Historia ya Tippu Tip

Historia ya Tippu Tip

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Hamed bin Mohammed el Murjebi (183714 Juni 1905)
800px-TipputipPortrait.jpg

Alijulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip.
Alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika Afrika ya Mashariki na Kati wakati wa karne ya 19.

HISTORIA YAKE
Babake alikuwa mfanyabiashara Mwarabu Muhammed bin Juma, mamake aliitwa Nyaso. Hamed aliingia katika shughuli za biashara tangu umri wa miaka 12 akafaulu katika biashara ya misafara kati ya Zanzibar na Kongo. Alipanga misafara ya mahamali waelfu akipeleka bidhaa kutoka Bagamoyo kupitia Tabora hadi Ujiji kwa Ziwa Tanganyika na ndani ya Kongo. Bidhaa alizobeba alitumia kujipatia pembe za ndovu na watumwa; watumwa walisaidia kubeba pembe za ndovu njia ya kurudi hadi pwani. Hemed alitajirika sana. Athira yake ilipanuka katika Kongo ya Mashariki hadi alitawala eneo kubwa sana.
Hamed akapata jina huko Ulaya kwa sababu alikutana na wasafiri na wapelelezi Wazungu kama David Livingstone, Veney Cameron, Henry Morton Stanley, Eduard Schnitzer (Emin Pascha), Hermann von Wissmann na Wilhelm Junker ambao mara nyingi walipata misaada muhimu kutoka kwake.
Wabelgiji walipoanza kujenga ukoloni wao Kongo walimkuta kama mtawala wa Kongo ya Mashariki wakapatana naye na kumpa cheo cha gavana ya Mkoa wa Chutes Stanley ("maporomoko ya Stanley", leo Kisangani) mwaka 1887 alichoshika kwa miaka michache.
Mabadiliko ya ukoloni yaliharibu biashara yake akarudi Zanzibar 1890/91 alipobaki bila misafari mipya hadi kifo chake mwaka 1905.

ASILI YA JINA LA TIPPU TIP
Jina la TIPPU TIP alipewa na kabila la Wazaramo kwasababu ya mlio wa bunduki yake uliokuwa unatoa sauti ya tip tip tip hivyo basi Wazaramo wakisikia tu mlio wa bunduki basi wanakimbia huku wakisema Tippu tip huyo anakuja.
Yeye mwenyewe aliona watumwa ni sehemu tu ya biashara yake akitajirika hasa na biashara ya pembe za ndovu.

Hamed bin Mohammed el Marjebi amejipatia nafasi katika historia ya Afrika ya Mashariki kwa kuandika tawasifu au kumbukumbu ya maisha yake yeye mwenyewe. Katika lugha ya Kiswahili ni mfano wa kwanza wa tawasifu.
Pia ni mfano wa pekee wa kumbukumbu ya kimaandishi ya matokeo ya siku zile zisizoandikwa na Mzungu lakini ny mwenyeji. Hakuwa mtu anayemuogopa Mungu.
 
Kila kitu kina mwisho, watu wote tulijue hilo ili tuheshimiane na kuheshimu utu wa wengine.
Aliwatesa wenzake lkn mwisho wao wote ni kifo, kama kuna kukutana huko tuendako labda huwa wanamzomea na kumzaba vibao kama hana gobore lake huko
 
Mziki wa huko kwa SIR GOD usipime lazima apigwe tu huyo
 
Kila kitu kina mwisho, watu wote tulijue hilo ili tuheshimiane na kuheshimu utu wa wengine.
Aliwatesa wenzake lkn mwisho wao wote ni kifo, kama kuna kukutana huko tuendako labda huwa wanamzomea na kumzaba vibao kama hana gobore lake huko

Vipi watawala wa kiafrica wao je wanafanya nini? Kuuwa kwao ni jambo lakawaida tu.
 
Vipi watawala wa kiafrica wao je wanafanya nini? Kuuwa kwao ni jambo lakawaida tu.
Nimezungumzia watu wote pamoja na watwala bila kujali rangi, chama, taifa au kabila, tuheshimu utu wa wengine
 
Back
Top Bottom