Hivi biashara ya mayai ya kware iliishia wapi jamani?

Hata kinguru wa zanZibar wakitangaza wanaongeza nguvi za kiume wataisha wote
 
isije wakaibua mkojo wa kuku au jasho la kunguru. nchi iliyolelewa kwa ushirikia ina mambo aisee.
Jasiri asahau Asili! Ushirikina ndio asili yetu mkuu. Mengine yote wametuletea wazungu!
 
Dawa ni mayai ya kwale pori. Tatizo wafugaji walishaanza kuwalisha madawa, hayakuwa tena dawa.
 
Ufugaji wa mbuzi wa maziwa, ufugaji wa sungura, kilimo cha Uyoga na kilimo cha matikiti maji
Vyote vilikuja kama upepo na kuondoka kama upepo
Ila bora hata hivi ulivyovitaja utaweza kula mwenyewe kama umefanya kwa kiasi na si biashara kubwa
 
NAKUMBUKA MTAJI KAMA LAKI SABA ULIKUFA.
 
Waliyapa promo sana hayo mayai ni booster Mara 3 zaidi ya mchuzi wa pweza.....watu wameyala mpaka basi lakini holaaa! Jogoo hapandi mtungi kikamilifu na raundi moja ikimalizika mtu anahema kama punda..watu washarudi zao kwenye michuzi ya pweza
 
Bro Tulimumu utashangaa sanaaaa!!!!! je umesahau kikombe cha "BABU" vipi kuhusu mihogo mibichi na karanga,vipi kuhusu etc etc!!! wengi wetu wamekuwa watu wa kufuata mkombo tuuuuu!!.Hivi sasa ni kumuunga mkono mtukufu ndio ina trend, chambilecho"Hili nalo litapita"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…