi, hujui kuhusu misri chini ya farao?

Au wewe unajua ni hadithi tu za kutunga!!?

Kipidi hicho hiyo marekani inayoisema ilikuwa si loloote!

Nyie wcb ni shidaaa!!
Embu zitaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom