Hivi Azam mnapohamisha kuonyesha mechi kwenda ZBC AU Azam Extra huwa mnamtaarifu nani ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huwa nashangaa sana ninapoona mechi imetangazwa kuonyeshwa labda Azam Sports 2 , halafu muda unafika haionekani au imehamishiwa channel nyingine bila taarifa , hivi mnadhani ni nani ataota kwamba game hii iko channel ya ZBC 2 wakati mlitangaza kuwa itakuwa Azam Sports 3 ?

Kwa mfano , walitangaza kwamba game ya league 1 kati ya Rennes na Aj Auxerre ingeonyeshwa Azam Sports 3 , muda ulipofika game yenyewe hakuna Japo tangazo bado lipo , kumbe wameihamishia Azam Xtra ! sasa tutajuaje ? na hii si mara moja , huu ndio mchezo wao , hii kitu haikubaliki .

Badilikeni haraka sana , Ni kweli kwamba Azam ni yenu lakini sisi tunalipa hela zetu , msituburuze na tuheshimiane
 
Aisee mkurugenzi, hiyo Azam Sports 3 imeanza lini kuonekana kwenye kisimbuzi cha Azam? Ninachofahamu,kuna Azam Sports One Hd, na Azam Sports two Hd! Then inafuatia Utv!!
Rudi kachungulie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…