Historia ya Wachagga: Koo, Kabila na Falme-Mangi


Kwanza ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mr Mushi kwa kuwa kisababishi cha kuanza mada hii ambayo imeleta na mengi katika kujifunza juu ya historia ya uchagani. Kutokuridhika kwako hukukaa kimya na kunung'unikia vitandani kama watanzania wengi walivyo, bali uliamua kutoa dukuduku lako ili kupata taarifa sahihi. Mimi naona hiyo ni hatua ya kijasiri na ya kishujaa. Mpaka sasa mheshimiwa Mnyika hajajitokeza kujibu tuhuma hizo hivyo inathibitisha kwamba ni kweli alisema na inaonekana hakuwa na uhakika na anachoongea. Mnyika ni miongoni mwa watu wengi katika jamii yetu ambao bila ya kuwa na taarifa sahihi iliyofanyiwa utafiti makini huibuka na kutoa matamko kwenye halaiki na hata kujiabisha kwa kudhani watanzania wote ni mbumbumbu. Sifahamu kabila lake au fani yake hasa ni nini lakini inaonekana dai alilolitoa dhidi ya mangi Sina wa Kibosho limetokana na kudandia historia asiyoijua mapana yake. Ni vizuri watu wakajifunza kuongea (hasa kwenye public) taarifa ambazo hata wakija kuulizwa baadaye watakuwa na uwezo wa kuzitetea kihoja na kuzithibitisha kitaalamu. Viongozi wa kwenye jamii ambao wanaongea tu chochote ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu.

Nikirudi kwenye mada, hasa dai alilolitoa mheshimiwa Mnyika ni kwamba uhasama uliokuwepo kati ya mangi Sina na mangi Rindi (Mandara) wa old Moshi ni wa kihistoria. Hapo nyuma, yaani 1890, mangi Rindi kwa kuona kwamba alishindwa kukabiliana na nguvu zilizokuwa zikiongezeka kila kukicha za mangi Sina kule uchagani, aliamua kutumia fursa yake ya ukaribu na wakoloni kule kwenye boma lake kuwachochea dhidi ya mangi Sina na kuwaahidi kuwapa msaada wa askari na njia za kuendea Kibosho kumshambulia mangi Sina. Mangi Rindi alikuwa ameona fadhaa kubwa ya kushindwa kumsaidia mangi Ngamini kule Machame dhidi ya mdogo wake Shangali ambaye alikuwa akisaidiwa na askari wa mangi Sina kumwezesha kutawala Machame. Huku akimchochea kapteni Johannes ambaye naye alishakuwa amekereheshwa na kitendo cha mangi Sina kuchochea vita kule Machame kumng'oa Ngamini, mangi Rindi alifanikiwa kumshawishi kapteni Johannes mwaka ule wa 1890 kwenda kushambulia ngome ya mangi Sina huku akimsaidia kwa kumpa askari kadhaa. Katika vita hiyo mangi Sina alishindwa vibaya na kulazimishwa kujisalimisha ambapo aliingia mkataba na wakoloni wa kijerumani kuwa mtiifu na kuiunga mkono serikali hiyo. Mangi Rindi aliitumia hiyo nafasi kumtia adabu adui wake na hata kumchochea kapteni Johannes kwamba mangi Sina ayasalimishe kwa mangi Rindi pia maeneo ya Uru na Kirua-Vunjo aliyokuwa ameyaweka chini ya himaya yake, sharti ambalo kwa kusaini mkataba wa kujisalimisha ilibidi akubaliane nalo. Mangi Sina aliamriwa pia amwachie mangi wa Uru ambaye alikuwa amemkamata na kumweka kifungoni. Ingawa mangi Rindi aliona faraja kwa kumtia adabu adui wake wa siku nyingi, tatizo ni kwamba alikuwa ameshaanza kuwa mgonjwa na mwaka huo wa 1890 inasimuliwa kuwa muda mwingi alikuwa yuko kitandani akiugua (inasemekana alikuwa amepooza kutoka kiunoni kuelekea chini miguuni). Mangi Rindi Mandara alifariki baadaye mwaka huo wa 1890 na mtoto wake Meli Mandara akatawala.

