Ukweli asiotaka kuueleza ni
Mohamed Said ni jinsi uhusiano kati ya walowezi Wazulu (Wakristo) na Manyema ulivyopandwa, ukakua na ukakomaa hadi wakawa ndugu wa damu.
Ukweli mwingine asiousimulia ni kilicho nyuma ya hizi jitihada zake za kutaka kuwakuza hawa walowezi wawe msitari wa mbele kama Watanganyika zaidi ya wazawa wenyewe wa asili.
Dini anaitumia tu kuficha lengo lake kwani Waislamu wazawa ni kama vile anawaweka daraja la pili. Anajua fika kuwa katika kitabu cha Watanganyika kilichotaja makabila yote ya Tanganyika wakati wa mkoloni, wazulu na Manyema hawapo.
Akafikiria namna ya kuwaingiza wazee wake kwenye historia ya Tanganyika ni kwa kutumia udini. Wazulu walikuwa ni askari vijana waliotoka vitani wakalowea Tanganyika na hawakuwa na familia.
Vijana wa Kizulu (Wakristo) wakatengewa na wakoloni eneo la Gerezani wakiishi na Manyema. Wakawaona mabinti wa kimanyema (Waislaam) kuwa ni wazuri na kutaka kuwaoa. Sharti walilopewa ili kuwaoa ni kubadilisha dini.
Undugu wa damu ukaanzia hapo na
Mohamed Said alizaliwa kwenye mazingira yanayofanana na hayo. Wajomba zake walikuwa Wazulu. Leo anawakuza wazee wake kama ndio hasa wapigania uhuru wa Tanganyika!
Vipi Watanganyika? Je bila walowezi hatungepata uhuru? Je bila wazulu na Manyema hakuna Mtanganyika angedai uhuru? Hizi nguvu zote za kuwaingiza na kuwatanguliza walowezi katika historia ya Tanganyika lengo lake hasa nini?
Eti ndio hao walowezi walioongoza mapambano ya kudai uhuru ni tusi kubwa kwa Watanganyika. Unamkuta mjukuu wa walowezi anamdhihaki hadi baba wa Taifa akidai si lolote, si chochote! Kwamba uongozi alipewa tu na wazee wa Gerezani!
Really? Naishia hapo.