Zakumi,
Nilitaka kuanzisha thread ya kuuliza Spirit ya Taifa la Tanzania. Labda Companero na Mkandarea watanisaidia.
Ukiwa hapa Marekani na kutokana na jinsi ya nchi ilivyoundwa, watu wanakuwa na confidence ya kufanya vitu hata ambavyo haviwezekani. Ukiwauliza, watasema hiyo ni spirit yao.
Kwa mfano: Bill Gates, vijana wa facebook, Napster etc, walipopata ideas za kutengeneza pesa, walikuwa tayari kuachia shule na ku-implement ideas zao. Ukiwauliza watakwambia hiyo ni spirit ya taifa lao.
Mkuu samahani sana nilikuwa sikuiona hii hapo mwanzo kumbe imekugusa kiasi hiki..
Well, nitakujibu kulingana na hoja zangu za awali..
Kwanza tuanze na Marekani wenyewe maanake sipendi tufananishe nchi hizi mbili kwa sababu hatulingani kabisa.. Ni sawa na kulinganisha Bacelona na Yanga, kwa sababu tu wote ni mabingwa wa nchi basi unashangaa kwa nini moja ina matokeo tofauti na nyingine.
Marekani hiyo spirit yao imetokana na kuwa na DIRA -
Declaration of Independence. Huu ndio mchoro wa ramani wa nchi waliyokusudia kuijenga na ndio uliozaa Constitution yao na hata American dream ambazo ni nguzo muhimu ktk ujenzi wa Taifa lao..
Kina Bill Gates, Napster na wengine wote ni matokeo ya watu walio pursue dream hizo na kwamba ipo sheria haki na wanajua safari yao inakwenda wapi..Kama dereva vile wa gari anavyoweza soma alama na kujua haki zake, sheria na safari yake kwa wakati mmoja..
Sisi on the other hand tunataka kujenga Taifa pasipo ramani, yaani tunafyatua matofali na kuweka nguzo ovyo ovyo wananchi wakibebeshwa zege hawafahamu kinachojengwa zaidi ya kufikiria TZ itakuwa kama Amerika!.
Nyerere alikuwa na fikra za jengo lake, Kaingia Mwinyi kabomoa nguzo kajenga zake, Mkapa naye kaingia na ufundi wake.. mwisho JK amejikuta ana nyumba nusu ambayo hajui ataanzia wapi.. Kusema kweli JK hajui aanzie wapi zaidi ya kuendelea kufyatua matofali kwa miaka yote minne kwani hana ramani ya nyumba..
Tatizo langu kwenu na ubishi wote huu ni pale nyie mnapotoa suggestion kwamba tujenge tu, kila mtu ashike kifaa anachoweza kukitumia tujenge nchi badala ya kusubiri ama kuitegemea serikali itufanyie kila kitu..Kweli wapo watu wanaosubiri ama kutegemea serikali iwafanyie kila kitu lakini pia ni ujinga kufikiria kwamba tunaweza jenga nyumba (nchi) pasipo kuwa na ramani..
Mfano mkubwa ni ujenzi wa nyumba nyingi nchini kujengwa ktk viwanja visivyopimwa..Matokeo yake ndiuo utata tulokuwa nao kila siku serikali inapotaka kujenga barabara au daraja inabidi watu wahamishwe na kulipwa fidia kwa sababu tu tumeanza na wananchi kufanya maamuzi yao kisha serikali inafuatia..matokeo yake barabara zinajenga si nzuri, pia bado hazitazami traffic for the next 20 yrs.. meaning miaka ijayo watabomoa tena nyumba nyinginezo kuongeza barabara..
Yote haya yanatokana na kutokuwa na mwongozo - Dira..wananchi wote hatufahamu tunajenga kitu gani zaidi ya kila mmoja wetu kufikiria ujenzi wa kibanda chake.
Mimi sii mpenzi wa Itikadi ambazo zinafuatwa kama msahafu..I believe in Idea kulingana na mazingira yetu yaani hakuna msahafu wa siasa ama itikadi unaoweza kulinbgana na maisha yetu.. Sii Ubepari au Ujamaa wa kuchongwa Ulaya..Lakini pamoja na yote haya huichukulia Siasa ama Uchumi kama imani ya dini. Sote tunataka kuokoka, tunataka mwisho wa maisha yetu kulazwe mahala pema peponi..Hata Pagan humwomba huyo Mungu Jua, Manson na Shetani wote wakiwa na imani kwamba maisha yao yote yanafuata barabara itakayowapeka ktk mafanikio..Na kwa kufuata Dira au (a Navigation system) inawasaidia kutopotea njia..
Tatizo la Tanzania leo hii mbali na kutokuwa na Dira tunaenda kwa baraka zake Mungu. Hivyo hata tukikimbia haiwezi kusaidia kitu kwani tunakwenda tusikojua, pengine mbio zetu zitatufikisha haraka Jahanam!