Kwa hiyo utaona sababu vita ilipokuja baadaye kati ya mangi Meli na wakoloni wa kijerumani kwa nini mangi Sina aliwasaidia wakoloni dhidi ya mangi Meli. Ni mambo ya uhasama na visasi, lakini pia kumbuka mkataba ambao alilazimishwa kuusaini hapo nyuma kama sharti lake la kujisalimisha. Ni hayo tu kwa leo.
 

Atakuja kujibu ngoja tusubiri.
 
Mangi Sina wa Kibosho (aliyeshika bunduki katikati ya maaskari wake). Picha ilipigwa mwaka 1894. Alifariki miaka 4 baadaye. Wageni waliomtembelea kwenye himaya yake walisimulia kama mtu aliyekuwa hodari na shujaa na alionekana mstaarabu na mpole (kama anavyoonekana kwenye picha) lakini alikuwa mtawala wa vita na asiye na huruma. Inasemekana mwaka 1890 aliposhindwa vita na wakoloni wa Kijerumani wakisaidiwa na Mangi Rindi wa Moshi, aliamuru wote wale ambao walisita kupigana vita au ambao hawakujulikana walipokuwepo wakati wenzao wanashinda usiku kucha kupambana kulinda ngome yake, wasakwe popote watakapopatikana na kuuawa.

Ikumbukwe pia jina la Kibosho ni jina lililotokana na utawala wa Mangi Sina. Kabla ya Mangi Sina eneo la Magharibi kidogo na ilipokuwepo ngome yake liliitwa Lambongo likiwa chini ya utawala wa ukoo wa Kirenga. Sina alipotwaa madaraka miaka ya 1870 akisaidiwa na askari katili kutoka Machame, alijenga ngome yake katika eneo lililokuwa likikaliwa kwa asili na ukoo wa Kiwoso ambao walimkaribisha na kumuunga mkono. Utawala wa Mangi Sina unaweza kukumbukwa kwa mambo makubwa matatu kihistoria:

  1. Historia ya nchi inaweza kubadilika ikiwa atapatikana mtawala mwenye maono makubwa na nia ya mabadiliko. Utawala wa Mangi Sina unatufundisha kwamba inawezekana kubadili kabisa mwelekeo wa nchi kama atapatikana kiongozi asiyeenda kwa mazoea na aliye makini. Inasemekana kabla ya utawala wa Mangi Sina wakibosho wengi walikuwa na kawaida ya kwenda kutumika kwa kufanya kazi mbalimbali Machame na kushiriki katika kutunza na kulinda mifugo mingi ya Mangi wa Machame. Mangi Sina aliijenga Kibosho iliyokuja kuwa utawala wenye mafanikio na amani kubwa kuliko zote uchagani enzi zake. Inasemekana wakati wa utawala wa Mangi Sina wakibosho walimiliki mifugo na mashamba na kuwa na amani bila kubugudhiwa na tawala zingine. Badala ya hofu ya kushambuliwa Walikuwa ndiyo washambuliaji.
  2. Ni utawala wa Mangi Sina ndiyo umetupa jina la nchi iliyokuja kujulikana maarufu kama Kibosho.
  3. Sina alichukua nchi ikiwa koloni la Machame na utawala uliozoea hofu ya kuchukua maamuzi magumu. Ilimchukua muda mrefu kubadilisha mtazamo huu wa jamii na hata kuthubutu miaka ya 1889 kupeleka maaskari wake kuishambulia Machame, kitu ambacho kilionekana kama ndoto za mchana kwa Wakibosho wengi. Mangi Sina aliipa Kibosho uhuru wa kujitawala na kujitegemea kabisa. Aliwapa Wakibosho ujasiri wa kwamba inawezekana.
 

JM enzi.
 
Exactly upo sahihi kabisa mkuu!
 
