Hivi Boka ana kipi cha ziada kumzidi Romalisa?

Hivi Boka ana kipi cha ziada kumzidi Romalisa?

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Hivi Boka ukiachana na miguu yake mirefu , kunyoa ndevu zake kama Sadart yule muimba bolingo wa bendi ya Fmacademia na mbio zake zisizo na plani kama yule nguruwe pori maarufu kwa sasa kama kasongoye, ana kipi hasa cha ziada kumzidi Romalisa mtambala?

Yaani jamaa anaweza akapanda na mpira kwa mbio za ajabu lakini atakapo fika eneo analo takiwa kupiga kurosi kitu atakacho kifanya wote mtabaki kinywa wazi.

Kiufupi jamaa hana utulivu na papara nyingi sana.
 
Valentino Mashaka hadi sasa ni bora kuliko Prince Dube kwa idadi za mechi walizocheza. Turudi kwenye mada Kibabage au Farid ana impact kwa timu kupata matokeo chanya kuliko mkimbia marathon.
 
Boka anaujua mpira
Ana skills za hatari
Ana kasi
Ana nguvu
Anakaba Kwa wakati
Ana umri mdogo
Labda kwa upande wa umri unaweza ukawa na hoja lakini kwa upande wa uwanjani sidhani kama uko sahihi.

Boka ana faida kwenye kulinda tu lakini kwenye kushambulia hana impact yeyote ile zaidi ya kubutua mipira hovyo na krosi zake zisizo na macho ,ukilinganisha na Lomalisa ambaye alikuwa na faida sehemu zote mbili na alikuwa anafanya mambo yake kwa utulivu.
Mpira wa kisasa unamuhitaji beki kama Lomalisa kuliko Boka.
 
Boka amecheza mechi takribani 5
Umemlinganisha na lomalisa aliyecheza Yanga miaka 2
Hii timu ni mpya, nchi ya ugenini, lugha inamsumbua, ana upweke
Yule ni binadamu
Mpe muda basi hata mwaka mmoja ndo umlinganishe na lomalisa
Ana mengi anaweza kuboresha
 
Atakuwaje mpweke wakati kuna wakongo wenzake pale yanga? Kwa idadi ya mechi alizo zicheza zinatosha kujua ni mchezaji wa aina gani.
 
Atakuwaje mpweke wakati kuna wakongo wenzake pale yanga? Kwa idadi ya mechi alizo zicheza zinatosha kujua ni mchezaji wa aina gani.
Haya mkuu
Naheshimu mawazo yako
 
Boka amecheza mechi takribani 5
Umemlinganisha na lomalisa aliyecheza Yanga miaka 2
Hii timu ni mpya, nchi ya ugenini, lugha inamsumbua, ana upweke
Yule ni binadamu
Mpe muda basi hata mwaka mmoja ndo umlinganishe na lomalisa
Ana mengi anaweza kuboresha
Huyo Lomalisa anayesifiwa tulikaa naye miezi kadhaa hadi kuja kueleweka na kukubalika. Ilifika hatua Kibwana Shomari akawa preferred kuliko Lomalisa. Alipokaa sawa leo ndo tunayasikia haya. Achana na mashabiki maandazi
especially from Koloz ambao mechi tano tu kwao msimu umeshaisha na conclusions kibao.
 
Back
Top Bottom