Hivi elimu yetu hapa Tanzania, inatuendeleza kifikra au inatudidimiza?

kamtesh

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,395
Reaction score
513
Let's be objective on the matter as we contribute kwaajili yaawndeleo ya nchi yetu. Angalieni wahitu wa kidatu cha nne na cha sita, na linganisha na muhitimu wa the same daraja kutoka nchi jirani ie. Zambia, Uganda, Kenya makadharika, tumekwama wapi? Ebu angalieni, mtoto form four au six, acha english, hata masomo mengine, unashangaa anvyo jieleza. Asilimia kubwa wanakua hawawezi kabisa kujieleza hata kujitambua. And these are wapiga kura watarajiwa. Tatizo liko wapi? Wachina wako mbele kwahio tatizo sio English then, so then what is it?
 
Elimu ni uwekezaji kama ulivyo mwingine wowote. ...faida ya uwekezaji wake inategemeana kwa kiasi kikubwa na kiwango cha mtaji wake....tukitaka kutoka hapa tufike mahali mwananchi ndiye amwambie mwanasiasa amfanyie nini na sio mwanasiasa ndo amwambie mwananchi atamfanyia nini....hapa namaanisha kuwa tuachane na ilani za vyama tuwe na ilani ya taifa ambayo inakuwa mkataba kati ya mwananchi na serikali, tukifikia hapo tutaweza kutoa sharti la anayetaka ridhaa ya wananchi awe yuko tayari kuwekeza kwenye elimu si chini ya asilimia 10 ya pato la taifa....kwa kufanya hivyo automatically maprofesa hawatakimbilia siasa inayolipa kwa sasa badala yake watasalia kwenye kufanya tafiti na kufundisha watu wetu na wenye digrii watafundisha shule za msingi. ...tofauti na sasa vilaza ndo wanakimbilia ualimu.
 
Kuna tatizo, si kwa wahitimu tu hata wafanyakazi. Linganisha utendaji wa kazi wa watu kutoka nchi hizo utaona.tofauti.

Nadhani exposure ya tz bado iko chini, na watu hawako aggressive katika kujiendeleza.

Hebu mtizame mnigeria hata ambaye hakwenda shule, anaweza kukushangaza.
 
Mtoto anatumia muda mchache shule kuliko nyumbani except wa boarding!!!!

Wewe kama mzazi role yako ni ipi katika kuhakikisha mtoto wako anakuwa vile ungependa awe???!!!

Unarudi umelewa, ugomvi nyumbani, mida wote kwa vimada, watoto hata weekend hutoki nao japo site tu wajue a b c za hapo???!!! Unataka exposure waitoe kwa walimu na vitabuni??!!

Nakumbuka mzee alikuwa anakupa gazeti umsomee ye kakaa tu kazi yake kukutwanga mwaswali lakini kumbe ilisaidia comprehension!!!!

Wazazi tuchukue majukumu kwanza then elimu itafundisha taaluma, hivi wazazi wangapi wana wall chats za rangi, utambuzi,namba, maumbo majumbani kwa watoto wadogo na wanafundisha hivyo vitu???!!!!!

Utalaumu serikali lakini mtoto anabaki kiwa wako!!!!

snowhite, Ennie, King'asti, BadiliTabia
 
Last edited by a moderator:
Ccm....................ni tatizo.....................................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…