Yaani nimemshangaa yule sijui ndiye Mwenyekiti wa kamati ya bunge anavyojikanyagakanyaga kuhusu neno 'dhaifu'.
Nchi hii tuna viongozi ambao ni hopeless kabisa! Yaani mtu anafura kwa sababu tu ya kuambiwa dhaifu?
Mimi nimefanya kazi kwenye taasisi za kimataifa. Kila tulipokuwa tunafanya development programs kwaajili ya wafanyakazi, Meneja alikuwa anaanza kwa kumwita mfanyakazi mmoja mmoja aeleze meneja ana weaknesses gani. Baada ya kuorodhesha weaknesses za meneja wako, kisha unamweleza strengths zake. Baadaye Meneja naye anakueleza weaknesses zako na strengths zako kwa kadiri ya mtazamo wake. Halafu anakuuliza na wewe mwenyewe unaona weaknesses zako ni zipi na strengths zako ni zipi.
Lakini hapa kwetu ni upuuzi mtupu! Ina maana wabunge wa CCM wanaamini Bunge halina weaknesses? Rais anaamini hana weaknesses? Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, polisi, n.k. hawana weaknesses?
Mbona tunataka kuwa Taifa la hovyo kiasi hiki? Hata mitume wa Yesu waliwahi kutamka, 'tukisema hatuna dhambi tunajidanganya', hiyo ni sawa na kusema tukisema hatuna udhaifu au mapungufu, tunajidanganya.
Tatizo tuna wabunge na baadhi ya viongozi wasio na uelewa wowote juu ya uongozi. Watu waliopungukiwa uelewa na upeo.