Mangi Sina ni huyo aliochuchumaa upande wa kulia na sio huyo alioshika bunduki kama unavyodai wewe, alichukua madaraka kutoka kwa mama yake Mamka/Manka aliyekuwa Mangi wa kike hapo Kibosho pia hakuna ukoo unaitwa kibosho/kiwoso kama unavyonadi wewe,

Mangi alitokea ukoo mkubwa wa Mushi wenye linage ndefu ya kifalme kutokea Mangi Kimboka hivyo ukoo wake unajulikana kama Mushi ya Kimboka (Mushi Kimboka)

Watu wengi wamekuwa wakipotosha historia ya kweli kwa makusudi au kutokujua na hii huleta hisia tofauti kwa sababu wengi wanakuja na oral stories za sehemu wanazotokea ei Machame, Moshi, Marangu etc ambazo hazina back up yoyote na mara nyingi zinakuwa biased na upande mmoja

Historia inayotambulika dunia nzima kabla ya kuja kwa wazungu Kibosho ilitawala zaidi ya 50% ya wachagga wote, ukienda Machame, Rombo, Ugweno, Mamba, Siha etc utakutana na majina ya Mangi Malamya/Malamia ambao wote asili yao ni Kibosho na walipelekwa kusimamia interest ya Mangi wa kibosho

Mangi mwenye influence kubwa katika historia ya umangi mdogo wa kichaga Machame
(Sababu Machame haikuwai kujitawala kabla ya wazungu) ni Shangali ambae amakulia Kibosho na alisimikwa kuwa Mangi Machame baada ya mtangulizi Mangi Ngamini wa Machame kushindwa vita na kukimbilia Moshi kwa Mangi wa huko old Moshi Mandara

Kwa kumalizia Mnyika na jopo lake ni matapeli wa historia ya kweli kwa interest zao binafsi labda umaharufu kisiasa

-Mangi Sina alifariki mwaka 1897 (Cause of deal old age)

-Mangi Meli alifariki mwaka 1900 (Cause of death hanging)

Note, kosa alilonyongwa nalo Meli mtoto wa Mangi Mandara/Rindi ndio kosa hilohilo walimnyonganalo Molelia mtoto wa Sina muda huohuo siku hiyohiyo 1900

Hapa unaweza kuona hakukuwa na usaliti wowote ule aliofanya "The Great Mangi Sina" zaidi ya poroja za kutaka kumchafua huyu mtawala bora kabisa kuwahi kutokea katika historia

Mangi alifariki miaka mitatu kabla ya Meli kunyongwa, mtoto wa mangi Sina na Mangi mpya kibosho Moleia alinyongwa pia muda huo huo Meli akinyongwa, mastermind wa hii yote vitabu vinasema alikuwa ni Marealle yote kwa yote hauwezi kumuita Marealle msalita kwa sababu hakukuwa na common interest baina yao ila kila mmoja alikuwa anatafuta interest kuongeza umaarufu wake
 
Najua ni muda mrefu sana umepita tangu hii thread ianzishwe ila kwa kuwa sikuwahi kukutana nayo popote au kuiona ntajibu tu sababu hakuna namna nyingine,

Ss wenyewe hii stori kwetu ipo ila ni kwa version nyingine kwamba watoto wa kiume walikuwa wanatahiriwa pamoja kimakundi(Kibosho na Machame) na hivyo ilopofika zamu ya kwenda kutairiwa Machame basi huko wamachame wakawatairi watoto kwa hila kwa kukata dudu zao nusu/nzima kupekea watoto wote kutokea kibosho intake nzima kufariki, huku wenzao wakimachame wakifanikisha zoezi hill bila kupoteza watoto/vijana wao

Hii ilileta hasira sana Kibosho na wakaapa kulipiza kisasi kwa kuandaa karamu kwa wakijua Wamaachame wanapenda pombe na nyama basi wakaua na kwenda kupiga na huko Machame na kutawala kwa muda mrefu mpaka wakoloni walivyokuja

Lakini hizi zote ni stori tu ambazo hazina ukweli wowote ukweli ameandika Dundas tu katika kitabu chake

