Hivi dhamana inatolewa palepale mahakamani?

MWINUKAOSCAR

Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
40
Reaction score
1
Hivi wanaposema dhamana labda ya sh milion 20. Huwa unatakiwa utoe hiyo hela cash pale pale au la. Mana huwa tunagombana hasa humu vtuo vdogo vya polisi
 
Ndo maana ya dhamana ni lszima utoe cash kwa maana nyingine dhamana ni mbadala wako wewe
 
Hivi wanaposema dhamana labda ya sh milion 20. Huwa unatakiwa utoe hiyo hela cash pale pale au la. Mana huwa tunagombana hasa humu vtuo vdogo vya polisi
either of them, unaweza kuamua kutoa hela cash kesi ikiisha utarudishiwa zote, au ukatoa bondo ya maneno ya mdomo yakisindikizwa na hati ya mali kulinganana mahakama iliivyotaka. kwa uzoefu, wengi hupenda mali zisizohamishika iletwe hati yake, kesi ikiisha utarudishiwa hati yako. inategemeana na makosa, mengine madogomadogo hayahitaji hata kudeposit hati kabisa (hasa yale yenye dispute yenye thamani chini ya 10m)...ila ukiona una kosa lililotokana na mgogoro wenye thamani zaidi ya ten m, lazima hati. mfano, mtu ameiba milioni 20, hapo lazima udeposit cash nusu au yote, au utoe hati ya mali isiyohamishika inayosindikizwa na maneno ya mdomo tu. mind you, wewe mdhamini unajikomit, mshitakiwa akikimbia mahakama inaweza kukufunga au ukalipa fungu la dhamana.
 
Asante sana... Kwa hiyo mwenye haki ya kusema nitoe hiyo dhamana ni mahakama tu au hata huku vituo vidogo vya polisi?
 
Asante sana... Kwa hiyo mwenye haki ya kusema nitoe hiyo dhamana ni mahakama tu au hata huku vituo vidogo vya polisi?
hahaaha, kuna dhamana za aina kama tatu, kuna dhamana ukikamatwa na polisi, hiyo wenye mamlaka ni polisi wenyewe. ukipelekwa mahakamani na kusomewa mashitaka ile dhamana ya polisi imeshafia kulekule, pale unaanza dhamana mpyaaa ya mahakama. unaweza kufungwa na haujaridhika baadhi ya makosa ukaomba dhamana ukisubiria rufaaa. kwa ufupi ukiona umeshafika mahakamani mwenye mamlaka ni mahakama tu, polisi wewe sio mtu wao, watakachokuwa wanafanya ni kukuleta mahakamani na kukurudisha rumande tu hawana nguvu nyingine kwako zaidi ya hiyo, ila mahakama.kuna kitabu cha dhamana tumeandika, kizuri sana ni cha kiswahili,
 
Asante sana...kipo madukani hicho kitabu? Na ile dhamana kwa upande wa polisi unakatiwa risiti kama ni sehem ya mapato ya serikali? Mana huku vtuo vidogovdogo hawatoi hati za malipo wao wakshachukua ndio imeishia hapo.
 
dhamana haununui kitu, hela utakayoweka utarudishiwa yote, ni dhamana tu, hauwapi hela wakaile.at the end of the day its still your money and you will need to collect it back.
 
Asante sana...kipo madukani hicho kitabu? Na ile dhamana kwa upande wa polisi unakatiwa risiti kama ni sehem ya mapato ya serikali? Mana huku vtuo vidogovdogo hawatoi hati za malipo wao wakshachukua ndio imeishia hapo.
kitabu kipo madukani, hadi naogopa kutaja duka hapa manake niliweka link hapa wakaniban kwasababu nimespam. ngoja tu niwaache...au njoo pm
 
Pia kuna utaratibu Wa aina nne (4) Wa dhamana.

1.Dhamana ya Cash.

2. Dhamana ya Maneno (Bond)

3.Dhamana ya kuweka Mali au hati

4. Dhamana ya kujidhamini mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…