Hivi CCM bado chama cha wakulima na wafanyakazi? Polepole alikidhalilisha chama

Hivi CCM bado chama cha wakulima na wafanyakazi? Polepole alikidhalilisha chama

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
CCM ilipo asisiwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi. Ndio maana nembo yake kwenye bendera kuna nyundo kwa wafanyakazi na jembe kwa wakulima.

Filosofia ya CCM ni ya kiujamaa pamoja na kuukaribisha uchumi wa biashara huru.

Siku hizi ndani ya CCM hakuna Political Theorists wa kuelezea mlengo na muelekeo wa Filosofia ya chama.

Hapo katikati tumepata wapiga debe wa hovyo kabisa ambao hawajawahi tokea kwenye chama. Tulikuwa na kina Prof Mbwiliza , Bismark Mwansasu ,waliowiva toka Chuo cha CCM wakati huo Kigamboni. Sasa tukaishia na kina Polepole wapiga debe wa kijinga kuwahi tokea ndani ya CCM.

CLIP ya mavieitee ndio niliona CCM ya Mwalimu imeisha kabisa, maana kiitikadi Polepole hajui anaongea nini.

Pole CCM ya Mwalimu.
 
Hawa ni baadhi ya wanachama wake waandamizi Rostam na Dewji mabwanyenye wa Viwanda, Kimei banker, Shabiby na Abood mabwanyenye wa sekta ya usafiri, Kigwangala bwanyenye wa Kilimo,
 
Hatuwezi katu tukaishi na theory za kijima wakati muda wake umeshapita. Tanzania ile ya Nyerere ilikuwa ni kama gariinayoanza kuondoka ,huanza kwa mwendo wa pole pole( gia No.1 kisha huingia No 2 kisha Huingia 3 Sa Kwa sasa Tanzania iko kwenye Mwendo kasi mno kuelekea kwenye Uchumi wa kati, Watanzania wengi leo wnamiliki ,Baskeli, Pikipiki na Magari .Zma zile ilikuwa sanasana unaweza kumiliki gari la Punda.

Sasa huo ujamaa mnaoudhania kuwepo kwa sasa ni kitu ''In compatible'' kwa zama za Globalisation. Acheni gari lienge kwa mwendo kasi wakati Bara bara ni nyeupe bila mashimo.

Hongera Mama Samia, Kaza Mwendo tuwahi kufika. siku hizi ''Time is money''
 
Hatuwezi katu tukaishi na theory za kijima wakati muda wake umeshapita...
Sorry lakini nafikiri nikuite mtoto.

We mtoto hujaishi miaka ya kutosha kujua tulikotoka.

Uchumi unaouona leo msingi wake ni late 60s na70s.

Mwalimu alijenga viwanda zaidi ya 400 strategic, Mkapa akaviuza.

Kama ni magari ya punda hata leo yapo, nenda Bariadi uone wakulima wanasafirishia nini pamba.

Hatuwezi kurudi kule tulikotoka 100%, ila usipojua ulikotoka hata kule unakoelekea si ajabu ni kizungumkuti.
Nyie ndio watoto rika la Polepole Mavieite.
 
Hawa ni baadhi ya wanachama wake waandamizi Rostam na Dewji mabwanyenye wa Viwanda, Kimei banker, Shabiby na Abood mabwanyenye wa sekta ya usafiri, Kigwangala bwanyenye wa Kilimo,
Kwa hiyo ukisha kuwa bwanyenye ndo umepoteza haki ya kuwamwanaChama? Hivi,twendelee kuwa wakulima maskini ili tupate uhalali wa kuwa wanachama?
 
ccm sasa hivi ni chama cha watoto wa mjini. wapigaji, wakwepa kodi, wauza unga.
 
CCM ilipo asisiwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi.
Ndio maana nembo yake kwenye bendera kuna nyundo kwa wafanyakazi na jembe kwa wakulima...
Watu wasio na nia njema na CCM walijaribu kukigeuza chama kuwa eti ni cha wanyonge na masikini ili kutimiza malengo yao kisiasa.

Unyinge na umasikini ndio adui wa kuteketezwa toka enzi ya kupata uhuru.

Lakini wanyonge na masikini kwa context ya chama hawajawa defined.
 
Ccm bado ni chama cha wakulima na wadanyakazi?
Kwa hiyo ukisha kuwa bwanyenye ndo umepoteza haki ya kuwamwanaChama? Hivi,twendelee kuwa wakulima maskini ili tupate uhalali wa kuwa wanachama?
 
Kwa hiyo ukisha kuwa bwanyenye ndo umepoteza haki ya kuwamwanaChama? Hivi,twendelee kuwa wakulima maskini ili tupate uhalali wa kuwa wanachama?
Ati kuwa mkulima ndiyo uwe masikini?
Mtazamo huo ni wa ujima.
Rais Carter, mkulima wa karanga, alikuwa tajiri na akawa rais wa Marekani.
We must think big.
 
Back
Top Bottom