Historia za wachezaji: Mjue Ronald Koeman

mtalimaK

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Posts
245
Reaction score
232
JE UNAMJUA RONALD KOEMAN.

[emoji117][emoji117]Ronald Koeman ni mzaliwa wa mji wa Zaandam nchini Netherlands alizaliwa Tarehe 21 match 1963. Akiwa moja ya watu waluozaliwa na kipaji chake Mguuni ronald Koeman alikuwa beki mahali wa kati au kiungo mkabaji.

MAISHA YAKE YA SOKA
[emoji117][emoji117]Ronald Koeman alianza safari yake ya maisha ya soka katika club ya Groningen mwaka mwaka 1980. Akiwa Club ya Groningen Koeman ALicheza michezo 90 huku akifunga goli 33kuanzia mwaka 1980-1983 .

[emoji117][emoji117]Baada ya kuondoka Groningen Koeman alihamia Club ya Ajax ambapo ALicheza michezo 94 na kufunga magoli 23 kuanzia mwaka 1983-1986. Akiwa Ajax Koeman alipata mafanikio makubwa baada ya kushinda kombe ligi ambalo lilijukana kwa Jina la Eredevesie.

[emoji117][emoji117]mwaka 1986 ronald Koeman alihamia Club ya psv ambayo ni mahasimu wakubwa wa Ajax. Akiwa psv Koeman ALicheza michezo 98 na kufunga magoli 51 ambapo alifanikiwa kushinda makombe matatu ya ligi mfululizo kuanzia mwaka 1986 - 1989.

[emoji117][emoji117]safari ya Ronaldo Koeman uliendelea ambapo mwaka 1989 alijiunga na klabu ya Barcelona chininya Kocha Johan cryuff na kuunda kikosi hatari kilichoitwa the dream team kuanzia mwaka 1989-1995.

[emoji117][emoji117]akiwa Barcelona Koeman alifanikiwa kucheza michezo 192 na kufunga magoli 67 ikiwa ni pamoja na kushinda kombe la Spain alimaarufu kama la liga Mara nne mfululizo kuanzia mwaka 1991-1994, pia kwa Mara kwake na club ya Barcelona ilishinda kombe la uefa champion League mwaka 1992 dhidi ya Sampdoria huku bao pekee likifungwa na Koeman kwenye uwanja wa wembley.

[emoji117][emoji117]baada ya kuondoka Barcelona ronald Koeman alirejea nchini kwake na kujiunga na club ya feyenoord ambapo aliitumikia kuanzia mwaka 1995-1997 akicheza michezo 61 na kufunga magoli 19

[emoji117][emoji117]katika ngapi ya timu ya taifa ronald Koeman alianza kuitumikia timu hiyo kuanzia mwaka1982-1997 akicheza michezo 78 na kufunga magoli 14.akiwa na timu ya taifa ya Netherlands, Koeman alikuwa moja kati mastaa wa timu hiyo iliyowajumuisha wachezaji nyota kibao wakiwemo Marco van busten, Ruud Gullit, Frank Rijkaard na denis Bergkamp. Kikosi hiki atari kijiti shares Sana miaka 1988, 1990 & 1994.

SIFA ZA RONALD KOEMAN
[emoji117][emoji117]Ronald Koeman alikuwa na sifa kibao zilizo mfanya aonekani mchezaji bora kwa muda wake wote wa soka chache kati ya sifa hizo ni :-
[emoji117]a) Koeman alikuwa ni mfungajiwa penalty mzuri Sana.
[emoji117]b) Koeman alikuwa ni fundi wa kufunga magoli ya free kick
[emoji117]c) Koeman alikuwa ni bingwa wa kufunga magoli ya umbali mrefu kutokana na uwezo wake wa kupiga Mashuti makali golini.
[emoji117]d) ronald Koeman alikuwa fundi wa kupiga pasi kwa umbali mrefu na mfupi pamoja na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.

MICHEZO YAKE YOTE
[emoji117][emoji117]Katika maisha yake ya soka ronald Koeman ALicheza michezo michezo 690 na kufunga magoli 239, pamoja na kushinda mataji 20. hapa nadiliki kusema kuwa Huyu Jamaa alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli.

MAISHA YA UKOCHA
[emoji117][emoji117]Baada ya kutundika daluga Koeman alianza maisha mapya ya soka akiwa kama kocha. Katika maisha yake ya soka Koeman amefundisha vilabu vingi Sana hadi Sana na kushinda mataji kadhaa.
[emoji117]a)akiwa kocha wa Ajax alifanikiwa kushinda mataji matatu ya ligi mwaka 2001, 2002 & 2004.
[emoji117]b) baada ya kuachana na Ajax Koeman alihamia PSV na kushinda mataji mawili ya ligi mwaka 2006&2007.
[emoji117]c) Baadae alivifundisha vilabu vya benifica ya ureno, Valencia ya hispania, Southampton ya nchini England na sasa ni kocha wa Everton ya nchini England pia.