"Dundas ameandika kwamba tuliingia Machame na kuichapa fair and square, kwamba Machame ilikuwa ni tawala ndogo ya kimangi, kwamba Machame haikuwahi kuwa tishio kwa dollar nyingine za kichaga kabla ya wakoloni hasa waingereza na yote haya ni kweli sababu hakuna Mangi yoyote yule unaeweza kumtaja ambae alikuwa na umaarufu kuliko Sina na hii sio Machame tu bali uchagani kote

Mangi Sina aliingia Marangu na kuichapa fair and square, Sina aliingia Moshi na kuichapa ila alishindwa vunja boma la Mandara, hivyo hivyo Mandara alivyo ingia kibosho kwa usaidizi wa wajerumani na machief wote kasoro Machame ambayo ilikuwa chini ya Kibosho na kushindwa kuvunja ngome ya Mangi Sina kwa siku tatu wakiwa hawajafanikiwa kufuja ukuta wa boma hadi walipoamua kufikia makubaliano na mangi in only three conditions

1. Mangi Sina alitakuwa akubali kupeperusha bendera ya Ujerumani na sio ya sultan wa Zanzibar kama ilivyokuwa mwanzo

2. Mangi Sina alitakiwa kukubali na kuheshimu mamlaka ya tawala nyingine kama Mamba aliyokuwa akitawala hii iliamishiwa chini ya Mandara, pia alitakiwa kuacha Machame na Siha zijitawale na kuahidi kutovamia tena, pia kuheshimu title ya Mandara kama mangi mkuu

3. Alitakiwa kufungua ofisi ya akida "mswahili" atakae kuwa anareport taarifa zote za Kibosho kwa wajeruma HQ old Moshi

Mangi alikubaliana na conditions hizo zote na kuendelea na utawala wake kibosho na alikuja kurudishiwa Mamba kipindi cha Governor mpya Carl Peters baada Von Zelewsk kuondoka

Sababu wa kurudishiwa mamba ni kwamba baada ya Von Zelewisky (jina naweza kuwa nimekosea) rafiki wa Mandara kuondoka alikuja Governor Mpya Carl Peters alias mkono wa damu aliependelea zaidi Marangu na siasa za Marealle hivyo Mandara/Rindi kupoteza umaharufu wake

Historia ya Machame ilianza kushamiri baada ya vita ya kwanza ya dunia na mjerumani kumkabidhi Mwingereza uchagga, mwingereza alipendezwa zaidi na Machame sababu aliona wachaga wengine loyalty yao ipo kwa wajerumani ndio maana ali exile mamangi wengine wenye nguvu Mfano Ngilisho, Malamya kaka yake shangali pia na kuwapeleka Kismayo Somali huko ili kudhohofisha wenye nguvu na kutawala kirahisi

Von Zelewsk alishangazwa na boma la Mangi Sina "Mangi Sina Fortress" na kusema wazi Africa nzima hajaona finest defensive system kama hiyo ya boma la mangi ikumbukwe tu Von sio jina ni tittle anayotoa mfalme Kaiser mwenyewe kwa askari wenye weleti wa hali ya juu mno
 
Ndugu zanguni,
Nimevutiwa sana na huu uzi na sababu yake ni kuwa nimeandika kitabu ambacho utafiti wake ulinifikisha Machame na Old Moshi.

Halikadhalika utafiti huu ulinifungulia nyaraka zilizokuwako Machame zilizohifadhiwa kwa miaka 100.
Kama hili halitoshi nilihadithiwa historia iliyohifadhiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa takriban miaka 200.

Nataka nikuwekeeni hapa kipande kidogo katika yale niliyojifunza katika historia hii:

''Historia ya Wachagga imeandikwa kwenye upeo wa hali ya juu na Wazungu kiasi cha kumstaajabisha msomaji.

Inawezekanaje kwa Mzungu kutoka Ulaya mtu mgeni kuijua historia kwa undani wa kiasi kuweza kueleza mambo yaliyotokea miaka mingi sana iliyopita.

