Hivi bado Waafrika hatujaingizwa katika kundi la viumbe wenye uwezo wa kufikiri?

Hivi bado Waafrika hatujaingizwa katika kundi la viumbe wenye uwezo wa kufikiri?

JOKA55

Senior Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
110
Reaction score
74
Friedrich Hegel (August 27, 1770 – November 14, 1831) mwanafalisafa wa kijerumani alishawahi kuchambua uwezo wa binadamu duniani na katika uchambuzi wake sisi waafrika (kusini mwa jagwa la sahara) hakutuweka katika huo uchambuzi wake na alidai kama kuna uwezo wa kufikiri hata kidogo basi itakua maeneo ya afrika ya kaskazini (Kaskazini mwa jangwa la sahara)
Alisema mawazo yanaanzia Asia (Anti-thesis) Amerika (Thesis) Ulaya (Synthesis) akimaanisha ulaya ndo wakongwe wa kila kitu katika kufikiria. Wanaposhidwa Asia na Amerika ulaya ndo inakuja kutoa suluhisho kwa mambo magumu ya kidunia.

Mawazo haya aliyasambaza duniani kote na kwa kipindi kile dunia iliamini kabisa kuwa waafrika wako sawa na sokwe na kama wana uwezo wa kufikiri basi ni sokwe tu mwenye uwezo kidogo wa kufikiri dhidi ya sokwe wengine. Huyu bwana mawazo haya aliyajenga katika misingi ya wanafalisafa wengine magwiji kama kina Socrates, Plato, Aristotle na kwa kiasi kikubwa mjerumani mwenzake Immanuel Kant ambye anaheshimika sana kwa kazi zake kama Critique of Pure Reason, Critique of Practical Reason, Metaphysics of Morals, na Critique of Judgment. Kazi hizi zilisomwa sana na Hegel na zikachangia sana kwa yeye kufikia hitimisho kuwa watu weusi hawana uwezo wa kufikiri

Baada ya zaidi ya mika 100 ndo alitokea mmisionary kutoka Ubeligiji Placide Tempels aliyekua anafanya shughuli zake Congo Kinsahasa akakanusha kwa kuandika kitabu Bantu Philosophy na kuchambua kuwa waafika weusi ni watu na wana uwezo wa kufikiri. Lakini wazungu wakamuomba udhibitisho wa kimaandishi, bahati mbaya akashindwa kwani waafrika hawakua na utamatudi wa kuweka kumbukumbu katika maandishi. Kilichotokea ni kwamba kipindi hiki cha miaka zaidi ya 100 hakutokea mtu yeyote kukanusha hoja hiyo ya Hegel kwa hiyo ikaingia akililini mwa wazungu ambao mpaka leo kuitoa hiyo akilini mwao ni ngumu bado.

Japo baada ya hapo kuna waandishi wengi wa kiafka wamendika na kutetea na kuonesha uwezo wa mtu mweusi kufikiria. Mfano Odera Oruka kutoka Kenya katika kitabu chake cha Practical Philosophy anuelezea muafrika kama kiumbe maarufu kutunza vitu kichwani kwa hiyo hoja kuwa waafika hawafikiri kwa kuwa hakuna udhibitisho wa kimaandishi kwake ni upotoshaji mkubwa. Hii hoja yake kaiweka kama Sage Philosophy au hekima. waafika hasa wazee ni matajiri wa hekima na haliharibiki jambo kama wazee wapo.


Wapo wengine wengi waliotetea uwezo wa kufikiri wa mwafrika kama kina Alex Kagame, Kwame Nkuruma, J.K. Nyerere, Kwasi Wideru, Paulin Hountoundji, Nelson Mandela Leopord Sengo na kitabu chake maarifu Negritude na wengine wengi kwa uandishi wa vitabu mbalimbali.

Pamoja na juhudi zote hizo bado tuna matatizo makubwa ndani ya bara letu, hatuheshimiani, hatuna uzalendo, wazungu wanatengeneza silaha sisi ndo uwanja wa majaribio, madini yetu yanachukuliwa.

Niache huko nije hapa Bongo kwetu Tanzania, Hivi kweli watanzania tuna uwezo mzuri wa kifikiri? Mfano nchi imejaa mafisadi na sio kwamba hawafahamimiki lakini leo hii wapo mitaani eti wanatka kuwa wakuu wa nchi nasi tunawashabikia. Makosa tuliyoyafanya mwaka 2005 bado tunataka kuyarudia "KUWAPA WAFANYABIASHARA NCHI" hivi kweli hatuoni kosa tulilolifanya?

Kiukweli nchi hii kwa sasa inatakiwa kupewa mtu makini, mzalendo mwenye uchungu wa kweli na wananchi wanaohangaika kwa umaskini wakati nchi yao ni tajiri ajabu. Mfano mwingine, kama kweli tunafikiria kwa nini tunakubali Uraniam yetu inachimbwa na watu wanabeba na wanatuambia eti bado hawajaanza kulipa kodi kwa vile bado wako kwenye matazamio. Kwa nini tunaumiza viwanda vya sukari vya ndani kwa kuagiza sukari kutoka nje ili hali tukijua uwezo wa kuzalisha tunao na kwa kiasi cha kutosha?

Bahati mbya tena hata vyama vya upinzani kuna baadhi wantumiwa na watu wa nje kutuhadaa kwa maslahi yao, hivi kweli tunafikiri vizuri?

Naamini katika mtanzania bora awe chama tawala au upinzani

hayo na mengine mengi ndo yananirudisha nyuma na kuanza kufikiria hoja ya Hegel kuwa sisi waafrika bado hatuko ktk mzunguko wa binadamu wanaofikiri. Karibuni tujuzani kweli na idadi yetu ya karibu milioni 50 tunashindwa kupata mtanzania mwenye vigezo vya kweli tukampa nchi hii ninayoipend?
 
JOKA55, umejenga hoja ikajengeka. Hongera sana. Ila ndiyo hivyo tena haitasaidia, ukweli ndio huo kuwa hatufikirii. Inauma.

Haya mambo yanavyokwenda yanawezekana Afrika tu! Kwa maneno mengine hiyp dhana ya mzungu ndio uhalisia wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Bado sana mkuu, tena watanzania ndio tutakuwa wa mwisho kabisa kuingizwa, hata sokwe anaweza kutuzidi uwezo wa kufikiria, watafiti fanyeni kazi.
 
Back
Top Bottom