Hivi anayewajibisha bodi ya ligi ikivunja kanuni ni nani?

Hivi anayewajibisha bodi ya ligi ikivunja kanuni ni nani?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Kama mchezo unaweza kuahirishwa bila sababu ya msingi, na TPLB wakaona ni sawa, ni hatari kwa ligi yetu

Kwahiyo timu isipokuwa tayari kucheza inajiamulia tuu kuahirisha mchezo kwa visingizo uchwara halafu Bodi itabariki kwa kusogeza tarehe ya mchezo mbele

Kuna mdau amesema Kanuni inasema "Timu isipofika uwanjani, basi timu pinzani itapatiwa alama 3 na magoli 3. Sasa kanuni hii ina maana gani kama kuna uwezekano wa kukaa na kuyamaliza na mchezo ukapangwa wakati mwingine, Kanuni hii ina maana gani?"

Kwa hili la Derby ya juzi Bodi ya Ligi imevunja kanuni

Swali muhimu ni NANI WA KUIWAJIBISHA? Maana huku ni kuharibu ligi, hamasa za watu zimekufa, watu waletoka mikoani kuja kuangalia ligi leo timu inaamua tuu kususa na Bodi inaona fresh tu? Hii sio sawa

Bodi bure kabisa hii
 
humu kwenye JF kuna andiko linadai bodi ya ligi ina wanachama wa yanga wawili walioahirisha debi
 
Back
Top Bottom