Hivi CCM hawaoni aibu jinsi kampeni zilivyopooza halafu hakuna anayefuatilia?

Kuboma

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
1,466
Reaction score
2,581
Kweli binadamu akilitaka lake jambo huwa haoni aibu.

Hivi CCM mmekosa kweli washauli, heri mngebaki na uzoefu wenu wa kuiba kura lakini siyo kwa kampeni mnayoifanya isiyokuwa na mvuto, yaani mmechokwa mnajaribu kujilazimisha kucheka nafsi inawasuta, hamna furaha, uchaguzi umepoa, hakuna anayefwatilia.

Wagombea wenu walikuwa wanapewa umaarufu na wagombea wa Chadema, lakini sasa hawajulikani, hamna anayewafwatilia, yaani ule mchuano uliokuwa unafwatiliwa mfano mgobea fulani wa Chadema vs fulani wa CCM hamna hiyo tena.

Naamini huu ndiyo utakuwa uchaguzi wa ovyo kabisa kuwahi kutokea toka vyama vingi vianze
 
Leo nilisema ngoja niangalie kampeni dah kwakweli mbingu na ardhi yaani dah bira hela wangefanyia mambo mengine ya kuinua taifa.
 
Wenyewe wamejiita viziwi,unafikiri kuna kusikilizana au hata kuelewana?
 
Kwa mara ya kwanza sifatilii hii kitu inaitwa uchaguz habar nakutana nazo kwenye viredio vya fm tu kwa bahati mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…