"Hiv unajua Maharage ukiweka kitunguu saumu yanakua kama nyama"

Kwa chapati yanaenda vizuri.

Siku jaribu kuanza na swaumu na iliki pia.
Mkuu mimi nilikuwa napika wali mseto yaani nakaanga kitunguu swaumu na kitunguu maji afu naweka maharage na tupia mchele daah ilikuwa ni shida asubuhi nanunua maziwa napika chai nakula kiporo changu kinakuwa kitamu balaa nimeyamic maisha ya sanawari kwakweli
 
karibu tena aseeh...

hiki chakula sijawahi aseeh... itabidi siku mama klaree akisafiri nikijaribu kisirisiri.
 
Necessity is the mother of invention. Unakula maharage ya kitunguu swaumu yenye ladha kamaya nyama, huku unaepuka cholesterol ya nyama.
Hahahaha,sio kwamba vyuma mkuu
 
Hali ni ngumu, mchunga pia utakuwa mboga ya taifa wakati kwa wengi ni majani ya sungura.
Kwetu tunalima mchunga na sokon unauzwa kama mboga, upish wake ndo tatzo kuna hatua nyingi kama kutuma au kutoa hela tigo pesa au m pesa
 
Huwa nikipika mseto wa maharage familia haishibi Kwa utamu huo ni balaa watu wengi hawajui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…