Swet-R
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 5,613
- 8,082
Katika uzi niliofungua wa wale ambao hawajawahi kuonana na member yoyote humu Jf ilikuwa kipimo cha namna gani upendo umepungua katika jamii ya kitanzania. Nimegundua hali ni hatari,watu tunaogopana sana.
Tunaogopana kwa mambo mengi,linaoongoza kutekwa,kutapeliwa n.k n.k. Inasikitisha kuona upendo umepungua kabisa katika jamii yetu. Sijui tunakwama wapi?. Tanzania ilikuwa ni nchi inayoongoza kwa watu wakarimu sana,ajabu sasa tukwenda kuwemo kwenye watu wanaoogopana.
Zamani ilikuwa ukikutana na mtu uliekuwa pamoja kipindi cha nyuma mnakumbatiana mnahag,mnafurahi,lakini siku hizi ukimuona kwa mbele unamkimbia. Humu tu watu wengi hawataki kuonana wakati hili group tu lilitosha kuwafanya watu humu wawe ndugu. Tufanyeje ili kurudisha ile hali ya zamani?.
Hata ukija kwangu nikukaribishe bila wasiwasi hata kama sikufahamu?. Hata ukiwa na milioni 100 zako ukaribishwe tu nyumbani kwa Mtanzania mwenzako bila wasiwasi,ingali anajua uko na milioni 100?.
Turudisheje hii?