Hivi Diamond anazungumza na sisi au na Harmonize?’

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Inawezekana kinachozungumzwa na wengi kuwa Mkurugenzi wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz hajapendezwa na kuondoka Harmonize kuondoka kwenye lebo hiyo kuna ukweli.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na minong’ono kuwa wawili hao hawapo karibu na hawana mawasiliano kabisa hasa baada ya Harmonize ambaye Diamond alimkuza kisanii kuomba kujitoa kwenye lebo hiyo, akionekana kama hana shukurani baada ya mambo yote aliyofanyiwa ikiwamo kukuzwa kisanii lakini ameamua kutemana nao.
Kauli hiyo imeonekana ina mashiko kutokana na kile kilichosemwa na Diamond mara baada ya kukabidhiwa ubalozi wa kampuni ya Bomet inayozalisha sabuni ya unga ya Niceone, kuwataka vijana wakumbuke walikotoka.
“Kijana kumbuka sehemu uliyotoka na kumbuka na kuwaheshimu watu waliokuwezesha, mimi nisingeweza kufika hapa bila mameneja wangu na Watanzania ambao ni mashabiki wangu, nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwapenda,”
“Naamini kila kijana ameandikiwa fungu lake kwenye maisha na hakuna mtu anaweza kukushusha au kukuzibia riziki yako cha muhimu ni kufanya kazi na kumuomba sana Mungu,” alisema.

Licha ya kutomtaja mtu, kauli hiyo ilizua minong’ono kuwa inawezekana anamfikishia ujumbe huo Harmonize.
Ikihusishwa na mchuano kati yao unaoendelea mtandaoni ambapo Septemba 22, 2019 zilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Diamond akiwa Uwanja wa Taifa wakati wa uzinduzi wa tamasha la utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest), akionekana kazungukwa na vijana wengi wakimshangilia na kumwimbia.
Kesho yake Harmonize naye akaweka video inayomuonyesha akiwa kwenye uwanja huo siku ya mechi ya Taifa Stars na Burundi, ambapo naye alizungukwa na kundi la vijana kama ilivyokuwa kwa bosi wake wa zamani.
Mbali na hayo Diamond aliwakumbusha vijana kuwa ili kufikia mafanikio kama yake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
“Unaweza kuniangalia ukanichukulia poa, nitolee mfano jana kuanzia asubuhi nilikuwa narekodi video hadi asubuhi ya leo, nimejiegesha saa chache nagongewa mlango niende kwenye miadi ubalozini, nimetoka huko safari ya kuja hapa Kilimanjaro Hoteli ikaanza unaweza kuona ni jinsi gani natumia muda mwingi kufanya kazi,”
“Kwangu muda huu wa ujana ndiyo wa kufanya haya ninayoyafanya, hivyo kijana yeyote anayependa muziki na anatamani kuwa na mafanikio kama mimi akubali kulala uzeeni, kupumzika uzeeni,” alisema Diamond.
Alisema mafanikio hayaangalii kazi, hivyo vijana popote pale walipo bila kujali wanafanya kazi gani, wasikubali kuchoka kabla hawajafanikiwa.

Mwananchi
 
Je ilikuwa dhambi Harmonize kuweka clip kama alivyofanya Diamond?

Tusiwachonganishe hawa vijana. Tuwasapoti wafikie manono yao na si kuwafarakanisha!
 
Wasafi wanajichanganya sana, walisema Harmonize ameondoka kwa kuaga na uongozi umempa baraka zote huko aendako lkn sasa hivi wanaongea vitu kama vile Konde ameekimbia.
 
Tatizo kubwa la wanahabari wetu wakiwa hawana story watatafuta tu story kwa ulazima hata kama Haina connection imradi tu story yake iuze na hili suala wanaloendelea kulifanya litamwathiri Sana harmonize cos Hana fans kubwa kama ya diamond so fans wa diamond watamchukia harmonize lakini pia itamfanya hata diamond aanze kujuta uwekezaji alioufanya kwa harmonize hata kama Hana hili wazo kwa kujazwa na waandishi uchwara na mashabiki maandazi.
 
Nyani haoni kundule mbona yy hakukumbuka na alivyofanyiwa na marehemu Ruge Mutahab
 
Wasafi wanajichanganya sana, walisema Harmonize ameondoka kwa kuaga na uongozi umempa baraka zote huko aendako lkn sasa hivi wanaongea vitu kama vile Konde ameekimbia.

