Hivi akiwa Head of State ndio unakuwa Head of Government?

Hivi akiwa Head of State ndio unakuwa Head of Government?

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Niende tu moja kwa moja kwenye mada husika. Niko najiuliza, hivi siku hizi huko shule watoto wetu wanafundishwaje aisee. Nauliza hivi maana toka majuzi sielewi mwanangu kaona nini na wapi. Amekuwa ananiuliza na hii leo ni mara ya pili, "Baba, rais anaongoza na nchi? nikajibu ndio mwanangu!

Akauliza tena, rais anawaongoza na wabunge na mawaziri? Hapo nilisita kidogo, ikabidi nimtafakari kwanza huyu mtoto analenga nini. Lakini kiutani utani hivi ikabidi nimjibu ili aridhike, nikamwambia ndio.. anawaongoza! Japo hili jibu langu sikulitoa kwa kuelewa moja kwa moja kama nimekidhi haja yake.

Sasa wadau naoma mnisaidie ili nikasahihishe kama nilikosea. Hivi Tanzania ukiwa rais ndo unaongoza na serikali ama serikali inaongozwa na nani, ama serikali yenyewe ndo inajiendesha tu?
 
Kwa tanzania yes, ila sehemu kama israel, germany na uk! PM ndo head of govt, head wa state ni president (israel, germany) or king for uk
 
[emoji2][emoji2][emoji2]!
Kwa mujibu wa katiba ya JMT,raisi n both mkuu wa nchi na pia serikali.

Kuna mihimili 3 (arms of governments) yaani bunge,mahakama na serikali yenyewe,kwa dhana nzima ya utawala bora Kila muhimili unapaswa kujitegemea.

Asante umenikumbusha hii mada ipo kidato cha pili.

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom