Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Kwa waliowengi wanalijua hili neno la “Buffalo Solders” kutokana na Wimbo wa Bob Marley. Ukweli ni kwamba neno hili lina historia kubwa sana katka kuelezea histori ya Waafrika- Waamerika. kwa ufupi ni kwamba kwenye miaka ya 1866 kuliundwa kikosi cha wanajeshi ambacho kilihusisha Waafrika- Waamerika. Na kila kikosi kilikuwa na wanajeshi wasiopungua 1000.
Lengo la kuundwa vikosi hivyo ni kuimarisha amani na ulizi mara baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viilvyotokea kwenye miaka ya 1864-1865.
Waafrika- Waamerika wengi walijiunga japo mshahara ulikuwa mdogo kwani walikuwa wakilipwa dora13 kwa mwezi. Wengi walipenda kujiunga angalau wapate unafuu wa maisha nchini humo. Jina la “Buffalo Solders” lilitokana na wananchi ambao waliona namna ambavyo wanajeshi hao walivyokuwa wakipambana kama vile “nyati” anavyopambana.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa wanajeshi hao kuitwa “Buffalo Solders” au Wanajeshi Nyati. Na zaidi ya hapo, wanajeshi hao walikuwa na mtindo wa nywele nyeusi ambao ulifananshwa kama nyati. Katika mapambano asilimia kubwa ya wanajeshi walitumia farasi.
Jeshi hilo kwa kipndi chote hiko kilisaidia katika mambo mengi kama, vita vya Marekani na Ispania kwenye miaka ya 1890, vita vya Marekani na Ufilipino kweney miaka ya 1899.
Lengo la Hayati Bob marley kuimba wimbo huu ni kukumbusha nafasi ya mtu mweusi katika harakati za kuendeleza nchi ya Amerika.
Ni mimi MJUKUU WA CHIFU a.k.a kiboko ya bwanaake Nifah The bold
Sent using Jamii Forums mobile app