Nasikia anataka kulipishwa milioni 800
 
Diamond kasema ujana kazi kupumzika uzeeni. Mnachoona ni bifu tu. Mwenzenu anaingiza hela, swine !!!
 
Inawezekana kinachozungumzwa na wengi kuwa Mkurugenzi wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz hajapendezwa na kuondoka Harmonize kuondoka kwenye lebo hiyo kuna ukweli.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na minong’ono kuwa wawili hao hawapo karibu na hawana mawasiliano kabisa hasa baada ya Harmonize ambaye Diamond alimkuza kisanii kuomba kujitoa kwenye lebo hiyo, akionekana kama hana shukurani baada ya mambo yote aliyofanyiwa ikiwamo kukuzwa kisanii lakini ameamua kutemana nao.
Kauli hiyo imeonekana ina mashiko kutokana na kile kilichosemwa na Diamond mara baada ya kukabidhiwa ubalozi wa kampuni ya Bomet inayozalisha sabuni ya unga ya Niceone, kuwataka vijana wakumbuke walikotoka.
“Kijana kumbuka sehemu uliyotoka na kumbuka na kuwaheshimu watu waliokuwezesha, mimi nisingeweza kufika hapa bila mameneja wangu na Watanzania ambao ni mashabiki wangu, nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwapenda,”
“Naamini kila kijana ameandikiwa fungu lake kwenye maisha na hakuna mtu anaweza kukushusha au kukuzibia riziki yako cha muhimu ni kufanya kazi na kumuomba sana Mungu,” alisema.

Licha ya kutomtaja mtu, kauli hiyo ilizua minong’ono kuwa inawezekana anamfikishia ujumbe huo Harmonize.
Ikihusishwa na mchuano kati yao unaoendelea mtandaoni ambapo Septemba 22, 2019 zilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Diamond akiwa Uwanja wa Taifa wakati wa uzinduzi wa tamasha la utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest), akionekana kazungukwa na vijana wengi wakimshangilia na kumwimbia.
Kesho yake Harmonize naye akaweka video inayomuonyesha akiwa kwenye uwanja huo siku ya mechi ya Taifa Stars na Burundi, ambapo naye alizungukwa na kundi la vijana kama ilivyokuwa kwa bosi wake wa zamani.
Mbali na hayo Diamond aliwakumbusha vijana kuwa ili kufikia mafanikio kama yake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
“Unaweza kuniangalia ukanichukulia poa, nitolee mfano jana kuanzia asubuhi nilikuwa narekodi video hadi asubuhi ya leo, nimejiegesha saa chache nagongewa mlango niende kwenye miadi ubalozini, nimetoka huko safari ya kuja hapa Kilimanjaro Hoteli ikaanza unaweza kuona ni jinsi gani natumia muda mwingi kufanya kazi,”
“Kwangu muda huu wa ujana ndiyo wa kufanya haya ninayoyafanya, hivyo kijana yeyote anayependa muziki na anatamani kuwa na mafanikio kama mimi akubali kulala uzeeni, kupumzika uzeeni,” alisema Diamond.
Alisema mafanikio hayaangalii kazi, hivyo vijana popote pale walipo bila kujali wanafanya kazi gani, wasikubali kuchoka kabla hawajafanikiwa.

Mwananchi
Diamond anaongelea mambo ya msingi yaliyomfikisha hapo alipo sasa, ww unaleta ukoro - show wako hapa, hujui kitu.
 
Nimesoma habari kina kwa kina, nukta kwa nukta, nimemuelewa Diamond hasa kwenye kufanya kazi kwa bidii, kwangu naona ni ujumbe mzuri kwa vijana waufanyie kazi.

Haya mambo tuyaache tu. Mtu anawezasema chochote ni juu ya wasikilizaji kuchagua watafsiri vipi au wachukue kipi na waache kipi. Kwa upande wangu sijaona uchonganishi wowote nikirejea hii habari iliyowekwa hapa kutoka gazeti la mwananchi.
 
Wasafi wanajichanganya sana, walisema Harmonize ameondoka kwa kuaga na uongozi umempa baraka zote huko aendako lkn sasa hivi wanaongea vitu kama vile Konde ameekimbia.
Huyu jamaa awe mpole....
dogo ametoka ameenda kuangalia ustaarabu wake akaushe tu.....
sio kila siku habari hiyo hiyo...
ataonekana mchawi sasa!!...
roho imemuuma kweli....
Mm mwenyewe mwalimu aliyenifundisha kusoma nimempiga gap mbaya kabisa...
kutangulia sio kufika......
 
Back
Top Bottom