Hivi Cardinal Pengo ni Mtanzania?

Bluray,

..Hafif alikuja hapa jamii forums kuomba msaada wa tende apeleke "kwao" Rufiji.

..sasa sijui kama amemaliza kusambaza hizo tende, mpaka aje kung'ang'ana na masuala ya uraia wa Kardinali Pengo.

..unajua watu wengine wanajitafutia maumivu ya kichwa bila sababu yoyote ya msingi.
 
Naona watu wanamfukuza mwizi wa nguo zao wakiwa Uchi!.. Sijui nani kati yao mwenye akili timamu..
 

Damn! Ama kweli Zee la kufuturisha HM Hafif atakuwa kazidiwa swaumu. 😀
 
Wenye wivu na roho ya husda wajikaange kwa mate yao na damu ya mafisadi!Pengo ni mtanzania halisi wa kuzaliwa na mzalendo!
 


Sijamwona kwenye list hii Zawadingoda na Kanda2!!!!!!


kwa wakatoliki na wasio wakatoliki ni kweli kuwa polkarp kardinal pengo ana urai wa nchi mbili yaani vatican state na tanzania, kuna mikataba mingi ya kuhusu vatican state au holy see, leo nina haraka nitaweka bandiko hapa kumjibu mwenye hoja

Na urudi uj utetee uzushi wako. Ati una haraka kusema passport yake ya Vatican ni namba hii aliyoipata mwka fulani vivyo hivyo ya Tanzania inahitaji muda gani?
 
Aaah, Kaaaazi kweli kweli! Basi inatosha jamani, walau tupunguze ukali wa lugha.
 
Mimi nina hofu. Kumbukeni Rais wa CCM kasema bado kuna muda wa kushughulikia Waraka wa Wakatoliki. Anapanga kuushughulikiaje?

Hofu yangu ni kwamba CCM inapanga kampeni chafu dhidi ya Viongozi wa Kanisa Katoliki. Tunaweza kupuuza huku kuulizia uraia wake, lakini kuna watu wabaya kwelikweli ndani ya CCM. Nina hofu kubwa kwamba wanapanga sasa kampeni dhidi ya Kardinali Wetu. Nasali isiwe hivyo.
 
Hahaaaaa
Kundi maslahi mna hali mbaya sana mwaka huu

Kumbe mna ugando namna hiyo vichwani mwenu? Sasa naanza kuelewa kwanini Mengi alipingwa na waislamu kina Lipumba,Sofia Simba,JK,...alipotoa yale majina yake.

Give me a break
Sofia Simba si muislam. kwa hiyo ndio maana Mengi anatoa misaada yake kanisani ili kuwakomoa waislam? una maana MENGI kutembea na kundi la kina Mwakyembe,Sitta na Seleli analifadhili kundi hilo kwa misingi ya ubaguzi wa kidini?
 

Mimi nimeanza kuogopa mwelekeo wa serikali ya Kikwete. Soon watu wataanza kupotea kama ilivyokuwa wakati ule - Kabeho, Kibona, Rutihinda, na Katabalo, mkemia mkuu wa serikali, na wengine wengi.
 
Nimesikitishwa saana na wengi wa watu kutoa mfululizo wa matusi kwa muuliza suala.

hakika kama mtamsoma vizuri muuliza suala amebainisha nini wasi wasi wake kuhusu uraia na ameweka katika mfumo wa suala na sio habari.

Mimi nilitegemea wengi etu tungetumia muda wetu mwingi kumjibu suala lake na kuondoa wasiwasi wake lather than kumtusi bila kumpa jibu. Kiuandishi kufanya hivyo ndio kuzidi kutilia mashaka na hatimaye kujenga chuki miongoni mwenu.

Ammi Hafif.

Suala lako ni zuri sana na lina msingi mkubwa sana kwa wale wenye upeo mkubwa na ni challenge kwa watungasheria huko Tanzania na wanasheria pia lakini hata wananchi wenye kufatilia mustakabali wa siasa za tanzania.

Kifupi ili kupata jibu lazima tuzifafanue

Mosi:sheria za Kimataifa zinazohusu haki za mwananchi hususan kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa juu.

Pili kuangalia sheria za Tanzania zinazobainisha Haki ya mwananchi katika kuchagua au kuchaguliwa Uongozi wa juu.

tatu. Sheria za Uraia za Tanzania.

Nne. Sheria za vatican ( za uraia na haki za kiuongozi kuchagua ima kuchagulia.

Kwa upande wangu nitazifafanua sheria za Kimataifa na zile za Tanzania. lakini sina uwezo kuzieleza sheria za kanisa katoliki kwani sijazipitia .

