Historia za Kusisimua Lakini Hazifahamiki

Historia za Kusisimua Lakini Hazifahamiki

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
si you was kidding sema ndo limemfika...😂
Kenny,
Ahsante sana kaka.
Ngoja nimweleze Earle Seaton inaelekea kuna watu ndiyo leo wanalisikia jina hili katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Earle Seaton mtu muhimu sana.

1950 Abdul Sykes alimtia Seaton kwenye TAA Political Subcommittee akiwa mshauri katika suala la Tanganyika na Udhamini wa Uingereza kama League of Nations ilivyopitisha baada ya Ujerumani kushindwa WW1.

Seaton aliisaidia TAA HQ kuandika Mapendekezo ya Katiba kwa Gavana Edward Francis Twining.

Hiki ni kisa kirefu hapa padogo.

Haya mapendekezo ni sehemu ya hotuba ya Julius Nyerere UNO 1955 na halikadhalika yalijadiliwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954.

Seaton ndiye aliyeandaa madai ya ardhi ya Wameru kupitia Meru Citizens Union kwenda UNO na aliongozana na Japhet Kirilo New York kama mkalimani mwaka wa 1952.

Seaton ndiye aliyeishauri TAA ifungue mawasiliano ya moja kwa moja na UNO kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Katiba ya TANU ilinakiliwa kutoka katiba ya Convention People's Party ya Kwame Nkrumah wa Ghana.

Ushauri wa Seaton na sababu ni kuwa ikiwa Waingereza wameikubali katiba ya CPP wasingeweza kuikataa ya TANU ambayo imefanana na ya CPP.
 
Back
Top Bottom