Unaweza kudhania hivi ni vipande vya filamu ila hizi ni picha za ukweli.
View attachment 3195547
View attachment 3195549
Huyo binti hapo juu, mwenye asili ya Kihabeshi anaripotiwa kutekwa na kuteswa. Watekaji wanahitaji dollar 6000 ili aachiwe huru. Yupo katika mateso tangu may 2024. Hao wengine nyuma yake ni wahanga wa utumwa
Hii ndio picha yake alivyokuwa uraiani.
View attachment 3195567
Kiini cha madhara yote haya ni kuwepo kwa Utawala wa Kidikteta, hang over ya Udikteta wa Muammar Ghadafi bado inaendelea kuitesa nchi ya Libya.
Watawala Madikteta wanapoondolewa madarakani ni lazima nchi husika itapitia katika wakati mgumu Sana wa kuwepo kwa Ombwe la Utawala, hiyo ni lazima, wala haiepukiki. This is according to the Law of Nature.
1.Jaribu kutafiti kuhusu maisha ya Wajerumani baada ya kuondolewa madarakani utawala dhalimu wa dikteta Adolf Hitler, nchi hiyo ya Ujerumani iligawanyika katika vipande viwili vya Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi.
2.Jaribu kutafiti kuhusu maisha ya watu wa Zaire baada ya kuondolewa madarakani utawala dhalimu wa dikteta Mobutu Sese Seko, nchi hiyo ya Zaire ilivurugika kabisa na kusababisha kuuawa kwa Rais aliyerithi madaraka Bw. Laurent Kabila.
3.Jaribu kutafiti kuhusu maisha ya watu wa Sudan baada ya kuondolewa madarakani utawala dhalimu wa dikteta Hassan El Bashir, nchi hiyo ya Sudan Sasa ipo vitani na ipo hatari kubwa sana kwamba inaweza kugawanyika zaidi na zaidi na kuzaliwa kwa nchi zingine mpya.
4.Jaribu kutafiti kuhusu maisha ya Wakenya baada ya kuondolewa madarakani utawala dhalimu wa dikteta Daniel arap Moi chini ya Chama chake cha KANU, nchi hiyo ya Kenya iligawanyika katika matabaka mengine mengi zaidi mbali na matabaka ya kimakabila yaliyopo, na hatimaye nchi hiyo ilitumbukia kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe na kupelekea vifo vya watu wengi Sana.
5.Jaribu kutafiti kuhusu maisha ya wananchi wa nchi hizi baada ya kuondolewa madarakani tawala za kidhalimu za kidikteta zilizopo kwenye nchi zao: nchi ya Liberia baada ya kuanguka kwa Utawala wa Kidikteta wa Samuel Doe, nchi ya Italia baada ya kuanguka kwa Utawala wa Kidikteta Benito Mussolini, nchi ya Afrika ya Kati baada ya kuanguka kwa Utawala wa Kidikteta wa Jean Bedel Bokassa, n.k, n.k,.
Mifano hai ipo mingi Sana hapa duniani.