Historia ya utumwa ifutwe msingi na sekondari

Historia ya utumwa ifutwe msingi na sekondari

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ukienda katika jamii zetu hata watoto wadogo ambao hawajui maisha yanaendaje wanaamini mzungu ni mtu bora kuliko mtu mweusi.

Nimejiuliza sana dhana hizi zinatokana na nini lakini nimekuja kubaini kuwa dhana hizi walitujengea wakoloni enzi za ukoloni.

waafrika walichukuliwa kama tabaka la chini kabisa katika jamii na waafrika wote walioshuhudia yaliyokuwa yakitendeka katika jamii waliamini hivyo kuwa mtu mweupe ni bora kuliko mweusi.

Sasa shida ikaja kwenye jamii zetu kutunga vitu vinaitwa historia na kuendeleza simulizi za yaliyotukia enzi hizo kwa watoto wadogo vizazi na vizazi. Watoto hawa mbali na kwamba hawakuwepo kushuhudia hayo, lakini hadithi za mababu zetu waliuzwa, waliteswa, walitumikishwa zinaishia kuwajengea picha za yaliyotukia enzi hizo na wao kuamini mtu mweupe ni bora kuliko mweusi.

ni sawa na baba aliyekuwa akipigwa na kuonewa na jirani yake na yeye kuwachukua watoto wadogo na kuwahadithia alivyokuwa akipigwa na jirani, hakika kwa akili za watoto za kupangana nani ana nguvu kuliko wote darasi na nani namba mbili, ukiwaambia nilikuwa nachapwa viboko na jirani basi wanamuona jirani kidume.

Historia ya kuwafundisha watoto ni ile inayowaonyesha jinsi babu zao walivyokuwa mashujaa ili kuwajengea kujiamini na wao kupambana.

watu wazima ndiyo pekee wasome historia zilizokuwa zikishusha utu wa watu wetu.

lengo ni kujenga jamii zetu zaidi badala ya kutumia madhira yaliyopita kuendelea kuharibu jamii zetu.
 
Historia ni muhimu hata kama ni mbaya
Kupitia historia tunajua tulipotoka,tulipo na tunapoenda
Historia ndio maisha
 
Historia ni muhimu hata kama ni mbaya
Kupitia historia tunajua tulipotoka,tulipo na tunapoenda
Historia ndio maisha
Hizi kanuni ndogo ndogo tusizotafakari na kuchukulia mambo very serious ki urahisi tu.

mimi nakuuliza hivi

kama zamani ulikuwa mtu dhaifu unapigwa, unaonewa na wale waliokuwa wakikuonea unaishi nao mtaani, Leo hii una watoto hivi ni umri wa watoto wako utawaweka chini na kuwaeleza ulivyokuwa dhaifu ukionewa.

Najua kuwa historia ni muhimu lakini mtu yeyote mwenye busara ataangalia hii historia inaenda kuwajenga hawa watoto au kuwabomoa. Kama utaona inaweza kuwabomoa basi utaiacha siri mpaka wajenge uelewa wa kutosha.

Lakini mjinga pekee ndiye anayeweza kukalisha watoto wake wadogo chini na kuwaeleza mimi mama yenu mnayeniona hapa zamani nilikuwaga kahaba. Je historia hii itawajenga?

Lakini watoto hawa wakishakuwa wakubwa na kuelewa maisha, wameshajua ugumu wa kuendesha familia ndipo anaweza kuwaambia mimi niliwalea kwa shida, baba yenu aliniacha sina kazi wala nini na nilizamika kufanya ukahaba ili kuwalea. Wakiwa wakubwa watakuelewa na kuona huruma kwa mama yao. Lakini kwa watoto wanachojua ni ukahaba ni mbaya.
 
Historia ni muhimu bila kujali ni mbaya au nzuri
Dunia imeimarika kutokana na historia
 
Ungeshauri wafute mambo yanayohusu wazungi ningekupa credit sana
 
Ungeshauri wafute mambo yanayohusu wazungi ningekupa credit sana
hoja hapa siyo kuacha mambo ya wazungu au kuyabeba.

Hoja ni mtu mweusi anawezaje kujiamini, akajiona na yeye yuko sawa na mtu mweupe angalau kifikra.

mbona huku kwetu hatuwaoni matajiri matajiri ni tofauti na masikini, lakini kwenye ngozi nyeusi na nyeupe kuna kitu kinaendeleza dhana ya mtu mweusi ni duni na mweupe ni bora na moja wapo ni hadithi zinazoonyesha uzalilishaji aliofanyiwa mtu mweusi na mtu mweupe.

Hatuachi haya kwa faida ya wazungu bali kwa faida ya watoto wetu
 
Hii hoja ina mashiko sana naona iwepo historia ya maendeleo ya mtu mweusi tu

Historia ya Ukoloni na ukandamizaji iwe additional mtu aitafute mwenyewe kama yalivyo maarifa mengine
 
Kwa hiyo unaposema tuwafundishe kuhusu mashujaa wetu na sio wazungu,

Kwa mfano Mkwawa utawafundisha alipigana vita na nani kama sio hao wazungu, na pia wazungu ndio walioshinda,
Wakamkata kichwa wakapeleka ulaya,
 
Nadhani hili likiboreshwa kuna namna inaweza fanyika
 
Hii hoja ina mashiko sana naona iwepo historia ya maendeleo ya mtu mweusi tu

Historia ya Ukoloni na ukandamizaji iwe additional mtu aitafute mwenyewe kama yalivyo maarifa mengine
Historia ya ukoloni na utumwa ifundishwe kwa watu wazima ambao wameshajitambua kwa wale watakaochagua kuendelea kusoma historia.

lakini huku chini tujenge akili za watoto wetu kwa kuwaonyesha "the good side of being black man", ya kwamba tunaweza kufanya mambo makubwa tukiamua
 
Back
Top Bottom