Hitimisho la uzi “wale ambao hawajawahi kuonana na member yoyote humu JF

Hitimisho la uzi “wale ambao hawajawahi kuonana na member yoyote humu JF

Swet-R

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
5,613
Reaction score
8,082
Katika uzi niliofungua wa wale ambao hawajawahi kuonana na member yoyote humu Jf ilikuwa kipimo cha namna gani upendo umepungua katika jamii ya kitanzania. Nimegundua hali ni hatari,watu tunaogopana sana.

Tunaogopana kwa mambo mengi,linaoongoza kutekwa,kutapeliwa n.k n.k. Inasikitisha kuona upendo umepungua kabisa katika jamii yetu. Sijui tunakwama wapi?. Tanzania ilikuwa ni nchi inayoongoza kwa watu wakarimu sana,ajabu sasa tukwenda kuwemo kwenye watu wanaoogopana.

Zamani ilikuwa ukikutana na mtu uliekuwa pamoja kipindi cha nyuma mnakumbatiana mnahag,mnafurahi,lakini siku hizi ukimuona kwa mbele unamkimbia. Humu tu watu wengi hawataki kuonana wakati hili group tu lilitosha kuwafanya watu humu wawe ndugu. Tufanyeje ili kurudisha ile hali ya zamani?.

Hata ukija kwangu nikukaribishe bila wasiwasi hata kama sikufahamu?. Hata ukiwa na milioni 100 zako ukaribishwe tu nyumbani kwa Mtanzania mwenzako bila wasiwasi,ingali anajua uko na milioni 100?.

Turudisheje hii?
 
Mda mwingine ni mitazamo ya watu na sbb zao binafsi ndugu, na inabidi tuu iheshimiwe........
Sidhani km nikosa...

Wengne hawataki kbsa kujulikana sio kwa ID sio physical..
Wengne furaha yao ni kua anonymous..
Wengne kuna vitu wanaficha...
Wengine umbali....
Wengine Usalamaa....
Wengine hali/ngazi za maisha yao...
Wengine tofauti ya maisha waliyojijengea humu na maisha halisi...
N.k n.k.....
 
reyzzap, Ooooh...! Ok. Sasa wengine utakuta walifahamiana tangu zamani,wakapotezana,baadae ktk pitapita mmoja kabahatika kumuona mwenzie. Anamkwepa
 
Ooooh...! Ok. Sasa wengine utakuta walifahamiana tangu zamani,wakapotezana,baadae ktk pitapita mmoja kabahatika kumuona mwenzie. Anamkwepa
hahaaaa kumbe unamaanisha hiiii....
Alooo mm ukinikwepa km ulikua ni best yangu na bd nahitaj tuwe karb nakuungiaaaa.....

Watu wapambane....
Hii mara nyingi ikitokea turnup....
Maisha yakikaa huwezi kukimbia zaidi ya kufurahia....
Sema mtu km huyo unamwacha,
pengne kukutana na wewe ukazidi kumuumizaa...
 
Sijausoma huo uzi ila kwa ulichokiandika hapa JF ibaki kuwa JF, tujuane kwa ID tu na ikitokea vinginevyo iwe kwa hiari ya wahusika.

Huku mtaani napo tumeaminiana na kuonyesha kiwango kikubwa cha upendo bado wachache wamethamini na kujali huo uungwana. Hivyo basi, wengi wameamua kuchagua aina ya maisha wanayoona haitawazonga sana.

Kwa upande wangu napenda sana nimuonyeshe mtu upendo, kumwamini na kumheshimu hata ikiwa nnaemtendwa hatojali..inanipa utulivu na amani kuwapenda wengine.
 
reyzzap, Ahahaaaaa.. ! Hapo kwenye kumuungia tu. Vipi umefikiwa na mgeni labda iwe unafahamiana nae au hufahamiani nae. Anaomba hifadhi kwa usiku huu,kuhofia usalama wake,ana mfuko wake una milioni 100,na wewe unajua una milioni 100,vipi huwezi kupata katamaa mkuu?.
 
The Monk, Safi sana. Umechanganua vizuri mkuu,hasa hapo JF ibaki ilivyo. Na kuhusu campany,napenda pia hiyo kitu. Asante mkuu
 
Ahahaaaaa.. ! Hapo kwenye kumuungia tu. Vipi umefikiwa na mgeni labda iwe unafahamiana nae au hufahamiani nae. Anaomba hifadhi kwa usiku huu,kuhofia usalama wake,ana mfuko wake una milioni 100,na wewe unajua una milioni 100,vipi huwezi kupata katamaa mkuu?.
aaaaah, tamaa tumeumbiwaa, tofauti ni viwango na maamuzi,
akitaka alipofikia pawe salama 100% anigee kdg, hata bank huwezi weka hela bure.....
Akikataaa namzushia kesi ya uhujumu uchumi...

Wewe nikusaidie ulale kwangu na 100mil uniachie harufu tuu?
Hapana....
Hapa ule msemo wa
'wema ukizidi ni dhambi' nitautumia kuepuka hii dhambi...
 
Kila mtu afanye mambo yake yanayomhusu yeye na familia yake.
Kukitokea haja ya kukutana tutakutana.
Sio kukutana kutana tu bila sababu, mambo ya kufanya yapo mengi, muda mchache.
 
reyzzap, Ahahaaaaaaa...! Umeua mzee baba. Basi sawa. Sasa vipi wewe umetingwa ni usiku,unataka ujisitili mahala una milioni 100. Kwa mbele kidogo kuna kituo cha polisi,na upande mwingine ni makazi ya raia. Vipi utachagua ukajihifadhi uraiani kwa watu au ukajihifadhi polisi mpaka asubuhi?,ila popote utakapojihifadhi wajue una 100 mzee
 
Kila mtu afanye mambo yake yanayomhusu yeye na familia yake.
Kukitokea haja ya kukutana tutakutana.
Sio kukutana kutana tu bila sababu, mambo ya kufanya yapo mengi, muda mchache.
Ni kweli mkuu
 
Back
Top Bottom