Historia ya zao la muhogo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mihogo ni moja ya mazao makuu ya chakula katika nchi za ki tropic. Mihogo iligundulika kama mizizi inayofaa kwa chakula 900 BC huko Brazili na Bolivia. Wareno walitawala Brazil kwanza kabla ya kugundua Afrika. Enzi hizo katika usafiri wa meli walichukua wa Brazil wenye ujuzi ili kuwasaidia katika kazi za utawala Afrika. Wabrazili hawa walisafiri na mbegu zao za mihogo kuileta Afrika miaka ya 1850.

Mtwara na mikoa ya kusini mpaka Pwani mihogo inalimwa sana. Mtwara inapakana na Msumbiji, Msumbiji lilikua koloni la Wareno. Mihogo ni chakula chenye wanga kwa wingi. Wanga ni muhimu kwa mahitaji ya kila siku ya mwanadamu.

Wahenga wetu walijifunza kuihifadhi mihogo ili iwasaidie katika siku za njaa. Walimenya mihogo na kuianika . Mihogo iliyokauka huitwa makopa. Makopa yakitwangwa hutoa unga wa ugali., Makopa pia hupikwa na nazi kama kufungua kunywa.


Mihogo ni moja ya vyakula vikuu Brazil na hivi ndivyo wanavyoandaa.
 
Utamsikia mbongo " hivi ndiyo vyakula vyetu vya asili waafrika" nawaangalia halafu nasema hiii! Mahindi asili yake bara Amerika, viazi utamu Amerika, viazi ulaya, ulaya, mchele Asia japo kulikuwa na mchele pori west afrika. Migomba ni South east Asia kama sikosei miwa nayo hukohuko. Ngano mashariki ya kati. Matunda ya kizungu na mboga kama chinese ndiyo usiseme.

Vyakula vyetu vya asili nafikiri ni ulezi, mtama na magimbi. Ulezi ni bonge la nafaka. Ulezi una madini chuma mengi sana. Ni moja kati ya nafaka zenye nguvu. Tumeiacha na kukimbilia ugali.
 
Kwahiyo hizo chapati ndio zimepikwa kwa kutumia unga wa mihogo au mimi ndio sijaelewa?
 
huku kwetu ugali unaopikwa kwa unga wa muhogo tunauita bada upate na mchuzi wa chukuchuku wa kuku wa kienyeji sjawahi kuweza kula huo ugali ni mweusi unanatia mikononi.
 
huku kwetu ugali unaopikwa kwa unga wa muhogo tunauita bada upate na mchuzi wa chukuchuku wa kuku wa kienyeji sjawahi kuweza kula huo ugali ni mweusi unanatia mikononi.
Kuna muhogo mweupe. Ugali unatoka wa brown hivi. Ukipata na mchuzi wa nyama unatembea sana.
 
Nimecheka sana japo umeongea ukweli sisi vyakula vyetu vya asili nadhani ni mizizi,asali na matunda pori kama mabungo
 
mimi napenda bada la kuchanganyia yan unga wa sembe na huo wa muhogo kidogo upate na bamia la kukoroga na vijisamaki vya leo leo ntakula mpaka mkimbie lakini upikwe huo wa mhogo peke siuwez
Lile la mhogo pekee lipikwe na kuku mtetea achemshwe kwenye chungu na chumvi, mbirimbi na ka pilipili kichaa kamoja. Ninakumbuka tulikua tukienda kwa bibi kuku hapakuliwi mnakula kwenye chungu na bada linapakuliwa juu ya majani ya mgomba kwenye ungo. Ndiyo chakula cha wageni.
 
huku kwetu ugali unaopikwa kwa unga wa muhogo tunauita bada upate na mchuzi wa chukuchuku wa kuku wa kienyeji sjawahi kuweza kula huo ugali ni mweusi unanatia mikononi.
Mhogo ni mweusi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…