TUZO BINAFSI ALIZOSHINDA
[emoji117][emoji117]Katika maisha yake ya soka, Koeman amefanikiwa kunyakuwa tuzo nyingi Sana baadhi ya tuzo hizo
[emoji117]a) mchezaji bora wa Netherlands kwa miaka miwili mfululizo 1987&1988.
[emoji117]b) Koeman alifanikiwa kuingia kwenye kikosi cha uefa mwaka 1988
[emoji117]c) Koeman aliwai kuwa mfungaji bora kwenye michuano ya uefa champion League kwa msimu wa mwaka 1993-1994.
[emoji117]akiwa benifica mwaka 2011-12 alishinda tuzo ya Renus michels
[emoji117]pia akiwa akiwa nchini England amefanikiwa kuchukua ya kocha bora wa Mwezi September 2014, January 2015, na January 2016.

RECORD ZAKE AMBAZO HAZIJAVUNJWA
[emoji117][emoji117]Katika safari yake ya soka akiwa kama mchezaji ronald Koeman amefanikiwa kuvunja na kuweka record kadhaa. Chache kati ya record zake ambazo mkapa sasa bado zinaisha ni :-

[emoji117]a) ronald Koeman ndie mchezaji wa Barcelona anaeongoza kwa kufunga magoli mengi ya free kicks la liga akiwa amefunga magoli 25 akifutiwa na Leonel messi mwenye magoli 21 na Ronaldinho Gaucho mwenye magoli 20. Moja kati ya record zilimshinda Leonel messi kuvunja katika Club ya barcelona ni hii ya Huyu mwanaume wa shoka Koeman.

[emoji117]b) ronald Koeman anashikilia record ya kuwa beki aliefunga magoli mengi Zaidi katika historia ya mpira wa miguu akiwa amefunga magoli 239 katika mashindano yote.

HUYO NDIE RONALD KOEMAN KOCHA WA SASA WA EVERTON. [emoji122][emoji122][emoji122]

[emoji117]JE, unapenda makala zangu?
[emoji117]Tukane kwa makala zingine tena
[emoji117]Pia unaweza kunifuata inbox ili kunipa ushauri au kwa chochote unachopenda nikiseme juu ya soka
[emoji117]Mawasiliano zaidi email: mtalimakohi11@gmail.com.

KOHI[emoji118][emoji118][emoji118]
 
Mkuu leta na historia ya fundi wa soka duniani na Argentina Mzee Diego amando maradona/ mchawi wa soka enzi zake__ tuone vitu hatari akivifanya uwanjani.ambavyo havijafanywa na player yoyote isipokuwa leo messi pekee.
 
Mkuu leta na historia ya fundi wa soka duniani na Argentina Mzee Diego amando maradona/ mchawi wa soka enzi zake__ tuone vitu hatari akivifanya uwanjani.ambavyo havijafanywa na player yoyote isipokuwa leo messi pekee.
Saiz naandaa ya Ricardo Kaka baada ya hapo nitaileta ya Diego Maradona
 
hyo ya record ya magoli mengi ya freekick messi alishaivunja mwezi wa kwanza vs Villareal mwaka huu
 
hyo ya record ya magoli mengi ya freekick messi alishaivunja mwezi wa kwanza vs Villareal mwaka huu
Hii post niliandika kabla Messi hajavunja ilkuwa Mwaka jana mwezi wa 12
 
Ningefurahi kama utaleta na hawa legends
[emoji117] Rudi Voller
[emoji117] Hugo Sanchez
[emoji117] Bum kun Cha
[emoji117] Marius Trèsor
Hawa ni wachezaji walio katika list ya Fifa Classic XI (game)
 
Ningefurahi kama utaleta na hawa legends
[emoji117] Rudi Voller
[emoji117] Hugo Sanchez
[emoji117] Bum kun Cha
[emoji117] Marius Trèsor
Hawa ni wachezaji walio katika list ya Fifa Classic XI (game)
Usjal bro nitaleta just matter of time
 
Ushauri kila mchezaji anapohamia club nyingne tupia na picha take tuone jez ilimkaaje huko.
 
Huwa namfananisha sana Koeman na Denis Irwin full back wa zamani wa Man Utd.

Nae alikuwa fundi wa mipira iliyokufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…