Mwandishi Mwingereza Charles Dundas ameandika historia ya Wachagga kwa kiwango cha kustaajabisha. Charles ameelezea mengi ambayo mtu hupata tabu hata kuyafikiri achilia mbale kuyajua hadi awe ameyasoma.

Wachagga wana hulka pale wanapompenda mgeni basi watampa lakabu inayoendana na heshima ya kabila lao.
Charles Dundas walimwita, Wasaoye-o-Wachagga, yaani Mzee wa Kichagga.

Historia ya Muro Mboyo aliyeishi Machame katika miaka ya katikati ya karne ya 19 imeishi katika simulizi za ukoo wake unaofahamika kama ukoo wa Nkya, ikipokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kwa miaka inayofikia 200 kama ilivyoelezwa.

Historia hii haikupata kuandikwa popote kwa nia ya kuwa historia hiyo inaandikwa ili ije kusomwa.

Hata hivyo mtoto wake, Kirama Mboyo ameacha utajiri mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa hati ya mkono na nyingine zimepigwa chapa zinozoeleza historia ya babu zake waliomtangulia kiasi cha miaka 100 nyuma na kueleza pia historia yake mwenyewe pale ilipoingia karne ya 20.

Baadhi ya nyaraka hizi ziko katika mfano wa barua, taarifa na maelezo ya kawaida zina tarehe na zipo nyingine hazina tarehe wala jina la mwandishi.

Muhimu ni kuwa kumbukumbu hizi zinaeleza historia muhimu sana ya takriban miaka 200 nyuma ya Wachagga wa Machame na sehemu nyingine za jirani ambao walikuja kuwa Waislamu wa kwanza.

Hizi nyaraka kwa zile ambazo zina tarehe zinarudi nyuma miaka 100.

Kuanzia mwishoni mwa karne ya 19, kufuatia mgogoro wa Muro Mboyo na Mangi Ndeseruo Mamkinga (aliyetawala kuanzia 1855 – 1880), hadi kuingia karne ya 20, hali ya uchaggani haikuwa shwari.

Hali ya utulivu ilipatikana baada ya kuingia kwa Wamishionari kuanzia karne ya ishirini.

Wamishionari wa kwanza kuwasili walikuwa kutoka Ujerumani, Leipzig Mission na Uchagga nzima iliingia katika utulivu.

Utulivu ulizidi kushamiri hasa walipofika Waingereza baada ya Vita Kuu ya Kwanza (1914 – 1918).

Wakati wa utawala wa Wajerumani, Uchagga uliingia katika madhila makubwa na misiba mizito kwa watawala wao (waliokuwa wakijulikana kama Mangi) kukamatwa na kunyongwa kwa kuupinga ukoloni wa Wajerumani.

Tunaweza kuanzia hapa kurudi nyuma tukizipitia nyaraka hizi ili kupata historia ya Uchaggani kwa jumla ilikuwaje kabla ya kufika wakoloni Wajerumani ambao walitanguliwa na Wamishionari waliojiita pia ni wavumbuzi.''

Katika utafiti wangu mtawala wa kwanza kusoma historia yake ni Mangi Shangali Ndeseruo na nimesoma habari zake kutoka Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama ambae hapo juu kabla ya kuingia Uislam alijulikana kwa jina la Muro Mboyo.


Mangi Shangali Ndeseruo

 
Hii ni historia kubwa sana Mzee Said inastahili uitengenezee kabisa uzi wake rasmi ili ipate michango tofauti tofauti

Vitabu vingi nilivyopitia vinaelezea kulikuwa na uhusiano mkubwa baina ya Sultan wa Zanzibar na Kilimanjaro ila havikuandika kama kulikuwa na uhusiano wakidini zaidi ya biashara, ingependeza uanzishe uzi rasmi kwa ajili ya Uislam Machame na Kilimanjaro yote
 
Kuna kitabu pia niliwahi kukutana nacho kilimtambulisha Mangi Sina kama Sultan wa Kibosho, nikikipata nakiunganisha hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…