Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HISTORIA KATIKA PICHA MBILI 1955 NA 1993
Picha hizo mbili hapo chini zimepishana miaka 38 kwa mkato na kifupi unaweza kusema zimepishana miongo minne yaani miaka 40.
Picha ya kwanza ni mkutano kwa kwanza wa mwaka wa TANU Ukumbi wa Ghandhi, Hindu Mandal Dar es Salaam na picha ya pili ni kumbi wa Arnautoglo.
Yote ni mikutano ya chama cha siasa.
Wanachama wa vyama hivi viwili wamefanana kwa kila kitu lau kama ni watu waliopishana kwa mbali sana katika wakati na wastani wa umri.
Angalia picha hizo kwa makini hili utaliona.
Katika mkutano wa TANU wa mwaka wa 1955 kuna wazalendo wawili walikuja kuwakilisha Southern Province wakitokea Lindi.
Hawa walikuwa Salum Mpunga na Ali Mnjawale.
Kulikuwa pia na wazalendo wengine watatu kutoka Dodoma, Central Province: Haruna Iddi Taratibu, Mahdi Mwinchumu na Said Mussa waliohudhuria mkutano ule wa TANU wa mwaka wa 1955.
Nimebahatika kuzungumza na wajumbe wawili waliohudhuria mkutano huu: Haruna Iddi Taratibu na Salum Mpunga.
Nilizungumza na Salum Mpunga alasiri moja tukiwa tumekaa kwenye baraza ya msikiti mkubwa wa Lindi jirani na stendi ya mabasi.
Haruna Taratibu alinikaribisha ofisini kwake Dodoma.
Sikutaka wamalize kunihadithia historia ya TANU.
Mfano wake ni kama unaangalia senema nzuri ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika lakini ina mwisho mbaya wa kusikitisha.
Filamu ikimalizikia kwa kuonyesha wababe wakiuliwa mmoja baada ya mwingine.
''The Sand Pebbles,'' ni filamu nzuri ya kuvutia inayoonyesha ukandamizaji wa Wamarekani Mashariki ya mbali muigizaji akiwa Steve McQueen.
Nikimpenda sana muigizaji huyu.
Mwisho wa filamu Steve McQueen anauliwa katika mapigano ya risasi.
Siku zote najiuliza ilikuwaje hata historia ya TANU yote ikafutika na nini sababu ya kufutika kwake?
Wazee hawa wawili waasisi wa TANU Lindi na Dodoma walinieleza kuwa wasomi wote waliokuwapo katika miji yao waliogopa kujihusisha na TANU.
Chama cha TANU kikaasisiwa na wao.
Salum Mpunga alikuwa dereva wa lori na Haruna Taratibu alikuwa Fundi Mwashi mwajiriwa wa Public Works Department (PWD).
Hivi ingekuwaje endapo singebahatika kukutana na wazalendo hawa na wakanihadithia historia ya TANU?
Picha: Kulia ni Haruna Iddi Taratibu na Salum Mpunga katika utu uzima wao.