Historia ya Wilaya ya Ngara, utamaduni wa wakazi wa Ngara na chanzo cha jina la kabila la Wahangaza

Safi sana na nsoro ni moja ya ukoo wetu
 
all in all ngara ilitakiwa kuwa burundi au rwanda hata waangaza hawafananii na watanzania
 
all in all ngara ilitakiwa kuwa burundi au rwanda hata waangaza hawafananii na watanzania
Umeongea pumba ndugu yangu hivi hujui hii mipaka iliwekwa na wakoloni?? Vipi kuhusu wamasai, wajaluo,wanyasa, na makabila yote ya mipakani?? Rwanda, Burundi na Tanganyika kumbuka zilikua nchi moja enzi ya mjerumani.
 
Umeongea pumba ndugu yangu hivi hujui hii mipaka iliwekwa na wakoloni?? Vipi kuhusu wamasai, wajaluo,wanyasa, na makabila yote ya mipakani?? Rwanda, Burundi na Tanganyika kumbuka zilikua nchi moja enzi ya mjerumani.
rwanda na burundi hazikuwa chini ya mjermani bali mbelgiji na mfaransa kwa nyakati tofauti,nimekaa ngara nimesomea rulenge secondary najua ninachomaanisha
 
Asante mkuu. Ndio kabila langu ila nilikua sijui mambo mengi kiasi hichi,

Haya ndio matatizo ya kuzaliwa town na kukulia town.

Big up kwa uzi huu
 
Naomba kuuliza hivi kuna tofauti gani kati ya Wahangaza na Washubi? Kwangu huwa nawaona ni wale wale ila koo mbili tofauti. Meaning Bushubi(Washubi) na Bugufi (Wahangaza) lugha waitumiayo ni moja waishivyo nasikia ni sawa sawa. Naomba details za haya makabila...
 
rwanda na burundi hazikuwa chini ya mjermani bali mbelgiji na mfaransa kwa nyakati tofauti,nimekaa ngara nimesomea rulenge secondary najua ninachomaanisha

Kabla ya vita ya kuu ya kwanza Rwanda, Burundi na Tanganyika zilikuwa chini ya himaya ya German East Africa..... Kukaa/kuishi Ngara haimaanishi unajua au kusikia kila kitu juu ya Ngara.
 
Unaposema Mha, mhangaza, mshubi, mrundi na mnyarwanda kwamba lugha zao ni moja sio sahihi, isipokuwa lugha zao zinamwingiliano wa baadhi ya maneno na lafudhi ni tofauti.

Kwa mtu aliekulia Ngara kabla ya vita vya Burundi na vile vya Rwanda mwaka 1994, kilugha atakachoongea kwa baadhi ya maneno ni tofauti na kilugha kinachoongelewa na watu waliozaliwa wakati na baada ya vita hivyo.

Wakati wa vita wakimbizi kutoka rwanda na burundi wengi wao waliishi ndani ya jamii ya wahangaza, walioa na kuolewa na wahangaza, hapo ndipo lugha ya kihangaza ilianza kuingiza misamiati mipya kutoka rwanda na burundi ili wanapoongea waelewane. Lakni lugha hiyo ina lafudhi ya kipekee ukilinganisha na waha, washubi, wanyarwanda na warundi.

Naomba pia ieleweke kuwa mto ruvubu na mto kagera, imeungana mita chache kutoka kwenye daraja la kuingilia rwanda, kwa pamoja husukuma maji hadi kwenye maporomoko.
 

Lugha ya Wahangaza/Washubi na Warundi na Wanyarwanda ni ile ile. Yes, lafudhi inaweza kutofautiana kama vile Kiswahili kilivyo Bara na Visiwani. Tofauti ya misamiati inatokana na mazingira na experience watu wanayokulia hii ni katika lugha yoyote ile duniani. Mfano ukiangalia hata English ina misamiati tofauti kati ya England, New Zealand, Australia, South Africa, Marekani,Hong Kong, India etc. na sio kwamba lugha ni tofauti.
 
Nimeipenda sana hii,lakini hawa wahangaza si ndo wale wanyamulenge?
 
rwanda na burundi hazikuwa chini ya mjermani bali mbelgiji na mfaransa kwa nyakati tofauti,nimekaa ngara nimesomea rulenge secondary najua ninachomaanisha
Rudi kasome tena historia dogo, Rwanda, burundi na tanganyika ilikua nchi moja ikiitwa German Ostafrica...hao wabelgiji na wafaransa wamekuja kupewa tu baada ya mjerumani kushindwa ww1..Na waingereza wakapewa Tanganyika.
 
Nimeipenda sana hii,lakini hawa wahangaza si ndo wale wanyamulenge?
Vipi kuna UHUSIANO GANI kati ya Watutsi na Wahutu? Haya ni makabila? (Twayasikia Rwanda na Burundi). Je, na Ngara YAPO?
 
Rulenge ni tarafa iliyoko Ngara.
aisee nilikuwa Rulenge one time,aiseee ni bonge ya sehemu,barabara zinapitika mwaka mzima,hali ya hewa nzuri,maji ,umeme fresh,watu wakalimu yaani ni sehemu moja poa sana(wakati mwingine kuliko miji mikubwa Bongo),nilipapenda sana hapo,nilikuwa RHEC schools
 
Kuna baridi huko sio mchezo....I hope Kabanga Nickel project will one day take off
 
Naombeni kujua ni kambi gani ya wakimbizi ambayo bado ipo active Ngara. Naona google hawana hizo taarifa
 
Mwaka 2012 nilienda Ngara ...aisee kuna watumishi wa Halmashauri wanaongea Kiswahili kwa shida sana! πŸ˜‹ πŸ˜‹ πŸ˜‹
Hicho ndicho ulichokiona kutoka kwetu? Ulishawahi kufika Unyakyusani au Usukumani uwasikie ndugu zetu wa kule wanavyootaabika kuongea lugha yetu. Watu kibao wanaongea Kiswahili swafi Ngara, itakuwa ulikutana na mtu mmoja au wawili now una-generalize...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…