Kwani hata ukisoma International laws utaona vatican mnaiacha upande mwingine kwani haifungamani na sababu kuu za kuwa hivyo ni

1. Ni nchi ndogo kabisa Duniyani yenye idadi ndogo ya watu( Ina watu wasiozidi 600)
2. Asilimia zaidi ya 98 ya raia wake wanaume
3.Nchi yenye balozi (wawakilishi)zake kwenye nchi mbalimbali duniyani lakini hakuna hata nchi moja Duniyani yenye ubalozi wake ndani ya Vatican.
4. Nchi ambayo inaruhusu raia wa nje wanakuwa viongozi wake wa juu
5. wawakilishi wake a kibalozi lazima wawe maaskofu.

nasherehekea Eid lakini nitaeleza baada ya sikukuu.

nawatakia Eid Mubarak
 
Swaumu hufanya ubongo wakati mwingiene kushindwa kufanya kazi....upuuzi huu...!
Siyo wakati mwingine kaka........ Ila ni wakati wote, ile ni njaa tu ila inaitwa kwa jina jingine (la kidini). Mwenye njaa kufikiri ni tatizo.
 


Kwa Hakika Bi Nasriyah nimefarijika sana kwoko wewe kama mwandishi wa habari uliyobobea na mwanasheria uliotopea na uliyemakini sana katika kazi zako kuona watu walivyo wapuuzi ndani ya barza hii. wao kazi kutukana bila kuwa na hoja.

Mimi nipo na nasubiri jibu na ufafanuzi wako mwanasheria ili utoe funzo kwa hawa wazembe wanaotukana hapa.

Nawatakia Idi Njema.
 

Mimi siyo Mkatoliki hivyo Pengo siyo kadinari wangu, lakini nasema kama CCM watafanya kampeni mbaya dhidi yake huo ndo utakuwa mwisho wao. Pengo hajafanya jambo lisilo la kizalendo hivyo anasupport ya wananchi most of them are CCM. Hao CCM tumeshuhudia wakifanya madudu toka tupate uhuru. Wananchi wanaona bora kuitosa CCM na siyo maneno ya busara ya Mhe. Pengo.

Tatizo lililopo hapa wapinzani wa ukristo wamejificha nyuma ya CCM na kuendeleza mipango yao ya kupinga ukristo na Kristo. Hawa ndo akina barubaru. Ukitaka kuona hili chunguza post zote za huyu barubaru.

Halafu hawa watu waliojificha nyuma ya CCM wengine si CCM, hivyo kuporomoka kwa CCM wao hakuwahusu. Tena wanaweza kupiga jiwe moja ndege wawili yaani kuiangusha CCM na kupinga Ukristo.
 
Kwa taarifa yako Makadinali wote ni raia wa vatican na wanabaki kuwa raia wa nchi zao. kama mlifanya mchezo mchafu wa Uraia kwa Jenerali Ulimwengu jaribuni kwa Pengo muone cheche..The guy is smart, intelligent na hamlambi mtu miguu. Nukta
 
Gaddafi: I heard pengo siyo mtanzania
Mongella: Naona swaumu inakusumbua sana wewe

 

Unajiita "Mwanasheria wa Kimataifa" lakini ni wazi kutokana na maandishi yako hapo juu kwamba hujui hata kidogo tofauti iliyopo kati ya "Vatican City" na "Holy See".

Hebu tafadhali naomba utufafanulie maana ya "Vatican City" na "Holy See" na tofauti za kisheria kati ya mamlaka hizi mbili? Vitu vimewekwa wazi kwenye Wiki kwa kila mwenye kutaka kufahamu aelewe lakini bado tu Mmanga unaongopea watu na "utaalam" wako feki wa "Sheria ya Kimataifa" unaodai kuwa nao?! Ni aibu tupu!!
 
Dah! Kuna njia nyingi kweli za kutoa ushauri, ila hii twaweza ita njia kandamizi
 
hafif - pengo kupiga kura vatican sio tatizo kwenye uraia wake, kwa wa TZ walioshawahi kukaa UK watakueleza; raia yeyote wa commonwealth anaruhusiwa kupiga kura UK na hata mimi na wa TZ kibao tumeshapiga kura UK
 
hafif - pengo kupiga kura vatican sio tatizo kwenye uraia wake, kwa wa TZ walioshawahi kukaa UK watakueleza; raia yeyote wa commonwealth anaruhusiwa kupiga kura UK na hata mimi na wa TZ kibao tumeshapiga kura UK
.

Semilong je wewe unaweza kugombea kuwa waziri mkuu wa UK.

Elewa haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa juu.

Wewe unaongelea kuchagua na si kuchaguliwa. tafakari hilo.
 
.

Da Dede. Hivi kweli unajua unaongea kitu gani.

Hivi unajuwa Pope ni kiongozi wa hanisa katoliki Duniani na kiongozi wa nchi...?

Je tanzania kuna ubalozi na mwakilishi wa holy see au wa Vatican?

hebu jaza hapo nikupe max.

usichanganye mamlaka bwana na kubatilisha mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…