Hivi Diamond anaweza kukaa mwaka bila kutoa wimbo harafu asisahaulike kwenye ulimwengu wa muziki?

Nibozali

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2016
Posts
572
Reaction score
1,055
Kama ilivyo kwa baadhi ya wanamuziki ambao wanaweza kutoa wimbo na baadae kukaa mwaka mzima bila kutoa nyimbo zingine na bado hizo walizotoa zikaendelea kuwaweka kwenye ulimwengu Wa muziki wasisahaulike, je kwa aina ya Muziki na quality ya vibao vinavyotolewa na Diamond, anaweza kutoa kibao na kukaa mwaka mzima bila kutoa wimbo mwingine na bado nyimbo hizo alizotoa before zikaendelea kumwakilisha vyema na kumfanya asisahaulike kwenye gemu?
 
Akikaa miezi sita tu watu wataanza kujiuliza hv alikuwepo mtu kweli?
 
Hakuna msanii asitoe nyimbo mwaka mzima halaf awe tu anasikika haiwezekani. Na hata ikiwezekana basi mtu huyo atakuwa diamond kwanini kwa sababu ana fan base kubwa na ana mauzo makubwa. Naamini diamond hata asipotoa nyimbo mwaka mzima bado atauongoza mauzo katika mwaka huo aliokaa kimya kwa kuuza nyimbo zake za zamani
 
Mbona Kingwendu na miaka 3 bila wimbo ila yupo vizuri kisanaa.
 
Reactions: rr4

hawezi, yeye anabebwa na miziki ya wiki mbili na story za ufuska
 

kiba anaweza
 
wewe ni mhimili wa shetani, how dare you unamuwazia mabaya mwenzio hivyo,wakati wewe hata kuimba wimbo wa mstari mmoja huwezi.
 
Sasa hivi anatoa nyimbo mfululizo ila upepo hamuendei vizuri.
 
!wewe unaenda kazini kila siku ila mondi kutoa muziki kila .mwezi unakunja
 
Hivi lizaboni alikuwepo kweli? Maana naona siku hizi hasikiki tena na wenzie lumumba fc wakiambatana na laki si pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…